MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'AKHERA'/'AHERA'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'AKHERA'/'AHERA'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AKHERA'/'AHERA'.

Neno akhera/ahera katika lugha Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino [Ngeli: i-/zi-] maskani ya roho za viumbe zinapokwenda baada ya kifo.

Roho za wanadamu wote zitakuwa ahera (akhera) kusubiri siku ya Kiyama (Kisimamo kwa ajili ya kuhukumiwa).

2. Nomino [Ngeli: i-/i-] kule ambako inaaminika binadamu wataishi baada ya kufufuliwa. 

Nahau: enda ahera (akhera): kufa.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ahera/akhera( soma: aakhiratun/aakhiratan/aakhiratin آخرة)  ni nomino ya Kiarabu  yenye maana zifuatazo:

1. Maskani yatakayobakia milele baada ya kufa; kinyume cha dunia. Imeandikwa katika Qur'aan Tukufu, Sura ya 3 (Surat Aali Imraan, Aya ya 152 kuwa: Minkum man yuriidud Dun-yaa wa minkum man yuriidul aakhirata. منكم من يريد الدنيا ومنكم من يريد الآخرة (Yupo miongoni mwenu anayeipenda Dunia , na yupo miongoni mwenu anayeipenda Akhera ).

2. Mwisho.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  aakhiratun/aakhiratan/aakhiratin آخرة) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno ahera/akhera  halikubadili maana yake katika lugha yake asili - Kiarabu. 

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.