MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

RIWAYA YA SHAMBA LA WANYAMA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
RIWAYA YA SHAMBA LA WANYAMA
#1
MWANDISHI: George Orwell’s
MWAKA : 1967
Baada ya mapinduzi na kupata uhuru, mataifa haya hupata viongozi wanaojijali wenyewe na kujitakia makuu. Hawa huwa wameona upenyu wa kujilimbikizia mali na kupata mamlaka juu ya wenzao.
Katika riwaya hii, nguruwe wawili wachanga, Mzushi na Mkimwa, walitwekwa jukumu la kuwaongoza wanyama wengine katika kupigania uhuru
Baada ya kuupata wanaanza kubadilisha mustakabali wa awali.
Wanakuwa na ubinafsi na mapendeleo kwa nguruwe wenzao licha ya kuwa moja ya masharti yalikuwa uwepo wa usawa kwa wanyama wote.
Nguruwe walianza kujinufaisha peke yao kwa vyakula vya kipekee kama vile maziwa ya ng’ombe na tofaa.
Walifanya hivyo wakidai kuwa miili yao ni ya kipekee mno na kuwa wao walikuwa wakifanya kazi kubwa ya kufikiria sana kwa niaba ya wengine hivyo basi walihitaji chakula cha kipekee kama hicho!
Maajabu ni kuwa nguruwe wote walikubaliana kuhusu jambo hilo.
Matendo haya ya nguruwe yalikuwa na maana kuwa wao walijiona bora zaidi kuliko wanyama wengine wote.
Waliona kuwa wao walistahili kula vinono zaidi ya wenzao.
Mbali na nguruwe kujipendelea, wanatumia uongo ili kuwahadaa wenzao.
Waliwadanganya kuwa ili waweze kuwaongoza vyema, walilazimika kula vyakula vitamu na vya kipekee.
Waliwadanganya wenzao kuwa Mwenye shamba angerudi tena iwapo hawangeweza kupata chakula hicho cha kipekee. Vilevile, nguruwe walitumia propaganda ili kuwajaza kasumba wenzao.
Kuongoza
Kwa mfano, waliwafanya wenzao kujiona wajinga na kuwaona hao kuwa ndio tu wanaoweza kuongoza.
Wanyama wengine waliishia kuwa watumwa wao.
Walifanya kazi ngumu ilhali Nguruwe walikuwa wakiwahimiza tu.
Haya ndio maongozi yanayopatikana katika mataifa ya Afrika baada ya uhuru.
Viongozi wachache huona mbali na kuona jinsi ya ujinufaisha ilhali wananch wengune huwa kama watumwa wao, wakatumiwa kuwanufaisha wachache. Wananchi wawe macho dhidi ya mienendo kama hii ili isiruhusiwe kuendelea.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)