MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Katiba itambue Kiswahili kuwa Lugha ya Taifa

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Katiba itambue Kiswahili kuwa Lugha ya Taifa
#1
[Image: katiba.jpg]
Mjumbe wa Tume ya Katiba, Mohamed Yusuf Mashamba akifafanua jambo wakati wa ukusanyaji wa maoni katika Kijiji cha Kitere, Halmashauri ya wilaya ya Mtwara mkoani hapa juzi.Kushoto ni Mjumbe mwingine wa Tume hiyo, Dk.Sengondo Mvungi. Picha na Abdallah Bakari
Kwa ufupi
“Wenyeviti wa vijiji, vitongoji walipwe mishahara, wazee umri wa miaka  60 walipwe posho ya uzeeni kila siku” alisema Singa.
Abdallah Bakari, Mtwara
DIWANI wa Kata ya Ziwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, mkoani hapa, Mohamedi Mkiwa (72) amependekeza katiba ijayo itamke kuwa Kiswahili ndiyo lugha ya Taifa na shughuli zote za nchi zitaendeshwa kwa lugha hiyo.Akitoa maoni yake juzi mbele ya Tume ya Katiba ilipofanya mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi hao katika kijiji cha Madimba, Ziwani na Msangamkuu, diwani huyo alisema katiba ya sasa haitambui Kiswahili kama lugha ya Taifa.
Alisema kukosekana kwa kipengele hicho kunasababisha kupuuzwa kwa lugha ya Taifa na watendaji wa serikali wanaotumia lugha za kigeni katika shughuli za kila siku za utendaji wa serikali.
“Katiba itambue kuwa Kiswahili ni lugha ya Taifa na itamke wazi kuwa shughuli zote za kiserikali zitaendeshwa kwa kutumia lugha ya Kiswahili” alisema Mkiwa.
Aidha diwani huyo alipendekeza Rais kuongezewa madaraka kwa kuitwa Rais mtendaji badala ya sasa ambapo shughuli za kiutendaji zipo chini ya Waziri Mkuu.
Mkazi mwingine wa Ziwani Hassan Singa (76), alipendekeza viongozi wa vitongoji na vijiji walipwe mishahara kwa kuwa wanatumia muda wao mwingi kuhudumia wananchi.
“Wenyeviti wa vijiji, vitongoji walipwe mishahara, wazee umri wa miaka  60 walipwe posho ya uzeeni kila siku” alisema Singa.
Naye Mkazi wa Madimba,Abdallah Lina (54) alipendekeza siku ya kupiga kura wapiga kura wote walipwe posho kwa sababu wanatumia muda wa siku nzima kushinda kwenye foleni wakisubiri kupiga kura.
Maoni hayo yalihojiwa na Mjumbe wa Tume hiyo, Mohamedi Mashamba, aliyehoji iwapo haoni kwa kufanya hivyo wananchi watakuwa wameuza haki yao, swali ambalo lilijibiwa na Lina kuwa “Viongozi wamegeuza uongozi kuwa mtaji basi ni heri na sisi tukaambulia japo kidogo”
Mashamba alimweleza Lina kuwa iwapo maoni yake yatapitishwa kutakuwa na hatari kubwa ya nchi kutawaliwa na mafisadi, kwa kuwa wataweza kuwalipa wapiga kura.
Awali Mwenyekiti wa mkutano huo, Dk. Sengondo Mvungi  aliwataka wananchi hao kuwa wawazi kutoa maoni yao ili watunge Katiba itakayoondoa matatizo yao.
Mvungi alisema ni vema kwa wananchi wakaelewa kuwa Katiba waitungayo itadumu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo na kwamba ni muhimu matatizo yao wakayapa kipaumbele ili yapatiwe ufumbuzi na katiba yao.
“Katiba ndiyo maisha yako ya kila siku, sema unataka iweje, msiwe na hofu maoni yote yatachukuliwa, kwa maandishi, vinasa sauti na video” alisema Dk. Mvungi. Chanzo>>>>>
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)