MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

VIPENGELE VYA ELIMU MITINDO - Printable Version
|
VIPENGELE VYA ELIMU MITINDO - Printable Version
+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9)
+--- Thread: VIPENGELE VYA ELIMU MITINDO (/showthread.php?tid=666)
|
VIPENGELE VYA ELIMU MITINDO - MwlMaeda - 07-28-2021
Leo tutazungumzia vipengele viwili:
Mchomozo
na
Ukengeushi
Katika Maisha ya kawaida - Watu wanaoanza kupendana. Kuchumbiana.
- Hufanya nini ili kila mmoja kumpendezesha mwingine?
- Mavazi
- Mikogo
- Mazungumzo: utumiaji wa lugha ISIYO YA KAWAIDA ili kumvutia mwenzako
- Maisha ya kawaida Vyumbani/ Vijijini/ nk
Mchomozo ni nini?
- Ni kitu gani cha kawaida, hapa kimefanywa si cha Kawaida?
- Kwanini si cha kawaida?
- Jambo la kawaida, linafanywa KUONEKANA kuwa SI LA KAWAIDA.
- Sote tunajua GOOGLE
- Nini tunachokiona hapa? Na kina athari ipi?
Kawaida kufanya si Kawaida
- Vijijini ni kawaida kuona watu wenye makaptula yaliyochanika
- Siku hizi Vyuoni ni kawaida wanafunzi kutafiti kwa kutumia Google
- Lakini hapa ni nini si cha kawaida? Kutoka katika Ukawaida huo?
Chanzo – Wanaurasimi wa Kirusi - Wanaurasimi/ Usanifu wa Kirusi walishikilia kuwa sababu kuu ya kuwapo kwa sanaa na fasihi ni ili kuyafanya mambo ya kawaida yaonekane kuwa si ya kawaida.
- Katika huu usokawaida, kipengele fulani hujichomoza kutoka katika ile kawaida iliyozoeleka. Kipengele cha lugha au cha kisanaa katika fasihi.
- Tuangalie Usanii Huu. Making strange
MCHOMOZO – foregrounding…/2 - Mchomozo ni ujitokezaji wa vipengele vya KIISIMU katika muktadha mahsusi wa KIFASIHI kwa wingi, uchache au kutokutokea kabisa kulingana na kaida ilivyo.
- Mbinu za Kiisimu katika Fasihi ambazo kutokana na zilivyowekwa, humfanya msomaji kuvutwa kutoka katika kuangalia jambo LINALOSEMWA, kuangalia LINASEMWAJE
Mbinu za Kiisimu - SAUTI – Kushusha au Kupandisha. Au Kimya!
- Kicheko, Kilio, Ukelele (Mf. Katika Mashetani)
- MANENO – Kuweka neno fulani ambapo halikutarajiwa. {Shetani anamwambia Binadamu amuue – Mashetani}
- Hebu sikiliza na angalia mtu huyu anavyotoa salamu. Maneno anayoyaongea ni ya kawaida.
- Kwa nini tunasikia/ kuona usokawaida?
- HAMJAMBO?
Mifano zaidi ya Mchomozo………..
[*]Sikiliza maongezi ya Pazi na Tendegu ktk TENDEHOGO. Uk 1 – 3.
[*]Dhana ya Ubora Vs Udhaifu Maana ya Umoja ni Nguvu imesemwa kwa namna gani? Imesemwa kwa mfano wa Ubora Vs. Udhaifu
[*]Angalia mchomozo wa kikejeli katika “Cha Mnyonge” uk 89.
[*]
[*]Katika FASIHI
- Katika Fasihi, ili tuone mchomozo, hatuna budi kuangalia matokeo yake.
- Mchomozo unaweza kujitokeza kwa namna mbili: Ukengeufu na Usambamba.
- Katika UKENGEUFU/UKENGEUSHI Kuna vijitawi vingine.
- Katika Tamthilia: Ukengeushi
- Katika Ushairi: Ukiushi
[*][*]MATOKEO YA MCHOMOZO
[*]
[*]Ukengeufu/ Ukengeushi – alienation
[*]Hasa katika tamthilia. Kuifanya hadhira ijitenge na dhana ya mchezo irudi katika uhalisia wa maisha.
[*]“Hodi” ktk Heshima yangu.
[*]Sauti ya Kichaa, Kichaa ktk Pambo
[*]Ukiufu/Ukiushi – deviation
[*]Mabadiliko katika mpangilio wa lugha ili kukiuka ukawaida. Ukiushi huu hufanywa sana na Washairi au Waandishi.
[*][*][*]Ukengeushi
- KUMBUKA TUNAZUNGUMZIA MATOKEO
- Ni athari inayotokea wakati hadhira inaporudishwa katika uhalisi wa maisha kutoka katika hisia za kimchezo/ kifasihi.
- Kila wakati tunakumbushwa kuwa kuna hali halisi ambayo inaigizwa katika jukwaa (au inahadithiwa katika riwaya).
- Tazama KULI 132 mazungumzo baina ya Rashidi na Amina.
- Unapozama ktk hisia kuna ukengeushi unatokea na kukurudisha ktk hali halisi.
- Wimbo ktk Hadithi ya Cha Mnyonge utakitapika hadharani, ni aina ya ukengeushi.
- UKIUSHI
- Katika Ushairi hutumia pia taswira. Jazanda ya kawaida ambayo inawekwa kinyume cha mambo.
- HASA KATIKA USHAIRI na Vichwa cha Tamthilia au Riwaya:
- Lina Ubani (Kawaida ni Nini)
- Mvumilivu Hula Mbovu
- Asali Chungu
- Sukari yenye sumu n.k
- Kwesho tutaongelea Usambamba na Ukariri
[*][*][*]
[*]Usambamba
[*][*][*]
[*]Usambamba wa matukio
[*]Usambamba wa sauti, neno, sentensi, wazo
[*]Angalia usambamba katika Kusadikika 1 na 2.
|