MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI' (/showthread.php?tid=2586)

ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI' - MwlMaeda - 06-02-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI'

Neno *mahari*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: ya-/ya-]* yenye maana ya mali anayotoa mwanamume na kuwapa wazazi wa mwanamke anayetarajia kumwoa; mali au fedha itolewayo na wazazi wa mwanamume kwa wazazi wa msichana anayetaka kuolewa.

Neno *mahari* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *mahrun/mahran/mahrin مهر* lenye maana kile anachotoa mume kumpa mkewe kwa ajili ya kufunga ndoa kati yao.

Neno lingine la Kiarabu lenye maana ya mahari ni *swadaaqu صداق.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *mahrun مهر* lilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *mahari*  maana yake katika lugha asili - Kiarabu haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*