MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

KIMTANG’ATA MJINI TANGA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
KIMTANG’ATA MJINI TANGA
#1
KIMTANG’ATA MJINI TANGA
Katrin Bromber
     1. Utangulizi
Mnamo mwaka 1955 Wilfred Howed Whiteley eneo kusini mwa mji wa Tanga ili kuchungua lugha iliyozungumzwa pale. Matokeo ya utafiti wake aliyahifadhi katika kijitabu chake KI-MTANG’ATA. A dialect of the Mrima coast – Tanganyika kilichotolewa mwaka 1956. Lunga aliyoifafanua katika kitabu hicho ni lahaja moja ya Kiswahili ya kusini ambayo ilifanana na lahaja nyingine za eneo hilo – hasa Kivumba. Whitely aliipa lahaja hiyo jina la Kimtang’ata kufuatana na kijiji cha Mtang’ata. Maelezo yake yanaonesha kwamba Kimtang’ata kilikuwa
kikizungumzwa pwani kati ya Mwambani na Kigombe. Aidha aligundua kwamba matumizi ya lahaja hiyo yanaendelea kupungua. Hasa ni wanawake ndio watumiaji wa lahaja hiyo (Whiteley 1956: 3-5). Zaidi ya miaka thelathini Derek Nurse na Thomas Hinnebusch walifanya utafiti wa kiisimu katika eneo hilo mara nyingine. Waliwakuta wazee wachache tu waliozungumza lugha iliyofanana na Kimtang’ata kilichofafanuliwa na Whiteley (Nurse na Hinnebusch, 1993: 521). Wote watatu walieleza kupungua kwa hadhi ya lahaja hiyo kwa ongezeko la matumizi ya Kiunguja. Waliendelea kusema kwamba sifa za lahaja hiyo huonekana katika kiwango cha kileksika zaidi kuliko viwango vingine vya lugha. Kwa vyovyote, matokeo ya uchambuzi mwingine uliofanyika mwezi wa tatu mwaka 1996 mjini Tanga yanaonesha hali tofauti kidogo. Wahojiwa walitumia sifa za kiwango cha mofolojia zaidi kuliko zile za kileksika.

Maelezo ya makala haya yanahusu Kiswahili kitumiwacho na watu ambao husafiri mara nyingi kati ya vijiji vya Mwambani na Tongoni, ambapo lahaja ya Kimtang’ata ilitumiwa wakati wa uchambuzi wa Whiteley, na mji wa Tanga. Sehemu ya pili inahusu mazingira ya uchambuzi. Sehemu ya tatu mpaka ya tano zinatoa maelezo juu ya sifa za kilahaja katika viwango vya fonetiki, mofolojia na msamiati. Makala inamalizia kwa kufikiria uhai wa Kimtang’ata.

      2.  Mahojiano

Mahojiano yalifanyika mwezi wa tatu mwaka 1996. Marehemu Mwl. Pera Ridhiwani, aliyeheshimiwa sana na watu wa Tanga na watafiti wa lugha na fasihi ya Kiswahili, alikuwa ameshafanya miadi na wanawake kutoka Mwambani na Tongoni. Mwl. Pera alimfahamisha mhoji na wahojiwa. Alihudhuria kila mahojiano lakini hakuingilia mwenyewe hata mara moja. Wahojiwa walikuwa wanawake wane wenye umri uliozidi miaka sitini. Walieleza kwamba husafiri mara nyingi kati ya vijiji vyao na mji wa Tanga ili kuwatembelea jamaa zao. Kawaida yao ya kusafiri ilipunguza uwezekano wa kupata “lahaja safi”. Zaidi ya hayo mhoji alizungumza Kiunguja tu na kuonesha kwamba yeye mwenyewe hajui kutumia Kimtang’ata.

Walipoulizwa kusimulia vigano katika lahaja ya Kimtang’ata wanawake hao hawakufahamu. Kutumia kwa neno la Kimtang’ata ili kutaja yao ya mama kilikuwa kigeni kwao. Hali hii ingeonesha kwamba wanawake hao hawakujua kwamba kilugha chao ni tofauti na Kiswahili kizungumzwacho mjini au Kimtang’ata kimeshakufa kabisa.
Mahojiano na wanawake kutoka Mwambani yalifanyika ndani ya nyumba bila ya kuhudhuriwa na watu wengine. Kila mmoja alisimulia vigano viwili bila ya kuingiliwa na mtu yeyote. Mfumo wa matini hizo ni wa usimulizi tu. Mahojiano na wanawake waliotoka Tongani yalifanyika hadharani katika ua wa nyumba ya jamaa yao. Hivyo wote waliotaka kusikiliza walipata nafasi hiyo. Wasikilizaji wa kike na wa kiume umri mbalimbali waliingilia masimulizi kwa kutoa  maoni yao ama juu ya habari zilizoelezwa au juu ya matumizi ya lugha. Zaidi ya hayo wanawake wawili hawa walifanana kihadhi na kitabia na kusahihishana waliposikia ulazima wa kufanya hivyo. Mahojiano yalitoa matini zenye sifa za masimulizi na za mazungumzo.
       3. Fonetiki
Tofauti za kifonetiki zilitokea nadra tu. Kimsingi ilitokea ukaakaishaji wa fonimu /k/ mbele ya fonimu /i/ katika upatanifu wa ngeli ya saba. Matini zinaonesha sifa hii katika vimilikishi tu. Whitely (1956: 18) alitaja kipengele hicho kwa kiambishi awali cha nomino pia.
(1) Kigano kyangu kikeshilia hapo. (Kigano cgangu kikeshilia hapo)

        4. Mofolojia
Sifa nyingi zaidi zilitokea katika kiwango cha mofolojia kuliko viwango vingine vya kiisimu. Katika kitabu chake Whiteley (1956: 22) alieleza juu ya mifululizo miwili ya viambishi awali kiima vya umoja. Mfululizo wa Kiunguja ni-, u-, a- hutumika sawasawa na mfululizo wa Kimtang’ata si-, ku-, ka- ambao pia hutokea katika lahaja ya jirani Kivumba. Matini za 1996 zinaonesha wazi matumizi ya mifululizo yote miwili. Kwa vyovyote,  mfululizo si-, ku-, ka- unaambatana na mahali timilifu. Whitely alitoa mifano ambapo mfululizo huo ulitumiwa pamoja na njeo zote nyingine.

1.    Baba sinarudi. Kunarudi, wee
(Baba nimesharudi. Je, umesharudi?)

2.    Yule bwana kanakaa juu ya kiti.
(Yule bwana amekaa juu ya kiti.)
Kwa vile mazungumzo yalinaswa sauti mifano ya mpumuo wa /kh/ ili kuonesha ukanushaji wa nafsi ya pili na tatu ya umoja yaliyotokea. Nurse (1982: 173) na Nurse na Hinnebusch (1993: 365) wanaeleza mifano kama (4) na (5) kuwa ukanushaji wa kimsingi na unyambuaji wa /*nka/.
(4) Ebu khuolo wakezo? (Ebu huoni wakezo?)

(5) Lakini kila apatacho kikubwa khakimtoshi wala kidogo khakimtoshi. (Lakini kila apatacho kikubwa hakimtoshi wala kidogo hakimtoshi.)
Zaidi ya hayo mfano (4) unaonesha tangamano irabu katika silabi ya mwisho wa kitenzi. Kwa namna hii ukanushaji unasisitizwa mara mbili. Tangamano irabu ilitokea mara moja katika matini simulizi tu lakini mara nyingi katika matini mazungumzo yenye kitenzi –ona (simwono – simwoni) na –oga (sogo – siogi). Kinyume cha lahaja ya kaskazini ambazo zinatumia mpumuo kwa kuonesha tofauti za kisarufi, kazi hii imepunguzwa katika lahaja za kusini. Hivyo ukanushaji unaoneshwa kwa njia mbili katika matini: Kwanza kwa mpumuo na pili kwa tangamano irabu.
Katika vitenzi kiambishi awali kiima yu- badala ya Kiunguja a- kinachoashiria nafsi ya tatu umoja hutokea katika matini zote. Aidha kiwakilishi nafsi cha nafsi ya kwanza uwingi ni siswi badala ya sisi. Whitely (1956) na Nurse na
Hinnebusch (1993) hawakutaja maumbo hayo kuwa sehemu ya sarufi ya Kimtang’ata. Inawezekana kwamba yaliingia kutoka lahaja za kaskazini, hasa Kivumba. Zaidi ya hayo Meinhof (1905: 54) alieleza siswi kuwa kiwakilishi nafsi katika lugha ya Kidigo inayozungumzwa katika eneo la Tanga.
Kuhusu mofimu ya wakati, hali na namna (TAM) matini zilionesha sifa ya kilahaja moja tu, maana yake matumizi ya –na badala ya Kiunguja –me- kutaja hali timilifu. Nurse (1982: 176) na Nurse na Hinnebusch (1993: 420) wakieleza kipengele hicho kwa lahaja za jirani Kivumba, Kipemba na Chichifundi pia.
Matini simulizi zinataja vitenzi zenye kisaidizi –(e)vu na kitenzi chenye mofimu –ki- zinazolingana na Kiunguja –likuwa na –ki­-. Kazi ya mifumo hiyo ni kuonesha sharti au tendo lifululizalo. Nurse (1982: 178) alitaja tungo hizo kuhusiana na Kivumba na Kitumbatu.
(6) Na baba kevu akanga
 (Na baba alikuwa akianga)
Upanuaji wa kitenzi unaonekana katika kitenzi –chukua kitungwapo katika kauli ya kutendewa tu, maana yake –chukulibwa badala ya –chukuliwa. Kitenzi hicho ni dalili ya pekee ya uviringishaji katika tungo ya kauli ya kutendewa. Kihusishi kinachounganisha kitenzi na mtendaji ni kitenzi shirikishi ni badala ya kihusishi na.
Kuhusu kirai nomino matini zinaonesha tofauti mbili zikilinganishwa na Kiunguja. Kwanza,wahojiwa walitumia kimilikishi –akwe (taz. Mfano (7)) sawasawa na –ake. Sacleux (1909: 116) na Burt (1910) walikuwa wameshataja –akwe kuwa kimilikishi kwa lahaja za kaskazini. Whitely (1956: 18) hakueleza unasibu katika matumizi ya tungo hizo mbili. Alitaja –akwe tu. Kama isemavyo mwanzoni mwa makala haya Kiunguja kimeathiri haswa lahaja jirani.
                        (7) Huyo ng’ombe aliyekuwa na nafsi yakwe khanashiba.
                             (Huyo ng’ombe aliyekuwa na nafsi yake hakushiba)
Sawa na lahaja nyingine pamoja na Kiunguja majina ya wajamaa  huunganishwa na vimilikishi kimsinyao. Sifa maalumu katika matini za Kimtang’ata ni usilimisho mbele ya irabu ya mwisho /a/ hugeuza /i/ mbele ya nusu-irabu /y/. Mifano kama (8) na (9) ilikuwa imeshaelezwa na Sacleux (1909: 118) kwa jumla lakini hakutaja matumizi ya usilimicho mbele kwa Kimtang’ata.
                        (8) Babiye ana mazizi ya ng’ombe mengi
                             (Baba yake ana mazizi ya ngombe mengi)

                        (9) Sasa amwuliza mamiye.
                            (Sasa anamwuliza mama yake)
Sifa ya pili katika kirai nomino ni mifano ya viwakilishi oneshi mbali vyenye mfumo h+upatanivu+le. Mieche (1979: 145) anaelez kazi ya mfumo huo kuwa ni kutilia mkazo. Mfano (10) unasaidia ufafanuzi huo.
            (10) Baada ya kumwoa mkewe, siku hiile yule bwana asomesha somesha moja kwa moja mpaka usiku wa saa nne, saa tano.
(Baada ya kumwoa mkewe, siku ile yule bwana asomesha somesha moja kwa moja mpaka usiku wa saa nne, saa tano.) kazi ya kutilia mkazo itakuwa wazi katika hadithi yenyewe. Mke wa mwalimu huyo alikasirishwa na bidii ya mume wake kadiri alimtamkia kuishi na jamii.
         5. Msamiati
Kwa ujumla msamiati wa matini zinazozungumziwa katika makala haya unafanana na ule wa Kiunguja. Sifa mbili zilizotokea ni vitenzi –ola na –uya. Nurse na Hinnebusch (1993) walifahamisha –ola (Kiunguja –ona) kuwa neno la Kimtang’ata na Kivumba. Whitely hakulitaja kabisa. Kitenzi -uya kinachofanana kikazi na -rudi liliingizwa na Whiteley katika orodha ya maneno ya Kimtang’ata (1956: 63). Sacleux (1939: 988) alieleza -uya kuwa linatokana na lugha ya kizamani iliyoacha maneno machache katika lahaja za kaskazini. Ili kusaidia maelezo yake alitoa ubeti mmoja wa Fumo Liyongo.

           6. Hitimisho
Lengo la makala haya lilikuwa kutafiti sifa za lahaja ya Kimtang’ata katika matini simulizi na matini za mazungumzo. Matini hizo ni mifano ya lugha ya wanawake wanaotoka vijijini ambapo, kufuatana na Whiteley, Nurse na Hinnebusch, Kimtang’ata kilitumiwa. Lugha ya wahojiwa ilichambuliwa katika viwango vya fonetiki, mofolojia na msamiati. Msingi wa ulinganisho ulikuwa Kiunguja, maana yake Kiswahili Sanifu.
Uchunguzi umebainisha kwamba sifa za kilahaja zilitokea nadra tu na matini zinaeleweka kwa watu wanaojua Kiunguja. Tofauti zilitokea haswa katika kiwango cha mofolojia. Hivyo matokeo ya utafiti huo yanahitilafiana na maelezo ya Whiteley, Nurse na Hinnebusch ambao walisisitiza sifa za Kimtang’ata haswa katika kiwango
cha msamiati. Hitilafu hizo zinaweza kuelezwa na sababu kwamba msamiati ni sehemu ya lugha ambayo hubadilika upesi zaidi kuliko zote. Zaidi ya hayowanawake hao husafiri mara nyingi kati ya vijiji vyao na mji wa Tanga. Ongezeko la usafiri linaelekea hali ambapo sifa chache za mofolojia zitakuwa kumbukumbu za mwisho za Kimtang’ata.
Uchunguzi juu ya mahojiano ulionesha kwamba wahojiwa walisahihishana lugha zao. Hali hii ingedokeza kwamba hawana uhakika tena kuhusu lugha zao za vijijini. Zaidi ya hayo hawakujua kwamba lahaja yao huitwa Kimtang’ata. Hivyo ni lazima kuuliza kama lahaja hiyo ilikuwa hai kweli wakati uliopita au kama Kimtang’ata ni mfano mzuri wa kubuni kwa kitaaluma. Mtu lazima ajiulize kwa nini Charles Sacleux aliyeishi jirani na kuandika kitabu kizima juu ya lahaja za Kiswahili hakutaja Kimtang’ata hata mara moja? Mohling (1995: 44) alisawazisha Kimtang’ata na Kimrima. Lakini Kimrima ni Kiswahili kisemwacho kati ya ghuba ya Vanga na Rufiji, yaani Kimrima ni istilahi inayojumlisha matumizi ya Kiswahili katika eneo linalohitaji ufafanuzi wa kiisimu zaidi. Mradi wa pamoja wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam na Chuo Kikuu cha Helsinki wa kuchambua matumizi ya Kiswahili kusini mwa Dar es Salaam, Unguja, Pemba, Tumbatu na Mafia ni mwelekeo mzuri wa kudhihirisha hali ya Kiswahili katika eneo hilo (Hurskainen 1998).
Kwa kumaliza inapaswa kusisitiza tena kwamba matini zilizokuwa msingi wa utafiti huu ni mifano ya lugha ya mjini. Wahojiwa na jamaa zao walisema kwamba vijijini kusini mwa Tanga watu wanatumia lugha tofauti kabisa. Lakini hawakuwa na uhakika kama lugha hiyo ni Kiswahili au lugha nyingine ya Kibantu. Hivyo, uchambuzi katika eneo hilo ungeweza kutoa matokeo tofauti.

Marejeleo
Kioo cha Lugha 2, 1996/97:15-21
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)