MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'BAFTA'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'BAFTA'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAFTA'

Neno *bafta* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya kitambaa cheupe kinachotengenezwa kwa nyuzi za pamba.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bafta* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'baftah*( *soma: baftatun/baftatan/baftatin بفتة )* ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana kitambaa cha hali ya juu kilichotengenezwa kutokana na nyuzi za pamba.

Vitambaa vya *bafta* ni mashuhuri sana nchini India na hutumika kushona suruali na mashati.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'baftatun بفتة* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bafta* halikubadili maana yake katika lugha ya Kiarabu.

*TANBIHI:*
Nomino *bafta* ni neno *lililoarabishwa* kutoka lugha ya Kifaransa likiwa na maana ya nguo iliyoshonwa, nyuzi zilizosokotwa, busati, aina ya nguo iliyotengenezwa kutokana na pamba, kitambaa kinachotokana na sufi.

Nchini Misri *bafta* ni kitambaa cha hali ya juu kilichotengenezwa kutokana na pamba nyeupe.

Nchini Syria *bafta* ni kitambaa kilichotokana na hariri.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*