12-22-2021, 07:35 PM
SINA HARAKA
simiĀ mwenye mamlaka, inipasapo kungoja,
Maana sina haraka, najua yajayo yaja,
wala sina mashitaka, nikadai jambo moja,
Anayejua Rabuka, lipi hasa lenye haja,
Na ikiwa hakutaka, aone halina hoja,
Simwangushii mashaka, kwa ubaya kumtaja,
akisema hili shika, akanipa wake mja,
sinipe ninayotaka, kishingo ama kipaja,
mie sitalalamika, kishingo sio kipaja!
Lolote likinifika, Mola nampa pambaja.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
simiĀ mwenye mamlaka, inipasapo kungoja,
Maana sina haraka, najua yajayo yaja,
wala sina mashitaka, nikadai jambo moja,
Anayejua Rabuka, lipi hasa lenye haja,
Na ikiwa hakutaka, aone halina hoja,
Simwangushii mashaka, kwa ubaya kumtaja,
akisema hili shika, akanipa wake mja,
sinipe ninayotaka, kishingo ama kipaja,
mie sitalalamika, kishingo sio kipaja!
Lolote likinifika, Mola nampa pambaja.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
Mwl Maeda