MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” *SEHEMU YA 4*

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” *SEHEMU YA 4*
#1
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ”
*SEHEMU YA 4*
 
Raisi akiwa ikulu, hakuweza kulala kabisa!, alitembea huku, mala akaenda kule, alilala akakosa usingizi, hakuwa na jinsi zaidi ya kuamka na kwenda kuketi sebuleni. “Lakini, hapa kuna kitu, nahisi mzee Jastin atakua anasiri nzito kaificha, kwanini alionekana kuwa na wasiwasi sana alipomuona Robert?, kwanini alitoweka bila hata kuaga baada ya mauaji ya mwanangu na mpaka sasa hajanipigia simu? “,raisi wa Tanzania, raisi aliyekuwa kipenzi cha watu kutokana na uongozi wake kuwa wa haki na kuleta maendeleo mazuri kwa wananchi, akiwa ameketi sebuleni aliendelea kujiuliza maswali mengi kichwani bila kupata jibu.
“Kesho nitamtembelea tena Robert hospitalini, lazima atakuwa anafahamu chochote “,raisi aliinuka na kisha kuelekea chumbani kwake huku akiongea peke yake mithili ya kichaa na kuamua kunitembelea hospitalini siku iliyofuata.
9:00 asubuhi.
Ilikua siku ya jumanne, siwezi kuisahau siku hiyo kwani ni moja ya siku ambazo niliweza kuamini kuwa mwenye pesa si mwenzako! ,japokuwa niliapa sitoweza kuzungumza chochote kuhusu kifo cha Jacob, nilijikuta nikizungumza kila kitu bila kuacha hata nukta !
” Nimefanya nini sasa, Rose atanifikiliaje?  ,si alinikataza nisiseme chochote kwani baba yake ataweza kuwa hatarini? “,nilikuwa nikijilaumu huku nikijuta kumwambia ukweli raisi, baada ya kunitembelea muda mfupi uliopita.Nilijiona mwenye makosa japokuwa mzee Jastini alikuwa amenitendea mambo mengi mabaya sana ambayo hakuna binadamu yoyote angeweza kumsamehe kama angeweza kutendewa.
*******
Ilikuwa ni asubuhi mida ya saa mbili siku ya jumanne, nikiwa nimeketi kitandani nilishangaa kuona madaktari wakikimbia huku na kule ndani ya wodi niliyokuwa nimelazwa.
“Mmmh hapa kuna jambo sio bure “,nilizungumza peke yangu huku nikiwashangaa madaktari ambao walionekana kuzunguka ndani ya wodi kukagua hali za wagonjwa huku manesi wakifanya usafi na wengine kubadili mashuka ya wagonjwa yaliyokuwa machafu, na kutandika mashuka masafi.
“Samahani wewe ndiye Robert!,”nilijikuta nikiulizwa swali na nesi ambaye sikuwahi kumuona tangu jumamosi nilipopigwa risasi na kufikishwa katika hospitali  ya Muhimbili, hospitali ambayo ilikua mala yangu ya pili kupatiwa matibabu huku nikiwa nasumbuliwa na matatizo yanayotaka kufanana.
“Ndiye mimi “,nilimjibu nesi, na kuanza kumshangaa sana kwani aliniomba nimpishe kitandani mala moja. Bila shaka!,nilitii ombi lake na haraka sana nilimuona akitandika kitanda changu kwa shuka jeupe, na kutoa shuka ambalo nilililalia kwa siku tatu mfululizo huku likiwa na mabaka mabaka ya damu kutokana na jeraha la risasi nililokuwa nalo.
Baada ya nesi yule kumaliza kutandika, aliweza kuondoka na kisha niliweza kurudi kitandani kujilaza huku nikiwaza kuhusu hatima ya mapenzi yangu ya mateso, na kujuta kumpenda Rose kwani majanga hayakuisha hata siku moja katika maisha yangu.
“Kijana hujambo ……!,unaendeleaje?  lilikuwa ni swali kutoka kwa raisi, raisi ambaye alifika wodini bila mimi kutambua kwani nilikuwa na mawazo mengi kwa wakati ule, nikiwaza kuhusu hatima ya maisha yangu yenye vitimbwi kila kukicha.
Haraka nilikurupuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo, na kisha kumsikiliza raisi alichokuwa akikizungumza huku nikipata jibu la swali ambalo nilijiuliza kuhusu pilika pilika za madaktari na manesi walizokuwa nazo asubuhi ile.
“Naendelea vizuri mheshimiwa “,nilimjibu raisi huku nikijilazimisha kuficha huzuni na mawazo mengi niliyokuwa nayo.
“Sasa nataka unisaidie kitu, pesa hii hapa, niambie kuna nini wewe na mzee Jastini mbona alitaka kukuua “,raisi aliongea kwa kunitega ili aweze kujiaminisha kama kweli kitu alichokiwaza kilikua sahihi.
Kutokana na pesa nyingi nilizokuwa nimeoneshwa, pesa ambazo zilikuwa ndani ya briefcase jeusi, sikuwa na jinsi ilibidi nitiririke kila kitu. Kwani njaa nayo ilikuwa ikinisumbua, sikuwa na kazi zaidi ya kumtegemea Rose ambaye alikuwa kama tegemezi langu lililobakia.
“Nilimpenda Rose tangu chuoni lakin alinikataa kwa sababu nilikua masikini, kama mwanaume mwenye mapenzi ya dhati sikukata tamaa, niliendelea kumfuatilia Rose hata baada ya kumaliza chuo, lakini Rose hakuwa tayali kunipenda hivyo basi aliamua kumwambia baba yake kuwa nilikua nikimfuatilia. Baba yake alinipatia onyo lakini sikujali, nilijikuta nikiendelea kumfuatilia Rose kitendo kilichopelekea wazazi wangu kuuawa na mzee Jastini “,niliamua kuishia hapo kwani nilisita kutamka jambo baya ambalo niliweza kufanyiwa na Rose, kuhusu kugongwa na gari na kisha kuvunjika miguu kwani sikujua kuwa alinigonga kwa makusudi au laa!
Baada ya kumalizia kumwelezea raisi kuhusu siri hii, aliamua kuondoka haraka na kisha kuniachia mawazo mengi sana kichwani huku nikijilaumu na kujuta kusema ukweli kwani Rose angeweza kunichukia na kisha kuniacha kwani nimemuweka baba yake mahali pabaya, lazima ataweza kukamatwa na kushtakiwa kuhusika na mauaji ya Jacob, mtoto wa Raisi.
Je raisi atatoa maamuzi gani kuhusu mzee Jastini! Vipi kuhusu Rose ataendelea kumpenda Robert!
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)