MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” **SEHEMU YA 05*

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” **SEHEMU YA 05*
#1
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ”
**SEHEMU YA 05*
Rodgers akiwa anaonekana kukosa amani kabisa kuliko siku zote ,alishindwa kula hata chakula kwani alipojalibu kula hamu ilikata ghafla hasa baada ya kukumbuka kosa ambalo ameweza kulifanya kwa bahati mbaya. “Shit! mission failed ………!”,sijawahi kushindwa! lakini katika swala hili, nikizubaa lazima serikali itafanikiwa kunikamata.”,ilikuwa ni sauti ya hasira kutoka kwa Rodgers, jasusi wa kimataifa ambaye aliongea huku akitupa simu yake chini na kuipasua ,kwani alikuwa na hasira iliyopitiliza kiasi kwamba angeweza kuua mtu yeyote kama angekuwa karibu naye.
“Vipi Rodgers kulikoni!, nimesikia sauti ya kitu kudondoka chini, una tatizo gani “,mzee Jastin alifika haraka sana sehemu ambayo ilikuwa imejaa zana mbalimbali za kufanyia mazoezi, bila shaka ukiingia tu lazima utatambua chumba kile kilikuwa ni cha kufanyia mazoezi, tena mazoezi ya karate na wala sio mbio za mita mia moja. Mzee Jastin alishangaa kumkuta Rodgers akiwa ana mawazo mengi, huku simu yake ikiwa imepasuka vipande! vipande! na kuamua kumuulza tatizo ambalo lilikuwa likimsumbua.
“Bosi!, siku ambayo nafanya mauaji, nilishika siraha bila kuvaa gloves, bila shaka wataalamu wa kompyuta wanaweza kufahamu muuaji wa Jacob, kwasababu finger prints lazima zitaonekana tu! “,ilibidi Rodgers, jasusi wa kuaminika na mzee Jastin amweleze bosi wake ukweli. Taarifa ambayo ilimshtua sana mzee Jastin, kwani alitambua kuwa muda wowote lazima muuaji angeweza kutambulika!
“Big mistake! Lakini kulaumiana hakutasaidia chochote, inatakiwa haraka sana nikukatie tiketi ya ndege ukapunge upepo Mombasa, “mzee Jastin, mfanyabiashara maarufu na katili nchini Tanzania alizungumza huku akitafuta namba ya rafiki yake ambaye alikuwa akifanya kazi katika shirika la ndege la Air Tanzania.
“Tiketi imebaki moja ya leo usiku!, japokuwa watu wengi wanaitaka lakini mimi nakuuzia wewe rafiki yangu ………japokuwa uliniambia abiria wako ameahirisha safari “,ilikuwa ni sauti ya mtu aliyeonekana kuongea kwa upole sana, na ustaarabu wa hali ya juu moja ya sifa ambazo zilizingatiwa kwa wafanyakazi wa mashirika ya usafiri wa anga. Sifa zao za ukarimu hazikuachana mbali na wafanyakazi wa benki pamoja na kampuni mbalimbali za simu Sauti hiyo ilitoka kwa Juma, rafiki kipenzi wa mzee Jastin baada ya kupigiwa na rafiki yake aliyekuwa anahitaji tiketi ya ndege kuelekea Mombasa.
“Sasa hivi ni saa kumi jioni, ndege inaondoka saa mbili usiku jiandae! Kuanzia kesho jumatano maisha yako yatakuwa katika ngome yetu ya Mombasa, nenda kajifiche huko “,mzee Jastin alimpatia maelekezo Rodgers ,mala tu baada ya kukata simu ya Juma. Huku Rodgers akitabasamu na kisha kwenda kufungasha vilago vyake kujiandaa na safari.
*******
“Baba ni muuaji, usijilaumu sana kusema ukweli, aliyokutendea yanatosha, “,Rose aliongea huku akinifuta machozi baada ya kumweleza kila kitu kilichokuwa kimetokea. Jinsi raisi alivyonitembelea na kunipatia pesa nyingi nimweleze chanzo cha ugomvi wake mimi na mzee Jastin..
“Nyamanza mpenzi!, let’s go home ……just usimfikilie kabisa dady, baba gani siku ya nne sasa hajui mwanae anaishije, kazi tu kuvuruga mapenzi ya watu “,Rose alizidi kufoka  huku akinipandisha katika baiskeli yangu ya mataili matatu kwani tayali tulikuwa tumeruhusiwa.,niweze kwenda nyumbani.
Rose alionekana kuwa na hasira sana kwani tangu baba yake alipotoweka siku ya tukio, mpaka natolewa hospitalini tulikuwa hatufahamu sehemu ambayo alikuwa ameelekea, huku Rose akiishi peke yake kwani hakuwa na mama wala wadogo zake, au ndugu yoyote aliyekuwa akiishi naye.
Siku zote Rose hakutambua ni kwanini alikuwa akilazimishwa na baba yake kuolewa na mtoto wa raisi, marehemu Jacob. Lakini siri haikuwa siri tena, aliweza kugundua kila kitu, mpaka biashara haramu ambazo baba yake mzee Jastin alikuwa akizifanya
“Mtoto wako akiolewa na raisi, bila shaka raisi atakuwa ndugu yako  .kupitia wewe tutaingiza madawa mengi ya kulevya nchini Tanzania bila kuguswa na kujiingizia  pesa ndefu sana ” ,ulikuwa ni ujumbe wa barua pepe kutoka Mombasa, ujumbe ambao Rose aliweza kuukuta katika kompyuta ya baba yake alipojaribu neno la siri la kompyuta hiyo mala nyingi bila mafanikio. Alipojaribu tena na tena !,hasa baada ya kuandika jina Rose kwa herufi kubwa, kompyuta ya baba yake  iliweza kufunguka na kumfanya Rose kupigwa na butwaa kwani hakutambua kuwa baba yake alikuwa katili kiasi kile. Aligundua mauaji mengi ambayo baba yake aliweza kuyafanya huku akijishugulisha na biashara haramu za magendo.
*******
Raisi alitabasamu, huku akiwapongeza vijana wake kwa kazi nzito, kazi ya kugundua muuaji kupitia alama za vidole (finger prints) zilizoachwa katika bunduki ambayo muuaji aliitumia kumuua Jacob.
“Hii sura sio ngeni, lazima kuna sehemu tuliweza kukutana “,mheshimiwa raisi akiwa anaitazama sura ya muuaji katika kompyuta, aliongea huku akikuna kidevu chake, bila shaka alikuna kipele kwani hakubarikiwa kuota ndevu hata moja katika maisha yake.
“Mtu huyu akipatikana, lazima tutatambua siri nyingi nyuma ya pazia, haraka sana atafutwe! “, raisi aliongea na kutoa amri kwa vijana wake, huku akiondoka katika jengo la mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA …
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)