MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 10**

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 10**
#1
SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU “
*SEHEMU YA 10**
Mwamutapa;
        kila familia katika nchi ya Mwamutapa, wanaingiwa na hofu kubwa, baada ya kusikia sauti za kutisha kutoka msituni,asubuhi siku ya jumanne. Sauti hizo waliziipuuzia mwanzoni. Lakini, sauti hizo zilisikika tena kwa mala nyingine jioni ya siku hiyo hiyo, na tena sauti hizo zilikua nzito na za kutisha  kupita zile zilizosikika kwa mala ya kwanza. Kelele hizo zilisababisha familia nyingi kujifungia majumbani mwao, huku giza likiwa hata bado halijaingia japokuwa jua lilikuwa tayali limezama kutokana na uoga waliokuwa nao, kwani walifahamu sauti hizo zilitokea katika msitu wa majini bila kutambua chanzo chake, wala maana yoyote kuhusu sauti hizo.
Familia ya kina Ngesha ilikuwa moja ya familia zilizokuwa na hofu sana, kwani mama yake Ngesha alifunga milango yote na kisha kuketi sebuleni, katika nyumba yao ya udongo, na kisha kumsubili mwanae ambaye alikuwa hajarudi tangu alipoondoka asubuhi, na kumuaga mama yake kuwa ameenda kumtembelea rafiki yake Njoshi.
Lakini mama yake Ngesha alipojaribu kumsubili mwanae ili waweze kuelekea shambani pamoja, alishangaa mwanae alipochelewa sana. Kitendo kilichomlazimu mama yake kwenda shambani peke yake, kwani aliamini Ngesha atamkuta shambani,mala tu atakaporudi kutoka kwa rafiki yake.
Ama kweli, nani kama mama ?,kwani mama yake Ngesha alifanya shughuli za shambani mpaka mchana, lakini bila kutegemea, hakuweza kumwona mwanae akimfuata shambani. Hali hii ilimfanya mama yake Ngesha kuwa na hofu sana, na ukizingatia alikuwa tayali ameshazisikia sauti za kutisha asubuhi, mida kama ya saa nne. Hivyo basi, mama yake Ngesha alitambua kuwa siku hiyo ilikua tofauti sana na siku zingine, na haikuwa kawaida mwanae kuchelewa kiasi kile na kushindwa kumfata mama yake shambani, jambo ambalo lisingewezekana kwani Ngesha alipenda sana kumsaidia mama yake kazi za shambani.
Hivyo basi, baada ya mama yake Ngesha kuwaza na kuwazua, aliamua kusitisha shughuli zake za shambani mapema sana, mida kama ya saa sita hivi na kisha kurudi nyumbani, aweze kujua usalama wa mwanae, chezea Mwamutapa wewe!, muda wowote kifo kinaweza kukutokea bila mungu kupenda.
Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza, mama yake Ngesha alifika nyumbani kwake, lakini hakuweza kumkuta mwanae. Haraka sana wazo likamjia na kisha kufunga safari kuelekea nyumbani kwa kina Njoshi. Huko pia alipofika getini tu,komeo la mlango  liliweza kumkalibisha,komeo lililomaanisha hakukuepo na mtu yoyote nyumbani pale.
Asikwambie mtu,mama yake Ngesha alichoka!,alipigwa na butwaa huku maswali mengi yakimsumbua kichwani,kwani hakujua mwanae yuko wapi.Alihisi labda atakuwa hatarini,tena katika hatari kubwa sana.Hatari ya kutekwa na askari wa  mfalme,na kwenda kutumikishwa kazi nzito,kazi ambazo watu wengi walikamatwa na kwenda kuzifanya bila kupumzika ,na bila malipo yoyote.Na pale ambapo mtu yeyote alipojaribu kufumbua kinywa chake,na kudai haki yake,bila huruma kifo ndio zawadi na tuzo pekee aliyolipwa kama malipo ya jasho lake,chezea mfalme wa Mwamutapa wewe!.
Haya sasa,tuachane na hayo.Jua likiwa linaanza kufifia huku ndege wa angani wakiruka ruka angani,na kuipendezesha anga ya Mwamutapa.Mama yake Ngesha anaamua kurudi nyumbani baada ya kusimama kwa dakika kadhaa mbele ya geti la kina Njoshi, huku akiwa haamini kile alichokuwa anakiona.
Ikiwa tayali mida ya jioni, akiwa anarudi Nyumbani,bila kufahamu ilikua ni saa ngapi, alisikia kelele nzito na za kutisha kutoka msituni ,kelele ambazo alizisikia kwa mala ya pili japokuwa kelele hizi zilitisha sana kuliko zile za awali, kwani zilisababisha mpaka ardhi kutetemeka. Lakini bila kupoteza muda, mama yake Ngesha aliamua kutimua mbio kuelekea nyumbani, mbio ambazo zilimfikisha nyumbani baada ya muda mfupi tu, kwani alitimua kama swala. Na mala baada ya kufika nyumbani, jambo la kwanza lilikuwa ni kufunga milango na madirisha ya nyumba yake, na kisha kuketi sebuleni kumsubili mwanae.
Msituni;
     Njoshi akiwa ameshikilia kamba yake kwa mkono wa kushoto, ghafla alishangaa majini wale wakipotea. Aliamua kutoka haraka sana shimoni, huku akiwa amelowa na mwili wake kutoa harufu mbaya, harufu ambayo ilisababishwa na maji machafu ya shimoni, maji ambayo yalichanganyikana na viumbe wengi wakiwa wamekufa na kuoza ndani yake.
“Mmmh wamekimbia?, au wamenitega tena? “,Njoshi aliongea baada ya kutoka ndani ya shimo na kushangaa kutokuta kiumbe yoyote yule, kitendo ambacho kilimtahadharisha aweze kuwa makini, kwani alifikili labda atakuwa amebadilishiwa mtego, aweze kunaswa kirahisi ,jambo ambalo lilimfanya aweze kuwa makini na asiweze kunaswa kwa mala nyingine tena.
“Hapa ngoja nisonge mbele, na giza tayali limeshaingia, inatakiwa nifike katika ngome ya malikia haraka sana, niweze kuiba fimbo ya kifalme na kuiandika jina langu, harafu nikachonge jeneza la ajabu kisha kesho asubuhi na mapema nirudi nyumbani “,Njoshi aliongea huku akianza kutimua mbio na kuelekea katika ngome ya malikia, kwa kutumia njia ile ile iliyokuwa imetegwa shimo na kufunikwa na udongo juu yake. Bila kutambua kuwa tayali kulikuwa na mtego mbele yake, mtego ambao ulikuwa katika ngome ya malikia, ngome ambayo ilihafadhi madini ya kila aina pamoja na vitu mbalimbali ikiwemo fimbo ya kifalme. Fimbo ambayo mtu anayetaka kuongoza Mwamutapa lazima aimiliki, na kuandika jina lake, na hiyo ndio itakua tiketi ya kuongoza nchi ya Mwamutapa.
Njoshi alizidi kusonga mbele huku akipanga mipango ya namna ya kufanikisha kutengeneza jeneza la ajabu haraka sana ili aweze kurudi nyumbani siku ya jumatano asubuhi, siku ambayo ilikuwa ya mwisho kukaa msituni, kwani mfalme alitakiwa azikwe ndani ya siku tatu   baada ya kufa, na kama angezikwa katika jeneza la ajabu nje ya siku hizi tatu, au angezikwa huku wananchi wa Mwamutapa wakiwa wamefahamu kuwa amekufa, mfalme hatoweza kufufuka kwani inatakiwa iwe siri.
Njoshi baada ya kukimbia ndani ya muda mchache tu ,kwa umbali kama wa mita mia moja aliweza kuiona ngome ya malikia, ngome ambayo ilizungushiwa nyasi na kisha kupambwa na maua mazuri sana, maua ambayo yalikuwa na harufu nzuri na kuwavutia ndege wengi pamoja na wadudu kuruka ruka katika ngome hiyo kufuata maua.
“Adui hayuko mbali, muda sio mrefu tutamtia nguvuni, yani atajuta kuingia katika ngome na msitu huu “,Malikia alizidi kuongea kauli za laana, kauli ambazo baadae zitamgharimu kwani ilikua ni mala ya pili akitamka kauli mbaya na za visasi kwa Njoshi
Hii ilikuwa ni kama miiko, kauli ambayo anaitamka malikia lazima aitimize, bila hivyo watu wake wataweza kufa ghafla,na  kisha ngome yake itateketea. Jambo ambalo baadae linaweza kutokea, kwani malikia alishindwa kumwadhimbu Njoshi na kulipiza kisasi ili atimize kile alichokuwa akikisema, na kuepusha balaa kwa watu wake.
“Aiw…eeeh mizimu wa babu zangu, niepu…sheni na bal…aa h…ili “,Njoshi aliomba mizimu iweze kumsaidia kwani bila kutegemea, alishindwa kutoka mahali alipo, wala kujitikisa , baada ya kukanyaga maji ya ajabu, maji ambayo malikia alinyunyizia kuzunguka ngome yake, pale tu Njoshi alipotaka kuingia ndani, katika ngome hatari ya malikia wa majini wa msituni.
“Aiweeh mtukufu Gutamanya, mkuu wa majini wote ulimwenguni, tayali nimemtia mikononi mwangu adui yangu”,malikia wa majini,msichana aliyekuwa mrembo sana,aliongea huku akiwaongoza majini wote kuelekea getini ,kwenda kumtazama adui wao na kumtambua,kwani maji yale yalikuwa na nguvu sana kiasi kwamba Njoshi aliweza kuonekana machoni kwa majini,bila kusaidiwa na  kitambaa alichokivaa kiunoni.
Mwamutapa;
        Ngesha na mama yake Njoshi walishangaa kukuta kila nyumba ikiwa kimya huku milango na madirisha yakiwa yamefungwa baada ya kutoka shambani. Haikuwa kawaida mji kuwa kimya kiasi kile muda wa saa moja jioni, hali hii ilimfanya Ngesha kumuaga mama yake Njoshi na kisha haraka sana akaelekea nyumbani kwao, ili aweze kujua usalama wa mama yake.
Akiwa katika hali ya mshangao, alishangaa mama yake akimkimbilia na kisha kumkumbatia huku akilia, baada ya kufungua mlango na kukuta mama yake akiwa ameketi sebulini akimsubili.
“Uko salama mwanangu, nilikuwa na hofu sana juu yako “,mama yake Ngesha aliongea maneno mazito yenye upendo ndani yake, maneno yaliyomfanya hata Ngesha aweze kutokwa na machozi, kwani alijiona mwenye makosa makubwa kumfanya mama yake awe na hofu juu ya usalama wake, kwani aliondoka tangu asubuhi bila kurudi nyumbani mapema.
Ili kujuwa hatma ya Njoshi msituni, tukutane katika sehemu ya 11
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)