Aina za Vitendawili - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Semi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=49) +---- Thread: Aina za Vitendawili (/showthread.php?tid=25) |
Aina za Vitendawili - MwlMaeda - 06-15-2021 a) Vitendawili sahili ni vifupi na huwa na na muundo mwepesi kueleweka. K.v.
b) Vitendawili mkufu huwa na vipande vinavyofuatana na kila kipande huwa na uhusiano na kipande kilichotangulia. Mfano “ nikisimama anasimama, nikiketi anaketi, nikiondoka huondoka pia”
c) Vitendawili vya tanakali hutumia tanakali za sauti Mfano: Drrrrrrh mpaka ng’ambo “buibui”; huku ng’o na kule ng’o.
d) Vitendawili sambamba huwa na maelezo marefu (kama hadithi fupi) halafu jibu lake huwa ni refu pia (kama mafumbo)
|