MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - VIPENGELE VYA ELIMU MITINDO

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: VIPENGELE VYA ELIMU MITINDO
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Leo tutazungumzia vipengele viwili:
Mchomozo
na
Ukengeushi
Katika Maisha ya kawaida
  • Watu wanaoanza kupendana. Kuchumbiana.
  • Hufanya nini ili kila mmoja kumpendezesha mwingine?
  • Mavazi
  • Mikogo
  • Mazungumzo: utumiaji wa lugha ISIYO YA KAWAIDA ili kumvutia mwenzako
  • Maisha ya kawaida Vyumbani/ Vijijini/ nk
Mchomozo ni nini?
[Image: Picture1-224x300.jpg]
  • Ni kitu gani cha kawaida, hapa kimefanywa si cha Kawaida?
  • Kwanini si cha kawaida?
  • Jambo la kawaida, linafanywa KUONEKANA kuwa SI LA KAWAIDA.
  • Sote tunajua GOOGLE
  • Nini tunachokiona hapa? Na kina athari ipi?
Kawaida kufanya si Kawaida
[Image: Picture2-300x223.jpg]
  • Vijijini ni kawaida kuona watu wenye makaptula yaliyochanika
  • Siku hizi Vyuoni ni kawaida wanafunzi kutafiti kwa kutumia Google
  • Lakini hapa ni nini si cha kawaida? Kutoka katika Ukawaida huo?
Chanzo – Wanaurasimi wa Kirusi
  • Wanaurasimi/ Usanifu wa Kirusi walishikilia kuwa sababu kuu ya kuwapo kwa sanaa na fasihi ni ili kuyafanya mambo ya kawaida yaonekane kuwa si ya kawaida.
  • Katika huu usokawaida, kipengele fulani hujichomoza kutoka katika ile kawaida iliyozoeleka. Kipengele cha lugha au cha kisanaa katika fasihi.
  • Tuangalie Usanii Huu. Making strange
MCHOMOZO – foregrounding…/2
  • Mchomozo ni ujitokezaji wa vipengele vya KIISIMU katika muktadha mahsusi wa KIFASIHI kwa wingi, uchache au kutokutokea kabisa kulingana na kaida ilivyo.
  • Mbinu za Kiisimu katika Fasihi ambazo kutokana na zilivyowekwa, humfanya msomaji kuvutwa kutoka katika kuangalia jambo LINALOSEMWA, kuangalia LINASEMWAJE
Mbinu za Kiisimu
  • SAUTI – Kushusha au Kupandisha. Au Kimya!
    • Kicheko, Kilio, Ukelele (Mf. Katika Mashetani)
  • MANENO – Kuweka neno fulani ambapo halikutarajiwa. {Shetani anamwambia Binadamu amuue – Mashetani}
  • Hebu sikiliza na angalia mtu huyu anavyotoa salamu. Maneno anayoyaongea ni ya kawaida.
  • Kwa nini tunasikia/ kuona usokawaida?
  • HAMJAMBO?
Mifano zaidi ya Mchomozo………..

[*]Sikiliza maongezi ya Pazi na Tendegu ktk TENDEHOGO. Uk 1 – 3.
[*]Dhana ya Ubora Vs Udhaifu Maana ya Umoja ni Nguvu imesemwa kwa namna gani? Imesemwa kwa mfano wa Ubora Vs. Udhaifu
[*]Angalia mchomozo wa kikejeli katika “Cha Mnyonge” uk 89.

[*]
[*]Katika FASIHI
  • Katika Fasihi, ili tuone mchomozo, hatuna budi kuangalia matokeo yake.
  • Mchomozo unaweza kujitokeza kwa namna mbili: Ukengeufu na Usambamba.
  • Katika UKENGEUFU/UKENGEUSHI Kuna vijitawi vingine.
    • Katika Tamthilia: Ukengeushi
    • Katika Ushairi: Ukiushi
[*][*]MATOKEO YA MCHOMOZO
[*]

[*]Ukengeufu/ Ukengeushi – alienation

[*]Hasa katika tamthilia. Kuifanya hadhira ijitenge na dhana ya mchezo irudi katika uhalisia wa maisha.
[*]“Hodi” ktk Heshima yangu.
[*]Sauti ya Kichaa, Kichaa ktk Pambo

[*]Ukiufu/Ukiushi – deviation
[*]Mabadiliko katika mpangilio wa lugha ili kukiuka ukawaida. Ukiushi huu hufanywa sana na Washairi au Waandishi.

[*][*][*]Ukengeushi
  • KUMBUKA TUNAZUNGUMZIA MATOKEO
    • Ni athari inayotokea wakati hadhira inaporudishwa katika uhalisi wa maisha kutoka katika hisia za kimchezo/ kifasihi.
    • Kila wakati tunakumbushwa kuwa kuna hali halisi ambayo inaigizwa katika jukwaa (au inahadithiwa katika riwaya).
  • Tazama KULI 132 mazungumzo baina ya Rashidi na Amina.
  • Unapozama ktk hisia kuna ukengeushi unatokea na kukurudisha ktk hali halisi.
  • Wimbo ktk Hadithi ya Cha Mnyonge utakitapika hadharani, ni aina ya ukengeushi.
  • UKIUSHI
  • Katika Ushairi hutumia pia taswira. Jazanda ya kawaida ambayo inawekwa kinyume cha mambo.
  • HASA KATIKA USHAIRI na Vichwa cha Tamthilia au Riwaya:
  • Lina Ubani (Kawaida ni Nini)
  • Mvumilivu Hula Mbovu
  • Asali Chungu
  • Sukari yenye sumu n.k
  • Kwesho tutaongelea Usambamba na Ukariri
[*][*][*]
[*]Usambamba
[*][*][*]
[*]Usambamba wa matukio
[*]Usambamba wa sauti, neno, sentensi, wazo
[*]Angalia usambamba katika Kusadikika 1 na 2.