09-03-2021, 04:18 PM
DOLA YA MRIMA (KILWA): ILIOKUWA TAIFA KUU AFRIKA KARNE YA KUMI (1070 A.D)
Na. Comred Mbwana Allyamtu
7/9/2016
Kilwa Masoko, Kilwa – Lindi, Tanzania.
7/9/2016
Kilwa Masoko, Kilwa – Lindi, Tanzania.
Mji wa Kilwa ni mji maarufu sana barani Afrika, najua watu wengi watashangaa kusikai nikisema Kilwa kuwa dola kubwa Afrika, yeah lazima washangae hasa hawa kizazi cha leo ambacho kwao udaku ndio habari ya mjini, mji wa Kilwa una sifa kubwa kuliko mji wowote ule Afrika, sio kwamba kwa sababu ya jina lake au ukarimu wa watu wake bali ni kwa historia yake toka zama za kale za historia ya ulimwengu pamoja na habari za wanahistoria toka duniani kote.
Bila shaka binafsi sina shaka kabisa na hili, kwa sababu nilipata bahati ya kutembelea iliokuwa miji kazaa ya Dola la Mrima yani miji ya kilwa, Tanga( mta’nga’ta), Sadani, Kaole, Zanzibar,Mombasa na Bagamoyo lakin pamoja na kujionea utajili wa kihistoria niliojionea sikusita kabisa kukubaliana na historia hiyo ya Dola la Mrima lililokuwa likipatikana pwani ya Azania na ndio Dola ililokuwa dola kuu Afrika kiuchumi, kijeshi, kisiasa na kiteknolojia.
Pia ndio dola lililokuwa na ushawishi katika ulimwengu wa zama hizo iliokuwa ukiongozwa na Dola la Rumi na baadae Dola la Hermani (Ujerumani).
Taifa la Mrima ni Dola lililo kuwa likipatikana mashariki ya bara la Afrika iliokuwa pakiitwa “Azania” na ilikuwa na miji mikubwa iliokuwa chini ya himaya ya dola hilo zaidi ya 36 kama Lamu(Amu), Mvita (mombasa), Ofiri(Sofala), Rhapta, Mafia, Unguja na Cambula (pemba), Ngozi(Mogadishu), Simayu(kisimayu) na makao makuu ya dola ilikuwa Kilwa.
Historia ya utawala wa Dola la Mrima kiutawala ilikuwa chini ya “mwinyi mkuu” (sulutani) ambaye yeye alisaidiwa na mihimili mingine ya dola.
Pwani ya Azania ni pwani ilikuwa inapatikana mashariki ya Afrika kuanzia Msumbiji ya leo mpaka Asmala(Eritria) ya leo. Azania ni neno lenye asiri ya kiarabu yani “Ajania” ikiwa na maana ya “isiyokuwa warabu”. Historia ya mwambao huu imefahamika tokea zama za mwanzo za mileniamu (1st millenia) katika kitabu cha “The periplus of Arithrean sea” unaweza kupata maeelezo zaidi ya namna gani dola ya Mrima ilivyo shamiri duniani kote.
Pia wanahistoria kama BetramThomasThomas na M.H. Dorman ambao wote kwa pamoja wameeleza kwa pamoja namna Dola hilo lilivyostawi sana.
?CHANZO CHA DOLA LA MRIMA-665 AD
Chanzo cha dola hii inaanzia kwa Hassani ibn Abduraufu (Mbega) ni moja ya watu ambao historia inaowataja kuwa viongozi wa mwanzo kuanzisha dola ya Mrima. Mbega inasadikika alikuja Azania kutokea Hijjaz na alifika mji wa mta’nga’ta (Tanga) na aliishi hapo mpaka mwaka 665 na baadae alielekea katika milima ya Usambala (kitabu cha zamani mpaka leo kilicho andikwa na taasisi ya utafiti wa kiswahili 1930) imejalibu kuelezea habali za mtuu huyu Mbega (Hassan ibn Abduraufu) kuwa aliishi Nguu huko Zigua na baadaye alielekea Kilindi alipo amua kuoa Bumbuli na baadae akawa kiongozi.
Huko “Kilindi” ilimfanya kuwa kiongozi wao baada ya kuwasaidia wakazi wa hapo kuwaondolea tatizo sugu la nguruwe pori kwani nguruwe hao walikuwa wanawatafuna watoto wachanga mpaka ilipo fikia mpaka mtoto wa kiongozi wa eneo hilo alipoliwa na nguruwe ndipo hassan ibn Abduraufu alipo fanikiwa kumaliza tatizo hilo na
Kuwafanya wenyeji kumpa jina la Mbega yani mkombozi( leberator).
Mpaka kufikia mwaka 689 alifanikiwa kusimamisha dola iliyojulikana kwa wakati huo kama Dola ya KILINDI. Makao makuu ya Dola ya kilindi ilikuwa Andeni na Dola hii ilienea tokea kwenye safu ya milima ya Usambala mpaka mombasa(mvita), Lamu(amu), mpaka Mogadishu(somalia). Pia ilikuwa na mji mikubwa kama Saadani, Pete, Tongoni, Kaole na Rhapta. Na ilipokuwa dola imara ilifahamika kama Dola la VEGA(Vega state) chini ya kiongozi alieitwa Kimweri ambaye alikuwa mjukuu wa Hassan Mbega. Na taifa(Dola) hii ilikwenda mpaka 1234 ilipo mezwa na dola jingine lililokuwa linajiimalisha (Mrima).
Dola ya Mrima ilipanuka kutokana na kile kilichoitwa mgogoro wa “Muhawiya” uliotokea bara Arabu na kupelekea idadi kubwa ya wageni kuhamia pwani ya Azania.
?VITA YA MUHAWIYA-680 A.D-685 A.D (61-64 HIJIRIA)
Hii ni vita iliyotokea katika himaya ya Uthumani (OTTOMANI EMPIRE) mara baada kharipha Ally ibn Abuu Twribu kulitokea utawala wa Banu Ummayya chini ya Muawiyya bin Abuu safiyani na baadae Yazid Bin Muawiyya wakati wa utawala huu hasa wa Yazid ulikumbwa na vita vya wenyewe kwa mda mrefu lakin wakati wa utawala huu ndio kipindi wakati dini ya uislam ilipo ingia barani ulaya (Hispania) 705-715 A.D
Lakini vuguvugu la migogoro ilizidi maradufu baina ya ukoo wa Abasi kujitenga dhidi ya ukoo wa Abuu Muslm ambaye aliungwa mkono kwa kile alichodai kuwa ni utawala wa U-calipha lazima utoke katika ukoo wa mtume muhamad (s.a.w) yani “Ahlul Bayt” lakin mwishoni Abuu Abass alishinda vita na vita kwisha 750A.D.
Katika mgogoro hiyo ya vita idadi kubwa ya wageni walihama bara Arabu na kuingia pwani ya Azania kupitia mji wa Asmara. kundi hili liliongozwa na Hamza ibn Marwani aliwasili somalia na ndio chanzo cha jamii ya (Polusa) ambaye ni miongoni mwa jamii (kabila) tatu zilizopo Somalia leo yani Olmo, Polcano na Polusa (ukoo wa Malwani).
Kundi hili ndio lililo anzisha makazi Asmara na mogadishu na baadae mwaka 780-900 A.D walipo anza kusogea mwambao wa kusini mwa pwani na hatimaye badhi yao kutia makazi Kisimayu, Lamu, Galisa katika Kenya na baadhi ya maeneo ya pwani ya Tanzania. (rejea kwenye andiko la Feeman Granville uk 35 history of East coast of africa).
?DOLA YA MRIMA (KILWA) 1300 A.D
Ukipitia andiko la Walter Rodney katika kitabu chake ” Africa development before 15C” amejalibu kuandika kwa undani namna gani dola la Mrima(kilwa) ilivyo kuwa na kuwa dola kubwa kabisa barani Afrika hata kuzidi dola zingine za afrika kama Songhai, Mali, Benin, Absinia na Ghana. Hii pia dola la Mrima ilikuwa kubwa mpaka dola kuu za dunia zama hizo kama Dola ya Rumi, Dola ya Herman na Dola ya Ottoman kuitambua dola ya Mrima kuwa ndio Dola kuu afrika. Na hata Hassan ibn Batuta alipo wasili mwaka 1300A.D alikiri kuwa
“Nilipo fika kilwa nilimkuta mtawala Wao na walinipokea kwa ukarimu mkubwa sana na walikuwa na kila kitu kama tulivyo navyo kwetu (bara Arabu)”. Hivi ndivyo kilwa ilikuwa maarufu sana. Kwani Muundo wa utawala wa Dola ya Mrima ( kilwa) ilikuwa na muundo wa kipekee ulioendana na mazingila ya kijografia ya wakati huo makao makuu ya dola la Mrima ilikuwa Kaole-Bagamoyo lakin makazi ya utawala yalikuwa Kilwa kiswani mahali ilipokuwa ikulu iliojulikana kama (Husuni).
Na mtawala wake alijulikana kama Hassan Sulyman kwa title ya Mwinyi Mkuu katika ikulu ya kilwa ndo iliokuwa ikulu kubwa Afrika kwa wakati huo kwani ilikuwa na vyumba 100 ambavyo vilikuwa vinatumika kama ofisi ya mwinyi mkuu na watumishi wake pia kulikuwa na idala malumu kama idala ya…
1-Uvuvi
2-Masoko na biashara
3-Elimu
4- uchumi
Na Afya.
1-Uvuvi
2-Masoko na biashara
3-Elimu
4- uchumi
Na Afya.
Katika Uvuvi ofisi zake za utendaji ziliwekwa eneo la Mussa Hassan ( Msasani). Masoko na biashara ziliwekwa bagamoyo(sadani). Idala ya Elimu ilikuwa Kilwa kiswani pia idala ya Afya iilikuwa Bagamoyo na ndipo ilipojengwa kituo cha Afya cha Tumbatu(shapani) na Makulunge kilichokuwa kikitoa tiba na kikiongozwa na Mtabibu Hamis mwinyi sembe shomvu alie pata elimu ya tiba katika chou cha Aveccina (Iraq) ushahidi wa habari hizi umeelezwa na Saleh Miskir toka iraq kwenye kitabu chake cha (A thousand and one night).
Katika Dola ya Mrima (Kilwa) kulikuwa na bandali marufu iliokuwa katika mji wa Rhapta hapa ndipo wafanyabiashara kutoka nje ya pwani ya Azania walifika kufanya biashara nao na pia katika uchumi dola ya Mrima (kilwa) ilikiwa tayali imesha tengeneza pesa yake ilikiwa inatumika katika biashara ya mabadilishano ya bidhaa na ndio dola pekee kwa wakati huo ilikuwa imevumbua utalatibu huo barani Afrika.
Mfano ni Hassan Ibn Batuta 1331-1333 A.D huyu alikuwa mpelelezi, msafiri, mtaalamu na Misionari wa kiarabu (kislam) aliefika pwan ya Azania katika karne ya 12C na alidhuru mji wa kilwa na Rhapta katika safar yake ambaye binafisi aliueleze mji wa kilwa na dola ya mrima kama dola kuu na kubwa iliokuwa imestalabika katika kiwango kikubwa na kutumia sarafu ya pesa katika mfumo wa uchumi (curency economy Oriented theory) kama sehemu ya mabadilishano ya bidhaa (rejea kitabu cha “Ibn Batuta” uk 143-147 chapa ya Beiruti) au vitabu kama “introduction” cha mohamed khadum, au kitabu “The incoherence for the incoherence” cha Benmon Harph Herzre chapa ya Jerusalem. Pia mwaka 1498 alipo fika Vasco Dagama pwani ya Azania alieleza namna Dola ya Mrima (kilwa) ivyo kuwa na nguvu.
?SAFARI YA VASCO DAGAMA KUJA PWANI YA AZANIA 1497 A.D
Vasco Dagama safari yake kuja pwani ya Azania ilipelekea pakubwa na uvumbuzi wa njia rahisi ya maji ya kufika India hii ilitokana na njia ya aridhi kufungwa na adui yao mkubwaa wa Dola ya Othuman (Ottomani Empire) ambaye alikuwa ametoka kushindwa kwenye vita ya msaraba (Crused War) ya ulaya hali hii ilipelekea miliki ya uthumani kupoteza makoloni yake ulaya kama Hispania jambo hili ilibidi mataifa ya uraya magharibi kutafuta njia nyingine salama kwani waliofia wafanyabiashara wake kutekwa iwapo wataendelea kutumia njia ya Constantinepoli mpaka india kwani wakati huo consatatinepoli ilikuwa chini ya Dola ya Ottomani.
?VITA YA MSALABA
Ni vita ilioanzishwa na Pope Urban II katika karne ya 13 A.D na vita hivi ilikwenda awamu nne na ilipelekea nchi nyingi zilizokuwa zinakaliwa na iliyokuwa Dola na himaya kubwa ya Uislam wakati huu ya Othumani (Ottoman Empire) ambayo ilikuwa imekalia mataifa kazaa ulaya kama Spain, Ugiliki, sehemu ya Ufaransa na sehemu ya kadha za ulaya ya kati ziliweza kujipatia uhuru. Na baadae mataifa hayo huru kuluongezeka hali ya kutokuwepo na Utengamano na kusababisha nchi hizo za ulaya kutafuta njia mbadala ya kufika India.
Ndipo Vasco Dagama alipo tumwa kutafuta njia nyingine na aliwasili pwani ya Azania mwaka 7/4/1497 alifika na merikebu yake iliokuwa ikiitwa “San Raphael” mombasa na baadae Tongoni na atimaye mji wa Kilwa. Pamoja na safari hii ya Vasco Dagama kilwa pia aliandika kwenye andiko lake habari za Mrima ( kilwa) kilichoitwa “Sarade san Raphael” yani ‘milima ya raphael mtakatifu’ inayopatika kwenye kitabu cha Kesteloot uk 86. Ndai yake Vasco Dagama kaelezea wazi kuwa dola ya Mrima(kilwa) ilikuwa dola kubwa na yenye pesa yake katika uchumi na utawala wake wenye nguvu. Hali hii ilimfanya Vasco Dagama kupeleka taalifa nchini mwake Ureno iliosababisha kuandaliwa kwa utaratibu ya utawala na uvamizi wa ureno pwani ya Azania.
?UVAMIZI NA KUANGUKA KWA DOLA YA MRIMA (KILWA)
Kutokana na ujio wa Vasco Dagama uliopeleka kuandaliwa utalatibu wa kupanua himaya ya Ureno ndipo Ureno ipo agiza jeshi la uvamizi pwani ya Azania kikosi kilicho ongozwa na kamanda Fransisco D’ Almenda ambacho kilianza safari na kuwasili kilwa tarehe 22/7/1505 akiwa na merekebu 22 zilizo jaa wanajeshi 1500 na siraha za kutosha ikumbukwe kwamba safari hii ya D’ Almeida ilikuwa tayali imeshatanguliwa na ile ya mashushushu ambao walikuwa tayali wapo mjini kilwa na tayali walikuwa wakiishi hapo mfano ni shushushu mreno aliejulikana kama Antonio Fernandes ambaye aliishi Kilwa kwa mdaa na kufanikiwa kuandaa wasaliti kazaa akiwemo mtu mzalendo wa kilwa aliejulikana kama Mohamed Ankoni. (Rejea kitabu “History of Africa” uk 129-135, Kelvin Shillington).
Kupitia ujasusi huu uliokuwa umeandaliwa na wareno mapema ulifanikisha mpango wake wa uvamizi (rejea kitabu “history of East Africa up to 19C. Uk 77)
1505 uvamizi ulianza katika miji mbalimbali ya pwani ya Azania ikiwa ni sambamba na ujenzi wa ngome za Ureno mfano wa ngome hizo ni ngome ya Ureno kilwa kiswani na Ngome ya Yesu iliopo Mombasa. Binafsi nilipata bahati ya pekee kabisa kama ilivyo kasumba yangu ya kupenda kutembelea (travelogy adventure) vivutio mbali mbali napokuwa ndani na nje ya nchi ili angalau niweze kujifunza jambo (perspective analysis).
Hivyo basi nilipo pata fursa ya kutembelea mji wa Mombasa mwaka huu ilikuwa tarehe 16/1/2016 na nilifika mahali ilipo ngome inayoitwa ngome ya yesu (Fort Jesus) mantiki ya kutoa kisa hiki cha kuzuru mahari hapo ni kujalibu kukuonesha namna ya Dola la Mrima namna lilivyo polomoka kwa usiku mmoja (siku chache) ukilinganisha na masiku lilivyojengwa kwa miaka isiopungua 200. Katika safari yangu katika eneo hilo la kihistoria mahali hapo panaofahamika kama Ngome ya Yesu (Fort Jesus) ndipo aliekuwa mwanamakumbusho (museulogist) alipo nipa simlizi ya kusisimua na iliyopelekea kudondoka kwa iliyokuwa dola ya Mrima (kilwa) ya pwani ya Azania.
Kwa mujibu wa maelezo ya msimulizi huyo uvamizi huo ulikuwa na sura mbili (2) na ulifanyika kwa awamu nne (4) .
?SURA YA 1
?AWAMU YA I.
Ilikuwa ni mnamo mwaka 1506 ambapo jeshi la ureno likiongozwa na kamanda fransisco D’ Almeida akiwa na jeshi alivamia mji wa kilwa mafia na baadae ZANZIBAR. Na ZANZIBAR kukawa eneo la kwanza la kireno kuwa chini ya himaya yake chini ya capteni Ruy Lourenço Ravasço.
Ilikuwa ni mnamo mwaka 1506 ambapo jeshi la ureno likiongozwa na kamanda fransisco D’ Almeida akiwa na jeshi alivamia mji wa kilwa mafia na baadae ZANZIBAR. Na ZANZIBAR kukawa eneo la kwanza la kireno kuwa chini ya himaya yake chini ya capteni Ruy Lourenço Ravasço.
?AWAMU YA PILI.
Awamu hii mnamo mwaka 1510 uvamizi ulifanyika kutokea kusini yani Sofala kuja mpaka kwenye visiwa vya “Mayote, Mororoni na Anjuani” jeshi hili liliongozwa na kapteni Vermudezi. Kikosi hichi ndicho kilichoenda kutia nguvu baadae Mombasa.
Awamu hii mnamo mwaka 1510 uvamizi ulifanyika kutokea kusini yani Sofala kuja mpaka kwenye visiwa vya “Mayote, Mororoni na Anjuani” jeshi hili liliongozwa na kapteni Vermudezi. Kikosi hichi ndicho kilichoenda kutia nguvu baadae Mombasa.
?AWAMU YA TATU.
Kikosi hiki kiliongozwa na kamanda D’ Almeida kufanya maangamizi eneo la kilwa, mafia na pemba (kamablu). Mwaka 1513 A.D
Kikosi hiki kiliongozwa na kamanda D’ Almeida kufanya maangamizi eneo la kilwa, mafia na pemba (kamablu). Mwaka 1513 A.D
? AWAMU YA NNE.
Hiki ndiko kilicho ongoza uvamizi kuanzia Malindi, lamu, pate, kismayu, Barawa na Mogadishu. Mwaka 1509-1516 A.D
Hiki ndiko kilicho ongoza uvamizi kuanzia Malindi, lamu, pate, kismayu, Barawa na Mogadishu. Mwaka 1509-1516 A.D
?SURA YA 2
Katika sura hii ni ule vamizi wa mji wa kilwa ambao kulitokea patashika ya mapambano. Na wanahistoria kadha pamoja na wakazi ambao wamelithi habali toka kwa kizazi kilicho ishi hapa huelezea kuwa baada ya uvamiz wa kilwa ndipo viongozi wa dini wakiongozwa na mtu aliefahamika kama Hassani mwnyipembe walifanya maombi matakatifu kwa zaidi ya masaa 9 hali iliyopelekea maajabu makubwa sana majabu hayo yapo yanaishi mpaka leo moja ya maajabu hayo ni …..
1- zile merekebu zilizokuwa pale songo mnara ziligeuka kuwa ” Majabali” na mabaki ya merekebu hizo ambazo ziligeuka kuwa majabali huonekana leo hasa ukiwa unatokea Dar es salam kuelekea Mtwara ambapo siku hizi kumewekewa taa nyekundu ili kuwaongoza mabaharia wasigonge miamba hiyo iliyokuwa merekebu na kugeuzwa kuwa Miamba.
2- pia kundi la wenyeji 100 ambao walikuwa wasaliti pia wamegeuka kuwa “Vichuguu” na mpaka leo huonekana pale msitu wa Mikoche ( mikoche historical site) pale kilwa kiswani ambapo hivyo vichuguu 100 vinavyo aminika kuwa walikuwa wasaliti huonekana hadi leo. Na ningependa kuwasihii kuwa iwapo utapata wasaa basi ebu tembele miji hii ikiwa ni pamoja ha eneo hili ili ili uweze furahia wingi wa maajabu na historia hii ambayo mimi Mbwana Allyamtu binafsi nilifarijika sana.
Lakin katika kipindi cha uvamizi huu Dola ya Mrima ilajalibu kuomba msaada toka consatatinepoli lakin msaada haukufua dafu kwani merikebu zao zilekuwa ndogo ukilinganisha na za wareno ambazo walukuwa wamejipanga kiasi cha kutoshakutosha kwani mashambulizi haya yaliacha athari kubwa na mbaya sana kama
“Vifo, uharibu wa miji na mali zao, kuangamiza kabisa baadhi ya miji kama Rhapta ambao uliangamia na kupotea kabisa mpaka ulipo kuja kuthibitika tena kwa mujibu wa kitabu (A Guide to Tongoni Ruins cha A.A.Mturi) kinachosema “The ruins of Rhapta are yet to be found though it is generally agreed tha the town was situated on Tanzania coast” yani ” mabaki ya mji wa Rhapta umeptikana tena kwa makubaliano ya pamoja kwamba kunauwezekano mkubwa wa mji huu ulikuwa pwani ya Tanzania”.
Mpaka kufika mwaka 1599 tayali ngome yote ya Mrima (kilwa) ilikiwa tayali imekaliwa na Ureno na kuifanya ngome ya Kiswahili ya Azania (Mrima) kuangushwa na kuwa chini ya Ureno ambapo utawala huu ulidumu takribani kwa miaka 100 bila maasi ya kujikomboa mpaka mwaka 1698 mapambano ya kujikomboa yalipo anza tena na kuifanya Ureno kuanza kuachia baadhi ya ngome za Mogadishu, Mombasa mpaka ZANZIBAR na kilwa na kuifanya Ureno kuludi nyuma na kubakia Sofala- mozambiq( musa bin beq) na kuamua kujizatiti na kujikita kiutawala huko amabapo utawala wake ulidumu kwa zaidi ya miaka 500 huko mpaka walipo kuja kuanza harakati za kujikomboa mwaka 2/6/1960 chini ya Eduardo Mondlande nakujikomboa kabisa kuwa huru mwaka 1975 chini ya “FRELIMO ya Samora Machel.
Watawala wa Dola ya Mrima (kilwa) kuanzia mtawala wa kwanza mpaka mwsho pale ilipo dondoka dola ya mrima jumla walikuwa ni “50” yani kuanzia mtawala wa kwanza Mwinyi mkuu Hassan bin Ali.(Allyamtu) mpaka na wa mwisho (50) yani ambaye uvamizi na utawa wa kireno ulipo shinda na kumuangusha alikuwa ni Mwinyi mkuu Said ibn Mwinyi.
?MWISHO.
Naomba nitangulize shukrani zangu za dhati kwa mwenyezi Mungu mwingi wa rehema (Allah) kwa utukufu wake kwa ulimwengu na mbingu yote na vyoye vilivyomo ndani yake.pia na pamoja na shukurani hizo za pekee kabisa pia naomba nipeleke shukurani zangu kwa wadau wangu wote ambao kwa pamoja wamenipa ushilikiano wa kufanikisha kuandika andiko hili langu kwa kiwango kikubwa japo kwa uchache tu japo natambua kuwa ni wengi kwa idadi lakin nyote nawashukuru kwa utukufu mkubwa kabisa.
Naomba nitangulize shukrani zangu za dhati kwa mwenyezi Mungu mwingi wa rehema (Allah) kwa utukufu wake kwa ulimwengu na mbingu yote na vyoye vilivyomo ndani yake.pia na pamoja na shukurani hizo za pekee kabisa pia naomba nipeleke shukurani zangu kwa wadau wangu wote ambao kwa pamoja wamenipa ushilikiano wa kufanikisha kuandika andiko hili langu kwa kiwango kikubwa japo kwa uchache tu japo natambua kuwa ni wengi kwa idadi lakin nyote nawashukuru kwa utukufu mkubwa kabisa.
Ambapo mmefanya niweze kulikamilisha jambo hili (andiko hili la nyumbani Azania) lenye mvuto na msisimko wa pekee kabisa kwa wakati. Lakin pia naomba kuwashukuru Bwana Alfosi wanjilu (Mombasa historical site) toka Kenya, Abdala msumbuko (Kaole historical site) bagamoyo na bibi aisha zuberi kutoka kiliwa historical site. Ambapo kwa pamoja mmefanya niandike makala hii kwa mvuto wa pekee kabisa kwani nimeandika yale ambayo nimeyaishi na kuyashuhudia kutoka kwenye ziara ya kujionea na kushuhudia historia ya miji hiyo.
Watafiti wengi na wanahistoria wengi sasa wanakubaliana kuwa Dola ya Mrima (kilwa) kuanzia mnamo miaka ya 967 mpaka 1399 A.D ndio ilikiwa dola kubwa ukanda wa kusini wa bara la Arabu na Ulaya. Pia ndio iliokuwa dola la 4 kwa “Ushawishi wa Dunia ya wakati Ule” ikiwa nyuma ya Dola la Rumi (ROME EMPIRE) Dola la Sackxoni (HEREMAN EMPIRE) Dola la Uthumani (OTTOMAN EMPIRE) na Dola la Mrima-(kilwa) (MRIMA EMPIRE)
Lakini kutokana na hira au ubinafsi wa wasomi wa kizungu (Eurocentric views) kwa makusudi wamefunika kabisa historia hii na kuifanya isaulike kabisa hata bila soni moyoni mwao lakin pia hata nchi yetu imeshindwa kuitambua historia hii kwa upana wake na kuifanya kuwa chanzo cha muhimili wa taifa letu la Tanzania katika historia na uchumi.
Pia kasumba hii imeathili mataifa yote yani Kenya, Somalia, Msumbiji na hata Tanzania wote wameshindwa kuenzi historia hii ili iwe ni urithi wa vizazi vyetu na duniani kwa ujumla kwani wenzetu Ugiliki na italia na mataifa mengine ya ulaya wamegeuza historia kuwa ni moja ya muhimili muhimu sana wa uchumi mfano tu kwa Ugilki kwani Ugiliki pekee huingiza Us$ 11.4 bilion( kalibu Tsh 26 Trilion) kwa mwaka kwajili ya ulithi wa tathinia nzima ya historia.
Kwanin sis tusiwekeze kwenye hili? Natamani sana kuendelea kuandika juu ya upembuzi yakinifu juu ya kile kinachoitwa kuwekeza kwenye “Curiosity asset” yani vitu vyenye urithi na manufaa ya pekee kabisa na vyenye mvuto wa hari ya juu. Hivyo basi itanibidi kwa naman yoyote ili niishie hapa kwa maana ya kuwa nitatafuta wasaa mwingine wa kuliandikia hili la kuwekeza kwenye “Urithi wa dunia” kwa upana wake.
Japokuwa kulieleza hili ni jambo la muhimu sana itanibidi sasa niandae makala ambayo nitaishauli serekali yangu tukufu ya Tanzania namna ya kuwekeza kwenye eneo hili ili tuweze kunufaika na historia ya Dola la Mrima (kilwa) kupitia kwenye nyanja za kiuchumi, kisiasa, kielimu na kifahali kama Taifa.
Sasa ningependa kuitua kalamu yangu kwa nukuu ya Mtawa (mwasisi) wa Dola la Rumi (Roma Empire) JURIUS KAISAR alisema ” Enzi ni fahali kwa jamii kama itakukumbusha ufahali wako kwa jamii nyingine na ukubwa wa jamii(Dola) yako kwani hukufanya uwe na sauti kwa jamii nyingine iwapo kama utaenzi iyo hadithi kipindi ambacho hauko nayo tena huo umiliki wako lakini utawafanya muwe mafahali kwa vizazi vingi vijavyo” 368 BC
?”MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU BARIKI KIZAZI CHETU NA FIKRA ZAKE”
NDIMI: COMRED MBWANA ALLYAMTU
© copy rights reseved
®written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika kwa mawasliano
™Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
®written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika kwa mawasliano
™Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234
+250733153930
+250788214234
Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail. Com
Mwl Maeda