TAALUMA YA ISIMU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: TAALUMA YA ISIMU (/showthread.php?tid=478) |
TAALUMA YA ISIMU - MwlMaeda - 07-09-2021 MUKHTASARI WA DHANA YA TAALUMA YA ISIMU
Wanaisimu wengi wamejaribu kufasili dhana ya isimu .kwa mfano , Richards et al (1985) anasema kuwa :
Isimu ni mtalaa ambao huchunguza lugha kama mfumo wa mawasiliano ya mwanaadam (TY) Hartman (1972) naye anasema: Isimu ni eneo maalum la mtalaa ambalo lengo lake huwa ni kuchunguza lugha .Wanaisimu huzichunguza lugha zikiwa ni nyenzo muhimu za mawasiliano ya mwanaadamu. (TY). Verma et al (1989)wanasema kuwa isimu ni sayansi kwa sababu hufuata mbinu za kimsingi za utafiti wa kisayansi.Mbinu hizi huhusisha sifa zifuatazo. 1. Uchunguzi uliodhibitiwa 2. Uundaji wa haipothesia 3. Uchanganuzi 4. Ujumlishi 5.Utabiri 6.Majaribio na uthibitishaji 7. urekebishaji au ukataaji wa haipothesia Hii ni kusema kuwa isimu haichunguzi lugha kiholela bali kwa uratibu na mwelekeo maalumu.katika kuchunguza lugha ,wanaisimu hutumia misingi ya kisayansi kama zifanyavyo sayansi zingine. TUKI (1990) wanasema kwa ufupi kabisa sana Isimu ni sayansi ya lugha. MATAWI YA SAYANSI Isimu historia Isimu fafanuzi Isimu linganishi isimu jamii isimu tumizi isimu nafsia. USAYANSI WA ISIMU Utoshelevu wa kiuteuzi Utoshelevu wa kiuchunguzi utoshelevu wa kiufafanuzi Uchechevu Uwazi MISINGI YA USAYANSI WA ISIMU Uwazi Utaratibu Urazini MAREJEO Mgullu,R.S. (1999) Mtalaa wa Isimu Fonetiki,Fonolojia na Mofonolojia ya Kiswahili.Longhorn Publishersar es salaam,Tanzania. Habwe,J. na wenzake (2004) Misingi ya sarufi ya kiswahiliPhoenix Publishers :Nairobi,Kenya. |