ETIMOLOJIA YA NENO 'MAKALA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'MAKALA' (/showthread.php?tid=2461) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'MAKALA' - MwlMaeda - 03-16-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MAKALA' Neno *makala* katika lugha Kiswahili *Nomino [Ngeli: ya-/ya-, pia i-/zi-]* yenye maana ya andiko kuhusu mada fulani ya kutolewa gazetini, katika jarida, kitabuni au kuwasilishwa kwenye mkutano, kongamano na kadhalika. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *makala*( *soma: maqaalatun/maqaalatan/maqaalatin مقالة)* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Andiko (utafiti) kuhusu Sayansi, Fasihi, Siasa au jamii linalotolewa kwenye jarida au gazeti, yaani: *maqaalatun siyaasiyyatin مقالة سياسية* makala ya kisiasa, *maqaalatun ilmiyyatun مقالة علمية* makala ya kisayansi/kitaaluma. 2. Tendo-jina *masdar مصدر* ya kitenzi *qaala قال* amesema; kauli. 3. Andiko kutoka kitabuni. 4. Msimamo wa kielimu/kitaaluma; *madhehebu* . Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *maqaalatun/maqaalatan/maqaalatin مقالة )* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *makala* lilichukua kutoka lugha yake ya asili - Kiarabu maana ya andiko kuhusu mada fulani ya kutolewa gazetini, katika jarida, kitabuni au kuwasilishwa kwenye mkutano, kongamano na kadhalika na kuziacha maana za *kauli* na *msimamo wa kielimu/kitaaluma*. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |