ETIMOLOJIA YA NENO 'BAFTA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BAFTA' (/showthread.php?tid=2602) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'BAFTA' - MwlMaeda - 06-19-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAFTA' Neno *bafta* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya kitambaa cheupe kinachotengenezwa kwa nyuzi za pamba. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bafta* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *'baftah*( *soma: baftatun/baftatan/baftatin بفتة )* ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana kitambaa cha hali ya juu kilichotengenezwa kutokana na nyuzi za pamba. Vitambaa vya *bafta* ni mashuhuri sana nchini India na hutumika kushona suruali na mashati. Kinachodhihiri ni kuwa neno *'baftatun بفتة* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bafta* halikubadili maana yake katika lugha ya Kiarabu. *TANBIHI:* Nomino *bafta* ni neno *lililoarabishwa* kutoka lugha ya Kifaransa likiwa na maana ya nguo iliyoshonwa, nyuzi zilizosokotwa, busati, aina ya nguo iliyotengenezwa kutokana na pamba, kitambaa kinachotokana na sufi. Nchini Misri *bafta* ni kitambaa cha hali ya juu kilichotengenezwa kutokana na pamba nyeupe. Nchini Syria *bafta* ni kitambaa kilichotokana na hariri. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |