ETIMOLOJIA YA NENO 'AKHERA'/'AHERA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AKHERA'/'AHERA' (/showthread.php?tid=2453) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AKHERA'/'AHERA' - MwlMaeda - 03-10-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AKHERA'/'AHERA'. Neno akhera/ahera katika lugha Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. Nomino [Ngeli: i-/zi-] maskani ya roho za viumbe zinapokwenda baada ya kifo. Roho za wanadamu wote zitakuwa ahera (akhera) kusubiri siku ya Kiyama (Kisimamo kwa ajili ya kuhukumiwa). 2. Nomino [Ngeli: i-/i-] kule ambako inaaminika binadamu wataishi baada ya kufufuliwa. Nahau: enda ahera (akhera): kufa. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ahera/akhera( soma: aakhiratun/aakhiratan/aakhiratin آخرة) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Maskani yatakayobakia milele baada ya kufa; kinyume cha dunia. Imeandikwa katika Qur'aan Tukufu, Sura ya 3 (Surat Aali Imraan, Aya ya 152 kuwa: Minkum man yuriidud Dun-yaa wa minkum man yuriidul aakhirata. منكم من يريد الدنيا ومنكم من يريد الآخرة (Yupo miongoni mwenu anayeipenda Dunia , na yupo miongoni mwenu anayeipenda Akhera ). 2. Mwisho. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu aakhiratun/aakhiratan/aakhiratin آخرة) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno ahera/akhera halikubadili maana yake katika lugha yake asili - Kiarabu. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |