SHAIRI: SIMBA KUMJIBU PAKA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: SIMBA KUMJIBU PAKA (/showthread.php?tid=558) |
SHAIRI: SIMBA KUMJIBU PAKA - MwlMaeda - 07-15-2021 Simba awapo nyikani – yeye si wakutishika,
Huwataka hayawani – mbuaji kwenye machaka,
Si viumbe vya bandani – vimtie kushutuka,
Simba kumjibu paka – nikujitowa thamani
Akaapo hadharani – kucha zake hufinika,
Mfano kiumbe duni – ela kwa yeye kutaka,
Vimbelembele pembeni – havimpi kusumbuka,
Simba kumjibu paka – nikujitowa thamani
Atembeapo ndiani – si wakupekwa haraka,
Anapishwa hapishani – apandapo na kushuka,
Wakuuliza ni nani – amuwekee mipaka,
Simba kumjibu paka, nikujitowa thamani
Huchaguwa ushindani – si huo wa vijipaka,
Ati pamoya ngondoni – na kuanza patashika,
Hilo litakuwa shani – na nimuhali kutuka,
Simba kumjibu paka – nikujitowa thamani
Kwenye mijusi kutani – ndiko kwa paka hakika,
Na kina panya tobweni – wamjibu akitaka,
Asijitie kundini – ya simba akayataka,
Simba kumjibu paka – nikujitowa thamani
2020.02.26, Yakubu Julius, Nairobi
|