08-01-2021, 02:56 PM
SWALI: Nini maana ya stadi ya kusikiliza? Eleza vipengele vyake
JIBU
Kusikiliza ni stadi inayomuwezesha mtu kupokea maarifa kwa kusikiliza toka kwa mtu mwingine, au kutoka kwenye media zilimorekodiwa masuala mbalimbali kama vile santuri,vinasa sauti,tepu rekoda au hata kwenye redio.
Stadi ya kusikiliza kama zilivyo stadi nyingine hutawaliwa na vipengele mbalimbali ambavyo husimamia usikilizaji wa mtu. Vipengele hivyo ni:

- Viungo timamu vya mwili vinavyohusiana na usikiaji
- Utayari wa kusikiliza kinachosemwa na mzungumzaji
- Hamu ya kusikiliza kinachosemwa
- Utulimu na umakini wakati wa kusikiliza
- Uwezo wa kutafsiri na kuhusianisha yanayosemwa na mazingira yake ya kila siku
- Uchaguzi mzuri wa mawazo makuu katika kile anachosikiliza
- Uzingatiaji wa mambo yanayozungumzwa na kutathimini umuhimu wake
Mwl Maeda