Hatuna budi kuwapongeza vijana wanajiotokeza kutafuta fursa za ajira kwa kufundisha Kiswahili katika asasi na taasisi ambako wapo wageni wanaotaka kujifunza Kiswahili.
Ijapokuwa baadhi ya walimu hawa hawana kiwango cha kuridhisha cha kufundisha na wala hawapati usaidizi wa kutosha kutoka katika Serikali zetu, ni dhahiri kuwa wanajitahidi.
Juhudi zinafanywa na watu binafsi katika kufundisha na kutangaza lugha ya Kiswahili katika ngazi mbalimbali za kimataifa.
Hatuna budi kuwapongeza vijana wanajiotokeza kutafuta fursa za ajira kwa kufundisha Kiswahili katika asasi na taasisi ambako wapo wageni wanaotaka kujifunza Kiswahili.
Ijapokuwa baadhi ya walimu hawa hawana kiwango cha kuridhisha cha kufundisha na wala hawapati usaidizi wa kutosha kutoka katika Serikali zetu, ni dhahiri kuwa wanajitahidi.
Hizi ni juhudi binafsi za vijana wetu za kujipatia ajira. Inafaa asasi na taasisi zenye jukumu la ukuzaji lugha ziongeze juhudi za kusaidia wimbi kubwa la vijana wenye elimu ya kutosha ya lugha ya Kiswahili kwa kujipatia ajira. Mfano mzuri ni viongozi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (Tataki), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) za kuanzisha mawasiliano na Chuo Kikuu cha Harare nchini Zimbabwe.
Taasisi hii ilifanya na mawasiliano na Chuo Kikuu cha Harare na hatimaye kufanikiwa kuwapeleka wahadhiri weledi wa Kiswahili waliokuwa tayari kwenda kufundisha Kiswahili.
Hatuna budi kuwapongeza wote walioanzisha mpango huu kwani ni sifa kwa taifa letu na faida kwa wahadhiri hawa ambao watakuwa ni mabalozi wetu katika nchi za nje kutokana na uzoefu wao.
Mpango huu wa kuwapeleka walimu huko Zimbabwe ulihitaji maandalizi ya kutosha ambapo hapo awali walianza kutayarisha mtalaa wa somo la Kiswahili nchini humo kwa kuzingatia stadi nilizotaja hapo juu na baadaye kuandaa vitabu, vielelezo na matini kwa ajili ya ufundishaji.
Walimu wanatakiwa kuwa wavumilivu kwani hii ni misingi waliyotakiwa kuandaa kwa wengine watakaokuja siku za baadaye.
Kwa kuanzia, somo lilianza kufundishwa katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe kwa lengo la kupata walimu ambao watasaidia kufundisha Kiswahili nchini humo kuanzia shule za msingi na sekondari.
Hivyo, darasa la wanafunzi 80 lilianzishwa mwaka 2012 likisimamiwa na walimu wenye uzoefu kwenye taaluma ya Kiswahili. Miongoni mwa walimu hao ni Titus Mpemba ambaye amewahi kufundisha darasa maalumu kwa wahariri, wahakiki na waandishi wa Kiswahili wa gazeti la Mwananchi na Mwanaspoti katika Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).
Hata hivyo, licha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kufundishia kwenye ngazi ya shule za msingi, bado wanafunzi na wananchi wa kawaida wanapenda kujifunza lugha hiyo kutoka kwa wenyeji wa Kitanzania.
Kutokana na mahitaji haya, gazeti la Mwananchi lina nafasi ya kuwa mojawapo ya marejeo wakati wa kujifunza, huku wakipata habari mbalimbali za kimataifa ikiwamo za Zimbabwe.
Njia mojawapo ya kuwaunganisha wanafunzi wa Zimbabwe na wenzao wanaojifunza Kiswahili ni kwa kutumia mtandao wa mawasiliano unaomilikiwa na Kampuni ya Nation Media Group ambayo ni kampuni mama ya MCL. Mtandao huu unajulikaka kama Swahili Hub na tovuti inafahamika kama www.swahilihub.com. Huu ni mtandao ambao umelenga kuwaunganisha watumiaji wa Kiswahili ulimwenguni kote.
Zaidi ya hayo, mtandao huu unatayarisha benki ya kuhifadhia majina ya vituo, vyuo shule na pia watafiti na wahadhiri wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kukusanya kazi zao za uhariri na uchapishaji wa makala, vitini na vitabu vya Kiswahili.
Wazungumzaji wa Kiswahili nchini Zimbabwe wanaweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwamo kukuza uelewa wa matumizi sanifu ya lugha ya Kiswahili kupitia makala za kitaaluma zinazopatikana katika mtandao wa Swahili Hub.
Stephen Maina anapatikana kwa baruapepemaina@mwananchi.co.tz