ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANA' (/showthread.php?tid=2544) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANA' - MwlMaeda - 05-06-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANA' Neno *amana* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo: 1. Kitu anachokabidhiwa mtu kwa utaratibu maalumu ili akihifadhi kwa muda na kukirejesha kwa mmiliki kitakapohitajika. 2. Kiasi cha fedha kilichowekwa benki; *akiba* . 3. Kitu chenye thamani kubwa. Katika lugha ya Kiarabu neno *amana* linatokana na neno la Kiarabu *amaanah (soma: amaanatun/amaanatan/amaanatin امانة)* lenye maana zifuatazo: 1. Kusalimika, nomino inayotokana na kitenzi cha Kiarabu *amina امن* amesalimika. 2. Akiba. 3. Hali ya kuhifadhi upendo na kutekeleza ahadi kwa namna inavyopasa. 4. Alichokifaradhisha (alichokifanya lazima/wajibu) Mwenyeezi Mungu kwa watu. 5. Msimamo thabiti na ukweli. 6. Chombo cha uendeshaji na usimamizi wa shughuli za taasisi, chama, jumuiya *al-amaanatul aamah الأمانة العامة* ofisi ya Katibu Mkuu; *Sekretarieti*. 7. Mamlaka ya usimamizi wa mji mkuu, *amaanatul aaswimah عاصمة العاصمة.* Kinachodhihiri ni kuwa neno *amaanatun امانة* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *amana* lilichukua baadhi ya maana za neno hili katika lugha asili - Kiarabu na kuyaacha mengine. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |