09-04-2021, 07:40 AM
MAKALA YA ARUDHI YA USHAIRI
MIZANI
Jambo linalonifanya nishikekalamu leo ni mijadala kuhusu mizani katika ushairi.
Mijadala kuhusu mizani hukosa mwelekeo, mantiki na huishia ubishi usio na joja zenye upembuzi yakinifu hivyo huishia hewani bila suluhu.
Watu wengi kwa utafiti wangu huingia katika mijadala ya kishairi wakijua wazi wakijua ,
1.Mizani ni idadi ya silabi katika mishororo ya shairi au utenzi.
2.Huingia na dhana ya kuhesabu silabi katika maneno yanayounda mishororo ya shairi.
Hupungukiwa mambo ya fuatayo.
1.Wanashughulikia kanuni za kishairi na si maneno katika sentensi.
2.Wanashughulikia muundo wa sauti katika mishororo ya shairi na si muundo wa silabi katika maneno ya senrltensi.
3.Hushindwa kujibaini kuwa arudhi katika ushairi inajihusisha na urari/usawa wa vina, mizani, maneno, vipande, mishororo na beti.
4.Hushindwa kujibaini sababu za kuwekwa mizani katika shairi.
5.Hushindwa kubaini kuwa kuna muundo na aina za mashairi ya kimapokeo na Masivina.
Hivyo huishia kwenye mtazamo binafsi bila kuzingatia arudhi.
Hivyo baada ya utafiti na upembuzi yaninifu na wa kina nimebaini mambo hayo juu hivyo kuamu kumwaga wino.
Mosi, Katika arudhi za kishairi urari ni kipaumbele ili kuleta _Utelezi wa lugha, Toni na Kiimbo katika kipimo cha kuamsha hisi chanya na mvuto na si uchovu wa hisia_ .
Hivyobkupanga ama kuhesabu mizani katika ushairi kipaumbele ni kuangalia arudhi katika urari wa mishororo na si silabi katika maneno ya kawaida au sentensi.
_Sababu_.Shairi lolote au aina ya wimbo huimbika kwa mlalo na si wima.
Kwa mantiki hiyo kuhesabu mizani kwa idadi ya usawa wa mlalo katika mishororo ni sahihi na si kuhesabu mizani kwa maana ya jumla ya silabi za kawaida katika muundo wa maneno au kanuni za sentesi za kawaida ambao hauna sababu yoyote arudhi za kishairi.
Mfano.Kama swali ni " Vipande katika shairi hili vina mizani ngapi? Ama, Shairi hili lina mizani mgapi? Ama, Jumla ya mizani katika beti za shairi ni mizani ngapi?
Kipaumbele kitakuwa katika kuzingatia urari wa mlalo ili kuwezesha shairi, utendi au wimbo kuimbika au kughani kiurahisi kwa mapigo ya mlalo ya kupanda na kushuka ya mshairi, mutribu au mwimbaji ili kuleta mvuto wa kishairi au mapigo ya kimuziki.
Mfano. Do, re, mi, fa soooooo!
Re, to, do, mi...........!
Kwa mantiki hiyo jumla ya mizani katika nusu mishororo au mishororo inaweza kuwa 6, 8, 9, 10, 12, 14, 15, 16, 18.
Na si jumla ya wima kama 32, 48, 64, 128 nk ambayo haina mantiki yoyote kwa mghani, mutribu au mwimbaji.
Atawianisha vipi kwa mfano katika pumzi ya 32, 48, 64, 128, nk inabidi awe na mapafu zaidi ya mapafu mia ya mbwa.
Rejea.Maswali ya ushairi PSLE uchambuzi wa NECTA 2020.
Rejea kamusi, na waandishi nguli wa medani ya ushairi hueleza dhana ya mizani katika ngazi ya idadi ya jumla ya usawa katika mlalo wa mshororo na si jumla kuu ya wima.
Karibu kwa hoja kuntu zenye mantiki.
_Mwandishi_ Mwl. Kizinga.
0718 932 888.
kizinga05@gmail.com

Mwl Maeda