MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

KUHUSU KUONA/KUONYA na KUONESHA/KUONYESHA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
KUHUSU KUONA/KUONYA na KUONESHA/KUONYESHA
#1
KUHUSU KUONA/KUONYA na KUONESHA/KUONYESHA

Nawaomba radhi wanaukumbi kwa kuwarudisha nyuma kwenye mazungumzo ya juzi, kuhusu haya maneno yaliyoko hapa juu.

Nianze kwa kuungama. Katika baadhi ya nyakati hutolewa maoni hapa, ambayo nami hutamani niongeze yangu, lakini hujizuia na kujiambia niyapishe yapite. Wakati mwingine huyapisha kwa kuogopea nisije nikaonekana najifanya kuwa ni mjuvi (mjuaji) mno! Lakini mara nyingine hushindwa kujizuia.

Mwenzetu, Bwana (au ni Bibi?) Nii Adjetey, aliomba aelezwe tafauti kati ya "kuonesha" na "kuonyesha." Wa kwanza aliyemjibu akaashiria kwa ufupi tu kwamba "kuonesha" latokana na "ona"; na "kuonyesha" latokana na "onya." Na wenzetu wengine wawili wakafuatia kwa kutoa mifano ya matumizi ya maneno hayo, na kuelezea kwamba "ona" lina maana sawa na "tizama" (tazama); na kwamba "onya" lina maana ya kukanya/kuadibu/kukataza. Nakubaliana na hayo.

Nitakalo kuongeza ni kwamba mbali na kuwa "onya" lina maana hiyo iliyoelezwa, pia lina maana ya "onesha" - ambayo naamini ndiyo maana yake ya asili. Katika lugha ya Kiswahili kuna maneno machache ya vitenzi vilivyomalizika kwa silabi -na, ambavyo vikibadilishwa katika hali ya kusababisha, silabi hiyo ya mwisho hugeuka na kuwa -nya.

Kwa hivyo, basi, ukinionya kitu huwa unanionesha kitu hicho. Waweza pia kumsikia mtu akisema kwamba Fulani alikuja hapa akaruonya vituko!

Na ukiwa mgonjwa, halafu ukala dawa ikakuponya, dawa hiyo huwa imekusababisha wewe kupona.

Tukija katika mambo ya uganga, waganga wanapofanya ya kufanya ili kugonya k'oma, huwa wanaisababisha mizimu kugona, yaani kuilaza au kuituliza. Katika Kiswahili cha kale - na hadi leo katika lugha za Mijikenda - neno "kugona" lina maana ya "kulala." Ndipo kwa wale walio na mke zaidi ya mmoja hutakiwa wagawanye ugoni kwa siku sawa sawa - ukilala siku mbili kwa mke wa kwanza, basi na kwa mke wa pili iwe ni siku mbili pia. Na kutokana na neno "kugona" ndipo tukapata neno "ngono", ambalo twalijua maana yake.

Miongoni mwa maneno yanayofuata kanuni hiyo ni "kana" (=kataa; kutokubali). Kwa hivyo, unapomkanya mtoto huwa unamkataza asifanye jambo fulani, aghlabu jambo ovu au la hatari. Pia neno "dangana" ((= kutokuwa na hakika ya jambo, au kutoujua ukweli wa jambo, au kutatizika na jambo). Kwa hivyo, unapomdanganya mtu huwa unamsababisha asiujue ukweli wa jambo fulani.

Basi, kwa ufupi, neno "onya" lina maana ya kusababisha mtu kuona, kutahadharisha, kukataza, kuadibu. Na "kuonesha" na "kuonyesha", au "maonesho" na "maonyesho", hiyo ni mibadala; hakuna tafauti ya maana.

Baadaye leo, inshaAllah, nitajaribu kutoa maoni yangu kuhusu neno "tasiliti", lililoulizwa maana yake.

- Abdilatif Abdalla
Mwl Maeda
Reply

Messages In This Thread
KUHUSU KUONA/KUONYA na KUONESHA/KUONYESHA - by MwlMaeda - 07-21-2021, 07:22 PM

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)