MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AMANI'

Neno amani  katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo:

1. Hali ya kuwapo utulivu dhidi ya usumbufu

2. Hali ya kuwa na usalama na utulivu; kutokuwa na vita au vurugu (machafuko) yoyote.

3. Makubaliano ya usalama baina  ya nchi zenye vita.

Katika lugha ya Kiarabu neno amani linatokana na neno la Kiarabu  amaanun (soma: amaanun/amaanan/amaanin أمان) lenye maana  zifuatazo:

1. Kusalimika; usalama; jina linalotokana na Kitenzi cha Kiarabu amina امن amesalimika.

2. Hali ya kuwapo utulivu.

3. Ahadi; makubaliano baina ya watu wawili au watu wengi.

4. Ulinzi.

5. Ukweli; kutokuwapo udanganyifu au dhulma.

Kinachodhihiri ni kuwa neno amaanun  امان  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno amani maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu inayohusu usalama na utulivu haikubadilika na maana ya makubaliano baina ya nchi zenye vita iliongezwa.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)