MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI'

Neno *mahari*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: ya-/ya-]* yenye maana ya mali anayotoa mwanamume na kuwapa wazazi wa mwanamke anayetarajia kumwoa; mali au fedha itolewayo na wazazi wa mwanamume kwa wazazi wa msichana anayetaka kuolewa.

Neno *mahari* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *mahrun/mahran/mahrin مهر* lenye maana kile anachotoa mume kumpa mkewe kwa ajili ya kufunga ndoa kati yao.

Neno lingine la Kiarabu lenye maana ya mahari ni *swadaaqu صداق.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *mahrun مهر* lilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *mahari*  maana yake katika lugha asili - Kiarabu haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*