MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - UKWELI na KWELI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: UKWELI na KWELI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
UKWELI na KWELI

Kama alivyoeleza Sheikh Khamisi Mataka, kwa upande mmoja kuna tafauti baina ya maneno "ukweli" (kwamba ni nomino/ jina: Huu ni ukweli) na "kweli" (kwamba ni kielezi: Ni kweli leo ni Ijumaa?).  Lakini kwa upande mwengine, na kwa maeneo mengine kuzungumzwako Kiswahili, neno "kweli" ni kielezi na ni nomino/jina pia. Kwa mfano, tuna misemo kama vile, "Kweli ikidhihiri, uongo hujitenga"; "Msema kweli ni mpenzi wa Mngu"; na mengineyo.

Mfano mwengine twauona kwenye tafsiri ya Qur'ani, Aya ya 81 ya Sura Israa (Banuw Israiyl). Sheikh Abdullah Farsy katika Kurani Tukufu amelifasiri neno la Kiarabu alhaqq (الحق) kuwa ni "ukweli"; na Sheikh Ali Muhsin Barwaniy katika tafsiri yake ya Al-Muntakhab  amelifasiri "kweli."?

Naye mshairi Shaaban Robert katika mashairi yake amelitumia neno "kweli" kuwa ni nomino/jina.?
Nami pia nimelitumia hivyo.?

Kwa hivyo, kwa ufupi, mtu ana hiari ya kutumia "ukweli" au "kweli" kuwa ni nomino/jina, na atakuwa hakukipotoa Kiswahili.
-Abdilatif Abdalla,
London,
22.10.2021