MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” SEHEMU YA 01

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” SEHEMU YA 01
#1
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” SEHEMU 01
MTUNZI : HAKIKA JONATHAN
Nikiwa sijitambui nilishituka usingizini na kuanza kupiga kelele kuomba msaada, sikuamini nilichokiona kwani mwili wangu ulijaa vidonda kila sehemu ya mwili wangu. Maumivu makali yaliutesa mwili wangu na kunikosesha furaha nafsini mwangu.
Sehemu zote za mwili wangu zenye vidonda zilifungwa kwa bandeji na kunifanya nizidi kuwa na hofu ,kwani sikujua chanzo chochote cha majeraha yale .Nilijalibu kuangaza kila kona ya chumba kile ili niweze kupata msaada, lakini niliambulia halufu kali ya dawa iliyopenya vilivyo puani mwangu na kunifanya nipige chafya mfululizo.
Chembechembe nyekundu za damu zilitoka mdomoni mwangu na kuchafua shuka jeupe nililokuwa nimejifunika, kutokana na chafya yangu isiyokuwa ya kawaida kwa mtu mwenye afya njema. Nilianza kulia kama mtoto mdogo aliyenyimwa ziwa na mama yake, baada ya kugundua sitoweza kutembea tena kwani miguu yangu ilikua imekatwa.
Nikiwa na huzuni niliyashika magoti yangu yaliyofungwa na bandeji, ghafla maumivu makali yaliongezeka mwilini mwangu kwani nilitonesha vidonda ambavyo vilikuwa bado vibichi na kujikuta nikianza kutokwa na machozi kama mtoto mdogo.
“Mungu wangu!! ” ,ilisikika sauti ya mshangao kutoka kwa msichana mrembo aliyevalia mashati meupe, bila shaka alikuwa ni nesi wa hospitali ile. Alitembea halaka sana kuelekea kitandani kwangu ili aweze kunipatia msaada.
“Pole sana kaka yangu, nakuomba upunguze jazba kwasababu unatonesha vidonda vyako na kujiongezea maumivu. “Alizungumza nesi yule kwa sauti ya upole iliyojaa huluma huku akiandaa sindano ya usingizi ili anichome nipate kulala.
“Asante sana dada yangu, lakini nimefikaje hapa? Nimepatwa na nini?,Hii ni hospitali gani?, na kwanini mmenikata miguu yangu?
Niliuliza maswali mengi mfululizo huku nikiwa na simanzi kubwa kupoteza miguu yangu, na kupoteza kumbukumbu yangu kichwani.Sikuweza kutambua chochote kwa wakati ule hata jina langu sikuweza kulitambua.
“Ulifikishwa hapa juzi ukiwa umepoteza fahamu, mwili wako ulijaa vidonda kila sehemu huku miguu yako ikiwa imesagika yote miwili. Kutokana na taarifa tuliyopewa ulikuwa umepata ajari ya gari. “
Msichana yule alinipatia majibu ya maswali yangu na kunifanya nizidi kupatwa na mshangao, “Nani alinifikisha hapa?, niliweza kuuliza swali lingine ili kupunguza maswali mengi yasiyo na majibu yaliyoko kichwani mwangu.
“Msichana aliyekugonga na gari kwa bahati mbaya, ndiye aliyekufikisha katika hospitali hii ya taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa MOI. Binti huyu alijitambulisha kwa jina la Jesca Jonathan, na kutokana na ripoti ya daktari miguu yako ilitakiwa kukatwa halaka sana ili kuokoa maisha yako.
Yalikuwa maelezo marefu sana kutoka kwa nesi huku machozi yakimtoka, kutokana na huluma iliyomjaa hasa akinitazama na hali mbaya niliyokuwa nayo.
*******
Nesi alinichoma sindano ya usingizi na kujikuta nikilala usingizi mzito ulionipelekea kusahau maumivu niliyoyapata kwa wakati ule. Nilikuja kuzinduka siku inayofuata na kushangazwa na kile nilichokuwa nakiona mbele yangu.
Msichana mrembo aliyekuwa chanzo cha maisha yangu kuharibika, alikuwa amesimama pembeni ya kitanda changu akiwa pamoja na nesi aliyekuwa akinihudumia. Hasira na chuki vilinitawala dhidi ya msichana yule na kujikuta nikitamani kumtoa roho yake kama ingiwezekana,kwani sikuona thamani ya yeye kuwepo hapa duniani.
“Kaka huyu ndiye dada aliyekugonga na gari kwa bahati mbaya na kukufikisha hapa hospitalini kwa matibabu”, nesi alizungumza maneno makali yaliyopenya maskioni mwangu na kuuchoma moyo wangu mithili ya mtu akanyagapo kaa la moto bila kutambua.
“Pole sana Robert, nafahamu kuwa unaumia sana kwa matatizo haya niliyokusababishia. Lakini haikuwa makusudio yangu kukusababishia ulema huu bali ni ajari tu ambayo ilitokea kwa bahati mbaya “,. msichana mrembo na mtoto wa kitajiri Rose alizungumza maneno ya kuniomba msamaha huku nesi akipigwa na butwaa kwani hakufahamu chochote kuhusu kufahamiana kwetu mimi na msichana yule.
Mimi kwa wakati ule nilizidi kulia kwa uchungu kwani niliamini Rose kanigonga na gari kwa makusudi, kwani nilikua kikwazo kikubwa katika mapenzi yake na mtoto wa raisi. “Nisamehe Robert, nisamehe Robert!…niko tayali kuwa na wewe. Nimeamini unanipenda kwa dhati Robert “,..Rose alizungumza maneno hayo huku akilia mithili ya mtu aliapo msibani, mala baada ya kufiwa na mtu tegemezi katika maisha yake.
“Siwezi kukusamehe mnafki kama wewe,pia baba yako mzee Jastini kapoteza maisha ya wazazi wangu  na kila niliyemtegemea ili tu nisiweze kuwa karibu na wewe na niache kukufuatilia ” ,niliropoka maneno kwa jazba na sauti kubwa iliyomfanya kila mgonjwa aliyekuwa wodini amelala kukurupuka na kutazama kilichokuwa kikitokea kwa wakati ule.
Nesi ilibidi asimamishe mazungumzo yetu,kwani yalikuwa kero kubwa kwa wagonjwa na wahudumu wa hospitali ile ya taifa ya Muhimbili. “Sa, sa.. ma… hani Rose na…na.. omba mpunguze kelele kwani mnawakera wagonjwa wengne ” ,.Nesi alizungumza kwa kusitasita kutokana na woga aliokuwa nao mala baada ya kumtambua Jesca Jonathan jina lake halisi ni Rose, mtoto wa mfanyabiashara maarufu na katili nchini Tanzania. Umaarufu pia wa familia ya mzee Jastini uliongezeka pale Rose alipotakiwa kuolewa na mtoto wa Raisi aliyeitwa Jacob.
Ilibidi tukae kimya kwani wote tulikuwa tukilia kwa wakati ule,nilifuta machozi huku nikishika magoti yangu na kusononeka kukosa miguu yangu iliyo kwisha katwa. Rose aliigundua huzuni yangu ilibidi anisogelee na kunikumbatia ili kunifariji na kunitia moyo, kitendo nilichokiona kama unafki kwangu.
Ujumbe
“Ukiwa nacho usimtese asiyenacho, kwani dunia huzunguka ipo siku asiyekuwa nacho atapata tu ”
Simulizi; MAPIGO YA MOYO
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)