MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : MAPIGO YA MOYO ***SEHEMU YA 02****

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI : MAPIGO YA MOYO ***SEHEMU YA 02****
#1
SIMULIZI : MAPIGO YA MOYO
***SEHEMU YA 02****
 
Rose alizidi kunibembeleza na kunitia moyo katika siku zote nilizokuwa nikipatiwa matibabu mpaka majeraha yangu yalipopona kabisa.”Kesho mgonjwa wako tutampatia ruhusa kwani afya yake imerudi katika hali ya kawaida “,dokta alimpatia ujumbe Rose kuhusu afya yangu na kutufanya tuwe na furaha sana kwa wakati ule. “,Asante sana dokta kwa kumuhudumia vizuri mgonjwa wangu”Rose alimshukuru dokta na kumpatia bunda la pesa kama shukrani kwa kunihudumia vizuri.
Siku iliyofuata niliweza kupatiwa ruhusa kurudi nyumbani, japo nilikuwa na furaha afya yangu kurudi katika hali ya kawaida lakini sikuweza kujuwa hatima ya maisha yangu. “,Robert mpenzi wangu nakupenda sana, sikujua kama ulikuwa unanipenda kwa dhati kiasi hiki “.Rose alizungumza maneno haya kwa tabasamu na kufanya uzuri wake kuonekana vyema katika mboni ya macho yangu. “Nakupenda pia Rose lakini siko tayali kuwa na wewe, nimeteseka sana kulitafuta penzi lako kwa muda mrefu na kuambulia maumivu…..inatosha siko tayali kuendelea kuumia “,nilizungumza kwa huzuni kubwa huku Rose akinifuta machozi na kunikumbatia.
“Kwa sasa nataka kufunga ndoa na wewe, sitaki tena kuolewa na mtoto wa raisi “,Rose alininyenyua na kuniweka kwenye baiskeli ya walemavu wa miguu aliyoninunulia na kisha kunitamkia maneno mazito yaliyonitia hofu sana. “Baba yako ataniua Rose mimi siko tayali, kawaua ndugu zangu na wazazi wangu ili nisiwe na wewe…. Siko tayali Rose…. Sitaki tena kuumia “,nilimjibu Rose majibu makali huku nikikumbuka vifo vya wazazi wangu walivyouawa kikatili kwa kuungua na moto baada ya banda letu la makuti kuchomwa na majambazi waliokuwa wametumwa na mzee Jastini kuniangamiza mimi na familia yangu. Nilikumbuka jinsi nilivyoshuhudia maiti saba zilizoungua na kuharibika vibaya, maiti mbili zilikuwa za wazazi wangu na zingine za wadogo zangu.Huku mimi nikiponea chupuchupu kwani siku hiyo nililala Morogoro mjini,nilipoenda kutafuta kazi baada ya kumaliza chuo kikuu.
Niliendelea kukumbuka jinsi kijiji chetu cha Mikese walivyohuzunika kutokana na msiba uliyoikumba familia yetu, huku wakinidharau baada ya kugundua kuwa kumtaka Rose binti wa kitajiri kimapenzi ndio chanzo cha vifo vya wazazi wangu. “,Watoto wetu wakisoma hawataki kuoa nyumbani kwao, hawataki kuoa masikini wenzao…. Ona sasa madhara yake ” ,nilikumbuka sauti ya mzee mmoja aliyeropoka maneno hayo msibani wakati tukiaga mwili wa ndugu zangu.
“Rose siwezi kuwa na wewe….. Umeniumiza sana “,nilitamka maneno hayo kwa msisitizo baada ya kukumbuka matukio ya nyuma yaliyotokea na kubadilisha furaha ya maisha yangu, huku chanzo kikiwa mimi kumpenda Rose msichana niliyesoma nae chuo kikuu cha SUA na kushindwa kuheshimu hisia zangu kutokana na umaskini wangu niliokuwa nao.
“Robert kila kitu kiko tayali, kesho inatakiwa mimi na wewe tufunge ndoa uwanja wa taifa….Jacob kaniruhusu nifunge ndoa na wewe badala yake kwani kagundua kuwa unanipenda sana tena kwa dhati “…..Rose alizungumza maneno yaliyonitia moyo na kunifanya nikubaliane naye. “,What….!! unasema kweli?…… niliongea kwa mshangao huku nikifuta machozi yangu na kukaa vizuri kwenye kibeskeli changu ili nimskie vizuri., “Ndio…. Kesho Tanzania nzima wanajua mimi nafunga ndoa na Jacob mtoto wa raisi, kwahyo kesho muda wa harusi utatokea wewe badala yake. “Rose alisisitiza huku akinitaka kukubaliana naye jambo ambalo sikuweza kulipinga tena kwa wakati ule.
Hatimae siku iliwadia, maelfu ya wananchi walifika uwanja wa taifa kushuhudia mtoto wa raisi akifunga ndoa. Wageni mbalimbali kutoka nchi jirani walifika kushuhudia sherehe hiyo, “Watakapo ita bwana harusi, tutaenda wote kwa pamoja lakini wewe utakua kama msindikizaji wangu ili wasigundue chochote “,Jacob alinipa maelekezo huku mimi nikimshangaa tu kwani ilikua mala ya kwanza kukutana naye dhaidi ya kupata taarifa zake kutoka kwa Rose.
“Ndugu wananchi tunaomba mpige kelele za shangwe bwana harusi anapoingia uwanjani “,MC alizungumza huku shangwe zikifuatia huku Jacob akisukuma kibaiskeli changu cha magurudumu matatu tukielekea uwanjani alipoketi bibi harusi. Shangwe na nderemo zilipungua kadri tulivyokuwa tukikalibia uwanja kwani walishangazwa na muonekano wetu .
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)