MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'BAGHAMI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'BAGHAMI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAGHAMI'

Neno *baghami* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: a-/wa-*] yenye maana ya mtu aliyepungukiwa akili.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *baghami* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'baghama* ambalo ni kitenzi cha Kiarabu chenye maana zifuatazo:

1. (Kwa mnyama Paa) amempigia mwanawe kelele kwa sauti nyembamba.

2. (Kwa mnyama Ngamia) ameacha kutoa sauti.

3. (Kwa mazungumzo) hakufafanua na hakubainisha maana yake.

4. (Nomino) koja au mkufu anaouvaa mwanamke.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'baghama بغم* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *baghami* lilichukua maana mpya ya *mtu aliyepungukiwa na akili* na kuacha maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*