SHAIRI: UTU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: UTU (/showthread.php?tid=1490) |
SHAIRI: UTU - MwlMaeda - 11-14-2021 UTU Siku hizi ukitaka kupona utapona kwa pesa, Utakufa bure, Kufa ni rahisi kuliko kupona! Wakati ukipambana na afya ya mwili, Wao hupambana na afya ya mifuko yao, Heri ufe kuliko kudhoofisha mifukoni! Pesa ndio huongoza hatua za binadamu, Bila pesa hufiki popote, Ukitaka kupumua huulizwa una bei gani? Pesa huamua upumue au ufe, Na ikisema kufa utakufa. Watu hawajali vyeti na ujuzi wako, unamjua nani ndio mpango, Humjui mtu, rudi na vyeti vyako panya wakafanye mazalia Ndivyo yalivyo maisha, Kila jambo limeshapigiwa mstari, Ukibishana nalo unagonga ngumi ukutani lazima utachubuka. Wanasema sisi watakatifu Hatuna chembe ya ukabila Bado hamjatembea, Kuna watu maarufu wa kubebana. Eti hizo ni konekisheni, haina haja uzoefu wako, Umesoma wapi na lini utaambiwa kajiajiri Wanatangaza watu wajiajiri Wao wameajiriwa Wanabadilisha VAT hawana karaha Kama zetu Basi wanazidi kuhubiri jiajirini! Wengine hawana vyeo, Wala ukiranja Ila matendo ya kinyama yamewatawala, Hao huparamia vichanga na kuvibaka Maagizo ya waganga wa jadi kuwa watatajirika Wengine hawalali hupita huku na kule kuvizia mikoba ya Wanawake Kila mtu huwaza mkono unaendaje kinywani! Wengine hukata tamaa na kukatisha maisha yao, Wanaona haiwezekani, Bora nife nikapumzike Wengine wamejenga mahekalu Sasa tuwaibie watu sadaka, Mambo ni mengi! Wanaookota makopo, Wanaouza miili Watu hawajali Wakati ukipambana umshinde adui umasikini, Mwanga anakuwangia, Raha yake uendelee kujitundika viraka mwilini, Yupo radhi asilale Usiku kucha aje akatike viuno katika chumba chako ukiamka umetenguliwa mgongo. Wengine huweka kando jitihada zao Mume na mke vitani Wapendanao huuana Mara tunasikia mke ameuawa na mumewe Hapo madhila yanawaangukia watoto Baba jela mama kaburini Watoto mtaani! Binadamu hatupendani Yupo radhi kumtesa mtoto wa mwenzake eti hakumzaa Atamchubua kwa bakora Na kumchoma Moto bila faida ni chuki Utu! Utu! Utu! hakuna utu! Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |