MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SABABU ZA KUTOKEA KWA LAHAJA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SABABU ZA KUTOKEA KWA LAHAJA
#1
Sababu za kutokea kwa Lahaja:
Utengano Wa kijiografia: kuna mambo yanayosababisha watu wanaozungumza lugha moja kutengana kimahali na kimielekeo. Utengano huo husababisha mawasiliano yao kupungua. Kwa kuwa mawasiliano  ni haba, kuna uwezekano mpana wa watu walioachana  kukuza upekee wa namna fulani katika usemaji wao. Kwa hivyo, msingi wa upekee wa usemaji au kuzuka  kwa  lahaja.
Utengano  wa kitabaka: katika jamii moja kunaweza kuwa na tabaka mbalimbali za watu . Kila tabaka hujihisi na kujitambulisha kwa namna ya pekee japokuwa matabaka hayo huishi katika eneo moja.
Msingi wa mwachano wa kitabaka huweza kuwa uchumi, dini, elimu, au siasa. Kwa sababu ya mwachano wa kitabaka, mawasiliano ya mara kwa mara baina ya watu wa tabaka mbalimbali hupungua. Na mawasiliano ya mara kwa mara yakipungua nafasi ya kuchipuka upekee hata katika usemaji hupanuka. Hivi ndivyo vianzavyo vipengele vya usemaji vifungamanavyo na tabaka.
Utengano wa kiwakati: wakati ni kipengele muhimu katika kuzuka kwa lahaja. Umbali tu hautoshi, uwe wa kijiografia au kitabaka. Hata baada ya wasemaji wa lugha moja kutengana kwa sababu ya hiki au kile, upekee katika usemaji hauzuki mara moja. Hutokea taratibu kadiri wakati unavyopita. Kipengele cha wakati ni muhimu vilevile katika ukuzaji wa lahaja za kijamii au za kitabaka. Hivyo ni lazima watu waliotengana wasikaribiane kwa muda mrefu kiasi cha kutosha kumea kwa tofauti za usemaji.
Ubinafsi: Tabia ya kibinadamu ya kutaka kujitofautisha na wengine humfanya mtu atafute namna mbalimbali za kujitofautisha na akikosa hutumia lugha yake kujitofautisha kwa jinsi ya usemaji. Utofauti huo wa kiusemaji kwa kuwa hauleti athari katika mawasiliano basi huitwa lahaja.
Shughuli zilizopo: Katika eneo lolote lenye shughuli za kibinadamu mara nyingi huibuka tofauti za kiusemaji kutokana na mwingiliano wa watu wanaokutana kwa shughuli zao. Tofauti zinazoibuka katika mazingira hayo huwa lahaja tu za lugha husika.
MAMBO YANAYODHOHOFISHA LAHAJA
Maendeleo ya njia za usafiri: kama vile barabara, reli, mitumbwi, nk. Vyombo hivi huwakutanisha watu pamoja hasa waliotengana kijiografia na matokeo ya kukutana huko husababisha kusawazisha hata namna ya kusema, maana za maneno.n.k.
Maendeleo ya njia za upashanaji habari: kama vile redio, televisheni, magazeti, n.k. vyombo hivi vya upashanaji habari huunda umoja wa pekee miongoni mwa watumiaji kwa vile wote huathirika na mawazo na usemaji wa namna moja kwa wakati mmoja.
Kuwepo chini ya utawala au dini moja: dini na utawala ni vitu vyenye kukazia umoja miongoni mwa raia au wafuasi wake. Umoja wa aina yoyote ni kichocheo cha ukaribiano katika usemaji na matokeo yake ni kusawazisha tofauti za usemaji.
Usanifishaji: husababisha baadhi ya lahaja kudumaa kwa sababu usanifishaji husawazisha matamshi ya maneno.
Biashara na dini: hivi pia ni vitu ambavyo huwakutanisha watu pamoja mara nyingi na kwa muda mrefu.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 2 Guest(s)