MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MISEMO YA VYOMBO VYA USAFIRI (2)

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MISEMO YA VYOMBO VYA USAFIRI (2)
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Misemo yenye Ujumbe kuhusu Maisha kwa Ujumla
 
      1. “Ajali sio kugongwa na gari tu, hata kukosea kuoa au kuolewa pia ni ajali”
 Maana:
·    Kuoa au
kuolewa ni jambo linalopaswa kufanywa kwa umakini sana.
·    Ndoa njema
ni kiini cha furaha na mafanikio; ndoa mbaya ni kiini cha faraka na maangamio
ya kimaisha.
·   Waoaji au
waolewa wanapaswa kuzingatia vigezo vya msingi katika kutafuta wenza wa kuishi
nao.
·   Mwenza akiwa
mkorofi ndani ya ndoa, maisha kwa ujumla huwa magumu na machungu.
       2.  “Asili haipotei”
 Maana:
·    Mambo ambayo mtu aliwahi kuyafanya katika maisha
yake ya awali hayawezi kubadilika yote hata kama atabadilisha mfumo au mtindo
wa maisha au utamaduni.
·   Mtu hawezi kusahau kwao.
·   Hata mtu awe katika maeneo ya mbali na kwao bado
vitu vya asili yake vitaendelea kubakia katika kumbukumbu zake; hivyo
atavitamani avipate.
        3.  “Bora uzima”
  Maana:
·   Vitu vyote ukose (kiuchumi, kielimu au kijamii)
lakini uzima (na uhai) uwepo.
·   Mtu hata akiwa na ulemavu wa namna yoyote, bado
sio tatizo ili mradi yuko hai.
·    Mengine yote ni ziada, kilicho muhimu ni uhai.
        4.  “Born to suffer”
  Maana:
·  Duniani ni sehemu ya kuchakarika, siyo kulegea.
·  Maisha ni kazi
·  Kiumbe yeyote anayeishi hapaswi kutetereka hata
kidogo.
·   (Mwandishi) Amezoea matatizo, shughuli ngumu,
shida na madhila mengine ya hali ngumu ya maisha.
·   (Mwandishi) hatishwi na lolote linaloambatana na
harakati za maisha.
       5.  “Chanda chema….?
  Maana:
·   Mtu anayetenda mema hutuzwa.
·   Ni vema tutende mema ili tuhifadhiwe au majina
yetu yatajwe vema hata baada ya kuondoka duniani.
·   Mambo mema huhifadhiwa vizuri na kwa fahari.
        6.  “Bora uzee kuliko uzembe”
  Maana:
·    Ni afadhali Mzee (ambaye mara nyingi nguvu huwa
zimemwishia) hufanya mambo yake taratibu na kwa umakini mkubwa, lakini
hufanikiwa au hufika mwisho; kuliko mtu mzembe ambaye huacha au husita kufanya
jambo kwa makusudi na mwisho haambulii chochote au hupata madhara.
·    Uvivu hauna faida katika maisha.
·    Vema kujitahidi katika jambo fulani lenye
mafanikio kuliko kuliacha kabisa.
       7.  “Hakuna tuzo ya ngono zaidi ya UKIMWI”
  Maana:
·    Uzinzi na Uasherati una hasara kubwa kwa mtu na
jamii; hasara kubwa ni kwa mhusika kupata maradhi kama vile UKIMWI.
       8. “Butua uwakomboe wenzako”
  Maana:
·   Tujenge tabia ya kuwasaidia wenzetu.
·   Fanya lolote uwezalo ili kuwasaidia walio chini yako.
·   Kumbuka kutumia kile ulichoruzukiwa na Mola kwa
kuwasaidia masikini.
       9. “Hata bibi alikuwa binti”
   Maana:
·   Maisha ni mapito yanayomtokea binadamu hatua kwa
hatua, hivyo, kuwa makini na kila hatua ya maisha.
·    Uhai, umri au utajiri huwa havidumu milele, bali
huisha au hubadilika baada ya muda.
·    Fanya ufanyalo lakini jua kuna kesho.
·    Kila jambo lina wakati wake.
      10.  “Bosi hanuniwi”
Maana:
·   Bosi (kiongozi) hata akikosea kwa waajiriwa wake
hawezi kuchukiwa, kwani yeye ndiye aliyeshinda maisha yao kiuchumi.
·     Mwenye mali au pesa anaweza kufanya chochote kwa
asiye nazo.
·    Katika kutafuta maisha tunaaswa kupambana na
changamoto mbalimbali zinazojitokeza.
      11.  “Bora lawama kuliko hasara”
Maana:
·    Ni bora mtu kumweleza ukweli wa jambo hata kama
hapendi, kuliko kukaa kimya na baadaye kitu kibaya kikatokea kutokana na huo
ukimya.
·    Hasara ni adui wa maendeleo.
·    Ni bora ulaumiwe kuliko kuingia matatizoni.
·    Kabla ya kukubali kufanya jambo au kitu
chochote, ni vema kuangalia na kupima matokeo yake.
.   Mtu anapaswa kuchukua uamuzi unaoleta madhara
madogo kuliko ule unaoleta madhara makubwa.
Chanzo:
Ponera, A. S na Kikula, I.S,  (2017) Misemo
ya Vyombo vya Usafiri. UDOM. Afroplus Industries, Ltd.