07-27-2021, 08:04 AM
SWALI: “Watumiaji wa lugha ya Kiswahili ni watu wa makundi manne (4) ” Thibitisha ukweli wa kauli hii.
Lugha ya Kiswahili inazungumzwa na watu wa makundi makubwa manne katika jamii. Makundi hayo ni:
- Wasemaji wa Kiswahili ambao ni lugha yao ya kwanza
- Wasemaji ambao Kiswahili ni lugha yao ya pili kwa mfano mtu anayefahamu lugha yake ya asili kama lugha ya kwanza
- Wasemaji wa Kiswahili wageni ambao wanakifahamu Kiswahili vizuri na kumudu kaida zake
- Wasemaji wa Kiswahili ambao hukifahamu kwa kiasi kidogo mno hasa wageni ambao huja kujifunza mila na desturi za waswali na kukaa nao kwa muda mfupi.
Mwl Maeda