12-28-2021, 08:10 AM
TAMATHALI ZA USEMI
Tamathali za usemi ni aina ya matumizi ya lugha yanayohusishwa sana na ushairi hata wakati mwingine waandishi wa nathari.
Ni aina ya msemo fulani kwenye lugha unaojaribu kufupisha maelezo kwa kuchora picha ya aina Fulani wenye kujaribu kushawishi mawasijiano ya kisanaa kwa njia ya kufuma hisia kwa wasomaji au wasikilizaji.
1.Tashbihi.
Hii ni mbinu ya uhusisho baina ya vitu viwili.Pia ni mbinu inayotumia uhamisho wa kimaana;yaani sifa, tabia, umbo, sura, muundo au umbo kutoka kitu kimoja huhamishwa kwenye kitu kingine, lakini hapa uhamisho au uhusisho si wa moja kwa moja, bali hupitia katika maneno kama : mithili, kama, mfano wa, vile, sawa, useme, na maneno mengine ya kuonyesha mlinganisho kati ya vitu mbali mbali. Mifano :
- Afya mwilini ni kama mafuta katika utambi wa taa
- Ana upara kama jagwa la Sahara
- Ali alinguluma useme simba mkali
- Alikuwa na midomo mikubwa yenye nyama iliyojikunja kama pua ya nguruwe
- Dunia ni kama uwanja wa mpira, kila mmoja anapasua kujua sehemu gani atapigania ushindi maishani mwake
- Alikuwa na nyusi mfano wa mwezi mwandamano.
Katika sentensi ya, afya inalinganishwa na utambi wa taa.upara wa mtu fulani unalinganishwa na jangwa la sahara katika sentensi ya
2, katika sentensi ya tatu tunaona mgurumo wa Ali ulilinganishwa na ule wa simba n.k uhusisho huo ambao si wa moja kwa moja unjaotumia maneno kama : kama, mfano wa, useme….kuonyesha mlinganisho kwa vitu mbali mbali ni Tashbihi.
2.Sitiari :
Ni tamathali ya usemi ambayo kwayo kitu matendo ya kitu au vitu kvyenye hulka mbali mbali, hulinganishwa na hali sawasawa ya maumkbile au jinsi ya utendaji.
Katika sitiari, maneno ya mlinganisho hayatumiki.Mlinganisho wa sitiari hufichwa ndani kwa ndani na hufichuliwa kwa hisi tu.
Mifano :
- Kamau alikua simba
- Mapenzi ni majani huota popote
- Kukopa harusi, kulipa matanga
- Tabia njema ni mzizi mkuu wa fadhila
- Ujana ni moshi, ukenda haurudi tena
- Maisha ya duniza ni bahari
3.Tashihisi
Ni thamathali ya usemi ambamo kuna hali ya mlinganisho baina ya vitu viwili lakini sasa kimoja cha vitu hivyo ni chenye uhai na cha pili si kitu chenye uhai. Hiki kitu kisicho na uhai au kisicho na tabia za kibinadamu hupewa sifa, tabia, sura au matendo ya kiuhai, au kiutu na kibinadamu.
Mifano :
- Ubaya hatimaye utamezwa na wema na sisi sote tushuhudie.
- Wakati ulikua ukipiga mbio huwahi mwisho wa mtu yule.
Katika mfano wa 1, tumeona kwambaq wema unapewa uwezo wa kumeza kama vile mwanadammu anavyomeza kitu.Na katika mfano wa 2 tunaona wakati unapoewa uwezo wa kwenda mbio kama kitu chenye uhai.
3.uhaba una ndwele mbi, una ndele mbi
uhaba Uhaba huleta dhambi, mtu hutamani kuiba
Uhaba hupiga kambi, lango hutia bawaba
Katika ubeti huu kutoka shairi la Mathas E.Mnyampala tunaona kwamba uhaba unapewa uwezo wa kukumbwa na maradhi(ndwele), uwezo wa kumletea dhambi na uwezo wa kupiga kambi.
3.TAASHIRA :
Ni namna ya fani ya usemi, ambao kwao, kwa sababu ya mwambatano wa ujamii au uhusiano mkubwa uliopo kati ya vitu fulani, ishara, alama, dalili, au neno Fulani, hutumika kuwakilisha tendo au kitu tupendacho kutaja, badala ya kueleza wazi wazi .
Mifano :
- Shoka la kata miti msituni
- Anavaa kanzu za china
- kila nyumba ina furaha kubwa ya mazao
- Fadhila nyingi na shangwe zilifika siteshoni ya treni mjini Dar es
Salamu
Shoka lakata miti yametumika kawakilisha watu wenye kukata miti Kanzu za china huwakilisha ka knzu zilizotengenjezwa uchina furaha majumbani huwakilisha watu wenye furaha nyumani, n.k
(i) Alama au ishara hutumika kufidisha hali fulani ya utendaji.
(ii)kitu au chombo cha utendaji huwakilisha mtendaji au watendaji (iii) Tendo huakilisha mtendaji.
(iv)mahali kitu kilipotengenezwa huakilisuha kitu kitengenezwacho.
(v)mtendaji huakilisha tendo.
4.Takriri :
Ni kmtindo wa uneni wa fasaha, ambao msemaji kwa makusudi au nia mahsusi, hurudia neno au maneno yale yale ili kutia mkazo au msisitizo zaidi, juu ya jambo asemalo .Mtindo huu wa msemo wa msistitizo, huwa na nia ya kutia nanga jambo Fulani ili liweze kumwingia msikilizaji moyoni apate kulidhibiti vizuri.
Mifano:
1. Kifo hakiogopi kiumbe chochote duniani.Kifo hakimuopi mtawala au raia, Kifo hakina tajiri au maskini, kifo hakichagui mzee au chipukizi .Kifo hakina mkubwa au mdogo. Kila kitu chini ya mazingira kiomesha pigwa muhuri na kifo.
1. Kifo hakiogopi kiumbe chochote duniani.Kifo hakimuopi mtawala au raia, Kifo hakina tajiri au maskini, kifo hakichagui mzee au chipukizi .Kifo hakina mkubwa au mdogo. Kila kitu chini ya mazingira kiomesha pigwa muhuri na kifo.
2.Tulipo karibia kupambazuka, tuliusikia vurumai kubwa, ’’ Mwizi.mwizi, mwizi huyo .Mkamateni mkamateni, mkamateni. Mwizi huyo mkamateni.’’
5.Tanakuzi :
Ni mtindo wa uneni wa fasaha ambao kwao maono au mawazo mbali mbali yenye mgongano na uhitilafiano, huunganishwa pamoja kakika sentensi au kifungu cha maneno ili kufanya mvutano mkubwa zaidi wa mawazo.
Mifano:
- Kukonda rahisi kunenepa kugumu
- Matengano ni huzuni makumbano ni lfuraha.
- Baada ya dhiki, faraja
- Hawa wanaingia hawa wanatoka
6.Tabaini:
Ni mmtindo wa uneni wa fasaha, ambao kwao msemaji husisitiza kauli au ukweli na jambo Fulani kwa kutumia maneno yenye ukinzani, aghalabu neno “si”.
Mifano:
- Lo, ama kweli Juma anafanana sana na babake, si kuwa, si nywele, si mdomo, si macho, si kichwa, si sauti !Ama baba na mwanawe wako kama pande mbili za sarafu.
- Kwake watu wote walikuwa sawa, si mdogo, si mkubwa, si masikini, si tajiri. Kwa kutumia neno “si”siyo kwamba twakanusha au kubomoa kauli tusemayo.
7.Kinaya:
Tamathali hii hutumika kwa kusemea kitu kimoja kwa kumaanisha kingine.Tamathali hii huweza kuonekana katika neno au kauli Fulani katika muktadha Fulani ilimojitokeza, au katika shairi zima.Kwa mmfano, shairi “Bustani”ya S.A.Muhammad, katika mojawapo wa beti zake, latongoa hivi : Yamerudikwa machicha, na maganda ya matunda. Na mwiku uliochacha, na mbali uliovunda. Harufu inopekecha, yanukia naipenda Hakuna inomchusha, bustani ya maua. Kinaya hapa inajengwa kuanzia mustari wa tatu pale ambapo harufu inayopekecha kuwa inasemwa inanukia na kupendwa na hatimaye bustani na taka, machicha, maganda ya matunda ambayo unaambiwa hapana inomchusha.Kinyume kipo pia pale ambapo uchafu wa kupindukia huitwa bustani.
- Kejeli:
Hii ni tamathali inayofanyia stihizai, kebehi au dharau.Anayefanyiwa kejeli huwa anasutwa kwa kutupiwa maneno ya kero. Kwa mfano : Wanyakyusa wanaoishi Tanzania Kusini wanawakejeli Wazungu jinsi wapendavyo pesa kwa kutumia dini:
Basikalija anasali wapi?
Kwenye mawe kwenye mawe
Watemi wanasali wapi?
Kwenye mizimu kwenye mizimu
Wazungu jee wanasali wapi?
Kwenye pesa kwenye pesa.
9.Tafsida:
Msemo wa adabu, ambao kwao mambo yasiyopendeza hatamkwi waziwazi, hasa hadharani, hutajwa kwa lugha ya siri bila kuchukiza au kuchafua moyo ili kinyaa au hali m, baya waonayo watu moyoni. Mifano :
- Acha naye aone cha mtemakuni, Mungu amemnyoshea kidole.
- Mbona mtoto yule ana mkono mrefu vile!
- Tafadhali nikumbushe, umenitoka machoni kidogo.
10.Dhihaka:
Ni tamathali ya usemi ambayo inatumiwa kwa kusema maneno ya kumjukumu na kumdhihaki mwingine kisirisiri.
Mfano :
Bwana Bwanyenye wewe ni miongoni mwa matajiri nchini Tanzania, ama labda nikuite kabaila, nanyi makabaila wa siku hizi mu wakarimu sana.Juzi umetoa shilingi mooja kama ya dawa ikiwa ni mchango wako kusaidia ujenzi wa makao makuu ya TANU. Ingawa maneno yaliyoambiwa bwana Bwanyenye juu ya kutoa shilingi ikiwa ni mchango wa kusaidia ujenzi wa makao makuu ya TANU ni ya sukari, lakini yalikuwa machungu moyoni.Msemaji hakuwa na nia ya kumsifu bwana Bwanyenye kama mtu mkarimu, bali nia yake ilikuwa kumdhihaki bwana Bwanyenye kama mtu bahili asiye na moyo wa uzalendo bora.
11.Chuku:
Hii ina maana ya kutia chumvi jambo fulani linapojadiliwa.Kwa mfano, mwimbaji wa taarabu anapomwimbia mpenzi wake kuwa pendo lake lina thamani ya kuti ambayo usiku na mchana linang’aa na kuenea chumba kizima-hii ni chumvi tosha. Pendo nlako nil la kutii moyoni limeshakaa Mchana na lailati, nuru yake huzagaa Ah! Mpenzi nimo peponi.
12.Tanakali sauti :
Huu ni usemi unaoonesha jinsi maneno ya lugha yanavyoweza kuiga sauti halisi. Kwa mfano, fisi anapotandikwa mwangwi wa mjeledi anasikika “chwaaa!” Rangi yake ni nyeupe, ila si nyeupe peee. Alikuwa na weupe, wenye wekundu haba
Njiwa huyu hulia kooo!!
Mazoezi:
Katika maandishi haya onesha tamatali za usemi zilizotumiwa?
- Pendo
Pendo, pendo wee!
Mbona huchoki kunisumbua?
Daima waninyanyasa,
Pendo adui ya wanadamu.
2.Mpenzi
Tanzania Tanzania, Tanzania!
Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania,
Jina lako ni tamu sana!
Nilalapo nakuota wewe,
Niamkapo ni heri mama we!
Tanzania, Tanzania!
Nakupenda, kwa moyo wote!
- suu ulimwengu bahali tesi
- Kamau alikua simba mkali
- mtoto huyo ana macho kama ya kobe
- Nakwenda kwa haja kubwa
- Ndege walijaa uwanja wote hata sindano haionekani.
Mwl Maeda