ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANI' (/showthread.php?tid=2521) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANI' - MwlMaeda - 04-20-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANI' Neno amani katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo: 1. Hali ya kuwapo utulivu dhidi ya usumbufu 2. Hali ya kuwa na usalama na utulivu; kutokuwa na vita au vurugu (machafuko) yoyote. 3. Makubaliano ya usalama baina ya nchi zenye vita. Katika lugha ya Kiarabu neno amani linatokana na neno la Kiarabu amaanun (soma: amaanun/amaanan/amaanin أمان) lenye maana zifuatazo: 1. Kusalimika; usalama; jina linalotokana na Kitenzi cha Kiarabu amina امن amesalimika. 2. Hali ya kuwapo utulivu. 3. Ahadi; makubaliano baina ya watu wawili au watu wengi. 4. Ulinzi. 5. Ukweli; kutokuwapo udanganyifu au dhulma. Kinachodhihiri ni kuwa neno amaanun امان lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno amani maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu inayohusu usalama na utulivu haikubadilika na maana ya makubaliano baina ya nchi zenye vita iliongezwa. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |