MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - KUBADILI MSIMBO KUNAVYOATHIRI KISWAHILI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: KUBADILI MSIMBO KUNAVYOATHIRI KISWAHILI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Kubadili msimbo ni dhana  inayomaanisha kuingiza maneno ya lugha tofauti pindi mtumiaji wa lugha atumiapo lugha fulani. Ubadilishaji wa msimbo hufanywa na watumiaji wengi wa lugha katika miktadha mbalimbali ya mtumiaji wa lugha. Malengo ya kubadili msimbo  hutofautiana kutoka kwa mtumiaji mmoja wa lugha hadi mwingine.
Ubadilishanaji wa msimbo hutawala katika maeneo mbalimbali kama vile bungeni, kwenye vyombo vya habari katika taasisi za elimu na baadhi ya sehemu za kazi.
Ziko sababu nyingi za kubadili msimbo. Miongoni mwa sababu hizi ni umilisi wa lugha zaidi ya moja dhana ambayo hufanywa na wasomi wanaofikiri kuwa ni kuweka msisitizo katika jambo linaloelezwa .
Dhana hii haiepukiki katika baadhi ya mazingira hasa katika ufundishaji wa lugha  za kigeni kwa kuwa kwa namna moja au nyingine  lazima ufundishaji wa namna hii  uhusishe tafsiri  ya lugha inayofundishwa  na lugha ya mwanafunzi husika.
Zaidi ya mazingira hayo, na katika utabibu, tafsiri na ukalimani si jambo la kuendelezwa kama wengIne wafanyavyo kwa kuwa lina madhara yake  katika lugha.
Kwa baadhi ya watu kubadili msimbo watumiapo Kiswahili limekuwa ni jambo la kawaida mno kwao. Mathalan kwao hao kila baada ya neno moja la Kiswahili linalofuata ni la Kiingereza au kila baada ya sentensi moja inayofuata  ni ya Kiingereza.
Sababu kubwa zinazowafanya watu kubadili msimbo ni  kudhani kuwa wakitumia lugha mbili  tofauti kwa wakati mmoja hasa lugha ya pili ikiwa ni Kiingereza, basi huonekana wasomi mbele ya jamii.
Miongoni mwa madhara ya kubadili msimbo bila sababu za msingi ni pamoja na ujumbe kutowafikia walengwa. Wako baadhi ya watumiaji wa lugha ambao hupenda kubadili msimbo bila ya kuangalia hadhira  husika kama inajua  lugha ya pili au la. Suala hili huifanya hadhira hiyo isielewe  kinachoongelewa na hivyo kushindwa kupata ujumbe unaokusudiwa.
Kubadili msimbo bila sababu za msingi hudunisha lugha. Lugha kuu ya mawasiliano  kwa wakati huo ndiyo inayoathirika. Ikiwa lugha kuu ya mawasiliano ni Kiswahili, basi lugha nyingine inayotumika hukifanya Kiswahili kionekane hakijakamilika kimsamiati na kiistilahi jambo ambalo si kweli.
Utumiaji wa lugha kwa mtindo huu ni chanzo cha matumizi mabaya ya lugha na upotoshaji wa ufasaha wa lugha. Pai hupotosha wanaojifunza  lugha mathalan   wageni na watoto wakadhani kuwa Kiswahili kipo katika hali hiyo ya mseto.
Mara zote mtumiaji wa lugha anapaswa kuwa makini  atumiapo  lugha ili kuhakikisha  kwamba anaitendea haki lugha. Kuchanganya maneno ya lugha zaidi ya moja kwa wakati mmoja bila sababu ya msingi siyo jambo zuri, tena ni fujo zinazosababisha adha masikioni.
Wakati wa vikao  vya Bunge, tabia hii imekuwa ni ya kawaida kabisa  kwa baadhi ya wabunge  wetu. Aghalabu hubadili msimbo bila kujali kuwa Watanzania  wengi  wanakielewa zaidi Kiswahili kuliko Kiingereza.
Watumiaji wa Kiswahili, tuache mazoea ya kuchanganya lugha bila sababu za msingi. Mazoea hayo mabaya hutufanya tuonekane hatujui Kiswahili wala Kiingereza. Kiswahili kinajitosheleza  kimsamiati na kiistilahi hivyo kinaweza kutumika chenyewe bila kuchanganya na lugha nyingine.