09-06-2021, 02:31 PM
Kukua na Kuenea Kwa Kiswahili nchini Tanzania
Wageni walipofika pwani ya Afrika Mashariki waliwakuta wenyeji tayari wana lugha yao yamawasiliano, ambayo ni Kiswahili. Kiswahili pia kilitumika kama lugha ya kibiashara miongonimwa wabantu. Hivyo wageni wa kwanza hawakuwa na sababu ya kutumia lugha nyengine zaidiyaKiswahili.Walilazimika kujifunza Kiswahili ili wakitumie katika shughuli zao mbalimbali zakibiashara zikiwemo shughuli za kibiashara, kidini na kiutawala.Wageni waliofika kwa nyakati tofauti katika pwani ya Afrika Mashariki ni waarabu, Wareno,Wajerumani na Waingereza. Kila kundi lililofika hapa likuwa na mchango wake katika kukuza nakueneza Kiswahili, pia wapo waodidimiza ustawi wa lugha hiyo.
UKUAJI WA KISWAHILI NCHINI TANZANIA WAKATI WA WAARABU
Kukua kwa lugha ni hali ya kuongezeka kwa msamiati wa lugha hiyo. Msamiati ni jumla yamaneno yanayotumiwa katika lugha fulani, ili lugha yoyote ikuwe lazima msamiati wake ukuwe.Wageni wa kwanza kuja Tanzania ni waarabu, kutokana na kuhusiana na Waarabu katikaNyanja mbalimbali. Ksiwahili kimechukua msamiati wa kiarabu ili kukuza msamiati wake, nitabia ya lugha zinapotumika pamoja huathiriana na kuchukuliana maneno. Yasemakanakiingereza kimeathiriwa na kilatini kwa kiasi cha theluthi mbili. Kiswahili kimeathiriwa na lughanyengine kama vile kihindi, kiajemi,kireno, Kijerumani, Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu n.k.Kiarabu ndicho chenye maneno mengi sana katika Kiswahili kuliko lugha ya taifa lolote jenginela kigeni, hii ni kwa sababu zifuatazo;(a) Bara Arabu ndiyo nchi ya kigeni iliyokuwa jirani zaidi na upwa wa Afrika Mashariki, hivyowatu wake waliingiliana zaidi na watu wa huku kuliko watu wengine wowote, maingiliano hayohayakuwa ya kibiashara tu bali hata ya kindoa.(b) Lugha ya kiarabu ndiyo lugha iliyotumika kufundishia dini ya kiislamu, hivyo waswahiliwalijikuta wanaingiza maneno ya kiarabu katika Kiswahili.
Sababu zilizochangia kukua kwa Kiswahili wakati wa utawala wa Waarabu
- Dini.
Waarabu walipowasili walianza kueneza dini yao ya kiislam kwa wenyeji wa upwa wa Afrika.Waarabu walianzisha madarasa ambayo walitumia kufundishia waafrika dini ya kiislam, wafrikahao walifundishwa kusoma na kuandika kwa hati za kiarabu ili waweza kusoma na kuelewa Qur-an.Lugha ya kufundishia katika madarasa hayo ilikuwa Kiswahili, hivyo waswahili walijikutawanaingiza baadhi ya maneno katika Kiswahili. Kutokana na dini na elimu tumeweza kupatamaneno ambayo tunatumia katika Kiswahili, maneno hayo ni kama vile; alajiri, alasiri, kurani,elimu, ratibu, inshallah.k
- Utawala.
Kutokana na kutawaliwa na waarabu,tumepata msamiati mwingi wa Kiswahili. Waarabuwalitawala Pemba, Unguja na sehemu za pwani za bara. Kutokana na kutawaliwa kuna baadhiya maneno ambayo yamechukuliwa kutoka lugha ya kiarabu na kuwa katika Kiswahili, manenohayo ni kama vile sultani, mwinyi,utukufu, enzi n.k
- Biashara.
Waarabu walipowasili katika mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki, walianza kufanyabiashara na wenyeji,kutokana na maingiliano hayo ya kibiashara , waarabu walianza kuingizamaneno mengi ya kiarabu katika lugha ya Kiswahili. Kutokana na maingiliano hayo yakibiashara, Kiswahili kilianza Kukua na Kuenea Kiswahili nchini Tanzania.kupanuka kwa kuongeza msamiati, na bila shaka hali hii ilisababihsa kukuwa kwa Kiswahili,mfano wa msamiati uliochukuliwa kutoka kwa waarabu na kingizwa katika Kiswahili ni jahazi,kodi, adesi n.k.
- Waarabu na ndoa za wabantu.
Wageni hawa walikaa kwa miak
Waarabu walipowasili katika mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki, walianza kufanyabiashara na wenyeji,kutokana na maingiliano hayo ya kibiashara , waarabu walianza kuingizamaneno mengi ya kiarabu katika lugha ya Kiswahili. Kutokana na maingiliano hayo yakibiashara, Kiswahili kilianza Kukua na Kuenea Kiswahili nchini Tanzania.kupanuka kwa kuongeza msamiati, na bila shaka hali hii ilisababihsa kukuwa kwa Kiswahili,mfano wa msamiati uliochukuliwa kutoka kwa waarabu na kingizwa katika Kiswahili ni jahazi,kodi, adesi n.k.
- Waarabu na ndoa za wabantu.
Wageni hawa walikaa kwa miaka mingi sana katika pwani ya Afrika Mashariki, walijikutawalowezi ambao mila zao na Kiswahili zilianza kuchangamana kwa kiasi fulani. Hivyo, waarabuwalijikuta wanatwa wake wa kibantu ili waishi kama mume na mke, lugha ambayo ilitumika sanakatika maisha yao ya ndo ilikuwa ni Kiswahili.Vile vile watoto waliozaliwa na wazazi wa kiarabu na kibantu walijifunza Kiswahili na kukitumiakama lugha yao ya awali. Malezi ya watoto hawa yaliegemea kwenye utamaduni wa Kiswahili,watoto hawa walikuzwa kwa lugha ya Kiswahili. Hata jamii ya watu wa pwani na Tanzania kwaujumla waliwaita watoto hawa “Waswahili” baada ya maneno kama vile “Chotara”.
Kwa ujumla utaona ndoa za waarabu na wabantu zilichangia pia katika kueneza lugha ya Kiswahili hapanchini Tanzania.
KUENEA KWA KISWAHILI WAKATI WA UTAWALA WA WAJERUMANI
Wajerumani waliingia nchini Tanzania, baada ya ujio wa waarabu na wareno. Wajerumaniwalipoingia nchini Tanzania walikuta tayari Kiswahili kinatumika kwa kiasi fulani. Ujio wao kamawakoloni, ulichangia sana kuenea kwa lugha ya Kiswahili. Njia zizotumika kueneza Kiswahilinchini Tanzania wakati wa utawala wa Wajerumani zilikuwa kama ifuatavyo:
(a)Utawala.
Kutokana na ukweli kuwa lugha ya Kiswahili ilikuwa imekwisha kuenea, Wajerumani waliamuakutumialugha hiyo katika shughuli zao za ki-utawala.Wajerumani walilazimika kujifunza lugha yaKiswahili huko huko Berlin kabla ya kuja nchini, kujifunza huko kulisaidia kuenea kwa Kiswahili.Kwa shughuli za kiutawala hapa nchini, ukolni wa Kijerumani ulitoa mwongozo kwa viongozi wanchini kujifunza na kutumialugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano katika utawala. Hiiilimaanisha kwamba wajumbe na maakida wote iliwabidi wajifunze lugha ya Kiswahili ili waweviungo wazuri waserikali na wananchi.
(b) Elimu.
Utawala wa Wajerumani uliteua lugha ya Kiswahili itumike kama lugha ya kufundishia, na piakutumika kama somo la kawaida katika shule za msingi. Baadhi ya shule hizo ni kama vileTabora, Mpwapwa na Kilosa,kwa mtazamo huo, wanafunzi na walimu walijifunza Kiswahili iliwakitumia katika shughuli za elimu na hivyo kufanya lugha hiyo kuenea kwa urahisi.
© Shughuli za kilimo (Mashamba).
Moja ya shughuli walizofanya Wajerumani, ilikuwa kuanzisha mashamba makubwa ya mazaoya biashara kama vile katani huko Tanga na kahawa huku Kilimanjaro na Bukoba. Katikamashamba haya kulikuwa na idadi kubwa ya vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi,lughailiyotumika ni Kiswahili, ambacho kilitumiwa na vibarua hao. Hivyo Kiswahili kilikuwa naongezeko la watumiaji na kufanya lugha hiyo kuenea.
(d) Mahakama.
Utawala wa Kijerumani ulitumia pia lugha ya Kiswahili katika shughuli za kimahakama.Wafanyakzai na wazee wa mahakama waliwahoji na kutoa hukumu kwa watuhumiwa kwakutumialugha ya Kiswahili. Hivyo shughuli za kati ziliendeshwa kwa Kiswahili na kufanya kiswailikienee chini ya utawala huu.Kiswahili baada ya UhuruBaada ya uhuru kuna harakati mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania katikakukiendelezana kukikuza kiswahili. Harakati hizo ni pamoja na kupendekezwa kuwa lugha rasmi1962. Mnamomwaka 1964 kiswahili kilipendekezwa kuwa lugha ya taifa na kuwa kitatumikakatika shughuli zote za kiserikali na kitaifa mfano katika elimu hususani elimu ya msingi.Kundwa kwa Chombo cha usanifishaji ambacho kilikuwa na kazi ya kuhimiza maendeleo yakiswahili,kutayaricha kamusi na vitabu mbalimbali vya sarufi na fasihi ya lugha ya kiswahili nakuandaawataalamu watakaoshughulikia usanifishaji wa kiswahiliPia baada ya uhuru kulianzishwa Taasisi mbalimbali zitakazoshughulikia lugha ya kiswahili.Mfano:-BAKITA, TUKI, TUMI, UKUTA, UWAVITA, Idara ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaamu.Baada ya uhuru nchini Tanzania kiswahili kilienea kwa kasi kubwa sana. Kuna sababumbalimbali ambazo zilichangia kukua na kuenea kwa kiswahili hapa nchini. Baadhi ya sababuhizo ni pamoja na:-(a) kuteuliwa kwa kiswahili kuwa lugha ya Taifa.(b) Kiswahili kitumike katika Elimu, mfano kuwa lugha ya kufundishia katika shule za msingi.© kuundwa kwa vyombo mbalimbali vya kukuza na kuneza kiswahili.(d) Kiswahili kuwa Lugha rasmi na lugha ya Taifa.(e) Kiswahili kutumika katika shughuli mbalimbali za kidini, shughuli za kisiasa na kiutawala nashughuliza kiutamaduni.(f) Uchapishaji wa vitabu na majarida mbalimbali.
- KISWAHILI KUWA LUGHA YA TAIFA
Baada ya uhuru mwaka 1962 kamati iliundwa ili kuangalia uwezekano wa kutumia kiswahilikatika shughulizote rasmi, mfano bungeni na shughuli zote za kiofisi. Pia kiswahili kiliteuliwakuwa lugha ya taifa 1964 ambapo katika shughuli zote za kitaifa zitaendeshwa kwa kutumialugha ya kiswahili.Hivyo kiswahili kilihimizwa kutumika katika mawasiliano yote hususani katika mawasiliano yotehasa katika shughuli za umma na Wizara zote, Serikali na Bunge, kiswahili kiliendelea kupandahadhi zaidi wakati wa Azimio la Arusha la mwaka 1967 kwani azimio hilo lilitungwa nakuandikwa kwa lugha ya kiswahili.
- KUUNDWA KWA VYOMBO VYA UKUZAJI NA UENEZAJI WA KISWAHILI
Tanzania baada ya uhuru ilifanya jitihada za kuunda vyombo mbalimbali vya kukuza nakueneza kiswahili katika nyanja mbalimbali mfano wa vyombo hivyo ni UWAVITA,BAKITA,TUMI,TUKI, Taasisi ya Elimu,TAKILUKI na Chama cha Kiswahili Chuo Kikuu Dar es salaam.
- KUTUMIKA KATIKA ELIMU
Kiswahili licha ya kutumika katika shughuli mbalimbali za kiserikali, kilipendekezwa kutumikaKatika shule za Msingi na kufundishwa katika elimu ya sekondari kama somo na katika vyuovikuu wanatoa shahada mbalimbali za lugha ya kiswahili. Pia katika Elimu ya watu wazimaambao hawakujua kusoma na kuandika.
Watu hawa walijifunza masomo mbalimbali kwa lugha ya kiswahili na kuwafanya watu wengikujua kusoma, kuandika na kuzungumza lugha ya kiswahili fasaha. Kampeni hii ilikuwa kwanchi nzima ambapo walijifunza elimu ya Afya, Siasa,Kiswahili, Kilimo na ufundi kwa lugha yakiswahili na kuwafanya watu wengi kuzungumzakiswahili sanifu.
- VYOMBO VYA HABARI
Tangu uhuru ulipopatikana kuna vyombo mbalimbali vya habari vilivyoanzishwa. Vyombo hivihutumika kueneza kiswahili kwa kiasi kikubwa na hufikiwa na watu wengi licha ya kuwepo kwachangamoto za kiuchumi. Vyombo hivyo ni magazeti na majarida mbalimbali ambayohuandikwa kwa lugha ya Kiswahili lakini kuna redio na runinga ambazo matangazo yakehutangazwa kwa lugha ya kiswahili. Hivyo kukifanya kiswahili kuenea kote ndani na nje ya nchi.
- BIASHARA
Shughuli za kibiashara nchini husaidia kuenea na kukua kwa kiswahili kutokana na kuwepo kwamakabila tofauti tofauti ambapo wafanyabiashara huweza kuunganishwa kwa lugha ya kiswahili.Hivyo kiswahili hudumishwa na kutumika katika biashara hizo.
- SHUGHULI ZA SIASA NA UTAWALA
Tangu wakati wa harakati za kupigania uhuru kiswahili kimetumika kama nyenzo muhimukuwaunganisha wananchi. Shughuli nzima za kisiasa zimetumia lugha hii katika kujiimarisha;mfano wakati wa chama kimoja, Azimio la Arusha na Mfumo wa vyama vingi Kiswahilikimetumika kama njia kuu ya mawasiliano.Pia katika utawala chama kinachotawala kimekuwa na harakati za kukiendeleza kiswahilli katikanyanja zote. Ambapo kiswahili kimekuwa kikitumika katika shughuli zote za kiutawala. Hivyoshughuli za kisiasa na kiutawala zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza, kukieneza nakukiendeleza kiswahili.
- UANDISHI NA UCHAPISHAJI WA VITABU
Kuibuka kwa waandishi wa vitabu mbalimbali vya kiswahili vya sarufi na fasihi ambavyovilichambua kwa kina mambo mabalimbali yahusuyo lugha ya kiswahili na utamaduni wake,mfano : Nkwera,Shabani Robart, Mathias Mnyapala na Shaffi Adam Shaffi. Waandishi wengine chipukiziwalijitokeza na wanaendelea kujitokeza katika tasnia hii ya uandishi wa vitabu.
- SHUGHULI ZA KIUTAMADUNI
Shughuli za kiutamaduni zimechangia kueneza kukuza na kuendeleza lugha ya kiswahili.Shughuli hizo ni pamoja na harusi, misiba, matanga na sherehe mbalimbali za kijamii ambazozimesaidia kukiendeleza kiswahili kwa kuwa huwakutanisha watu tofauti tofauti katika shughulihizo, ambapo huwalazimu kutumia lugha ya kiswahili katika mawasiliano na kufanya kiswahilikuendelea.Pia katika Sherehe mbalimbali vikundi vya sanaa na muziki vinavyotumia lugha ya Kiswahilikutumbuiza. Vikundi vingine huandaa nyimbo zao kwa ajili ya kukieneza kiswahili Tanzania
Mwl Maeda