ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHRAFU' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHRAFU' (/showthread.php?tid=2514) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHRAFU' - MwlMaeda - 04-17-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHRAFU' Neno *bashrafu* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya *muziki unaopigwa kwa ala tupu bila ya maneno.* Katika lugha ya Kiarabu neno *bashrafu* linatokana na neno la Kiarabu *bashrafu (soma: bashrafun/bashrafan/bashrafin بشرف)* lenye maana ya *utangulizi wa muziki unaopigwa kwa ala tupu bila ya maneno.* Kinachodhihiri ni kuwa neno *bashrafun بشرف* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bashrafu* maana yake ya msingi katika lugha ya Kiarabu haikubadilika. *TANBIHI:* Ingawa Waswahili wamesajili etimolojia ya neno hili *bashrafu* kuwa Kiarabu, uchunguzi wa asili ya maneno umebaini kuwa neno hili etimolojia yake ni *Kifursi/Kiajemi* na Waarabu wamelichukua huko. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |