JINSI YA KUTAMBUA MZIZI/KIINI KATIKA NENO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: JINSI YA KUTAMBUA MZIZI/KIINI KATIKA NENO (/showthread.php?tid=1566) |
JINSI YA KUTAMBUA MZIZI/KIINI KATIKA NENO - MwlMaeda - 11-27-2021 Mzizi au kiini cha neno huweza kubainika kwa kutumia mbinu zifuatazo:
Neno husika hufanyiwa mnyambuliko kwa kubadili viambishi kadiri iwezekanavyo na kisha kuchunguza sehemu isiyobadilika katika maneno yaliyotokana na mnyambuliko (vinyambuo).
Mf:Cheza ——- Mchezo Mchezaji Michezo -chez- Tumecheza Walivyotuchezesha
Mbinu hii hufaa zaidi kwa maneno ambayo ni nomino. Nomino zisizo na umoja na wingi aghalabu huwa ni maneno yaliyoundwa kwa mofimu moja hivyo si rahisi kupata mzizi na viambishi.
Mf:Mtoto ——– watoto (toto) Mzee ——— wazee (zee) Kifaranga —– vifaranga (faranga)
Vitenzi vingi vya Kiswahili huwa na muundo ndani na muundo nje. Ili kutambua mzizi wa kitenzi kwa urahisi ni vyema kukirudisha kitenzi katika muundo wake wa ndani. Kitenzi chenye asili ya kibantu muundo wake wa ndani huishia na irabu “a”. Kitenzi kikiwa katika muundo ndani na kuishia na irabu “a” basi hiyo irabu ikiondolewa kinachobakia huwa ndio mzizi.
Mfano:Walipigana —————- piga ——– pig- Tumemuimbia ———— imba ——- imb- Wanasomeshwa ———- soma ——- som- Iwapo kitenzi katika muundo wake wa ndani kitaishia na irabu tofauti na “a” basi yawezekana neno zima likawa mzizi au shina. Hali hiyo hutokea kwa vitenzi vyenye asili ya kigeni. Mfano: Waliosaliana ———- Sali Walivyostarehe ——- starehe Tulimuarifu ———— arif |