MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 32

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 32
#1
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU 
SEHEMU YA 32
Unajua bana kipindi kile Zamda alivyokuwa amepata mimba Kwakweli kama ni kuchanganyikiwa pale ilizidi ndiyo maana niliamua kufanya maamzi ya Haraka vile.
"Mama Zaidu akasema Hivi" Kwa vile hayakuwa mabaya Basi haina shida. Kwasababu kuna wazazi wengine Weee ni kuanza kupiga tu huyo mwanao.
Ni kweli. Ila kwasasa namshukru sana mungu hadi mda huu na namna tunavyoishi ni Kwasababu ya huyo Zamda na Zaidu wake.
Ndiyo maana wahenga wakasema kabisaaaaaaa kwamba usitukane mamba kabla hujavuka mto.
Ni kweli.
"mama Zamda naye akasema Hivi".Ni kweli kabisaaaaaaa. Kwasababu Yaani huyo Zamda ndiyo tungeamua kumsusa hivyo unafikiri mda huu tungekuwa hapa.
" Baba Zamda akasema Hivi "Lahasha.
" Mama Zaidu naye akawa na la kuongea. Alisema hivi "Unajua huwa tunasema mengi Mungu huyaficha katika uso wako.
" Baba Zamda naye akasema Hivi ".Ni kweli kabisaaaaaaa.
" Mama Zaidu naye akasema Hivi ".Kwasababu, Unajua uso wako na macho yako kama Ndiyo taa zako,Kwakweli kama ni kuona huwa zinaona kulikoni hata hiyo tochi.ila ndiyo hivyo kwamba kuna kitu ambacho milele mungu hawezi kukuonesha kamwe. Hata siku moja hawezi kukuonesha kwamba Kesho panakuje.
" Baba Zamda anasema ".Ni kweli. Hicho ni kitu ambacho kwa mungu amekuepeushia kutuwekea Kabisaaaaaaa.
Kwakweli siku hiyo maongezi Yale yalikuwa ni marefu na mazuri sana yenye Furaha kwelikweli.
Siku nazo zinazidi kwenda kama wasemavyo wahenga kwamba hata siku moja siku hazigandi hata kuwe na baridi ya namna gani.
Ambapo Hapo ni tayari kama nusu mwaka hivi kuisha Tangu Zamda na Zaidu kuoana.
Siku hiyo Zamda na Zaidu wakiwa wamekaa sebuleni Hapo. Glady na mdogo wake wakiwa wanacheza hapo pembeni.kwa mda huo ikiwa ni mishale ya saa mbili usiku wakiwa wanaangalia Runinga Hapo. Zamda akawa anasema Hivi.
Unajua Zaidu mume wangu.
Naaam mke wangu.
Unajua nimekuja kuamini Kweli katika Maisha sijui nisemeje tu katika suala la kusaidiana.
Kwanini?.
Yaani Unajua Mimi hapa siamini kwanza kama Mimi ndiyo naishi Kwenye Nyumba kama hii.
Aaaaa kwanini usiamini Zamda ?
Unajua Zaidu kule Kimbu ni kama nilikuwa nazimu kabisaaaaaaa.
Kivipi Yaani.
Yaani Zaidi kwa maisha niliyokiwa nikiishi yalikuwa sijui kama ni kwenye dunia nyingine Kabisa.
Haya Bana.
Yaaani tena mtu wa kumshukuru kabisaaaaaaa ni Jeni.Jamani Kwakweli Jeni sitomsahau katika Maisha yangu. Niliishi naye Katika kila aina ya maisha.
Sawasawa.Kwa mfano Zamda nikuulize swali rahis tu.
Ndiyo ndiyo uliza.
Aaaaa.mathalani Mimi na wewe tusingekutana ingekuwaje?.
Aaaaaaa kwakweli Zaidu Hilo ni swali lingine Kabisaaaaa.
Kwanini?.
Kwasababu, Kwaujumla nikienda moja kwa moja kwenye Majibu ni kwamba leo hii Mimi nisingekuwa hapa.
Ila ni kweli. Kwasababu hata Mimi bila huyo Jeni sidhani kama ningekuwa hapa.Ni ile tu kama mungu akikupangia.
Okay. Ila Unajua kuna issue nilitaka nianzishe hivi.
Issue gani Hiyo mume wangu?.
Aaaaa nataka nifungue kampuni hivi.
Kampuni?.
Ndiyo maana Yake.
Inahusu nini Hiyo?.
Aaaaa inahusu uchapishaji wa vitabu mbalimbali.
Ahaaaaa.utaiitaje.
Jina Ambalo nimeliandaa ni SAKAS.COM LTD PRINTERS
Hawatasema umeiga?.
Aaaaa hapana kuna maana ya Mimi kuita hivi.
Kwamba ina maana gani ?.
Tumeingia mkataba nao.
Mkataba kivipi?.
Aaaa natumia jina lao Lakini bidhaa ni zangu.siunajua tena Majina kama haya ni Majina makubwa.Kwahiyo ndiyo maana nakwambia nimeingia nao mkataba na kwa ujumla nawalipa.Haya Majina ni Majina makubwa.
Ndiyo.Alafu kweli Hawa jamaa noma wana hadi television yao,redio.
Ndiyo maana Yake.
Ahaaaaa. Kwani hadi leo Unajua kirefu chake Sijui kabisaaaaaaa.
Ahaaaaa. Ni kwamba. Kwanza hili ni kama jina la mtu.Huyo jamaa ni Kijana mdogo mdogo tu ambaye ni mjasiriamali kwelikwel.
Kumbe ni Kijana tu.
Ndiyo maana Yake.Aaaa Kwahiyo kutokana na jina lake namna lilivyo.
Anaitwa nani kwani jina lake la kawaida?.
Anaitwa Saidi Kaita
Ahaaaaaaaa.
Kwahiyo Ndiyo maana huyu jamaa kila kitu atakachoanzisha anaanza na SAKAS.COM kama ni TV anasema SAKAS.COM TV ,kama ni duka anasema SAKAS.COM shop. Pia anayo mini supermarket hapo kati inaitwa SAKAS.COM minisupermarket
Ahaaaaa Kwahiyo likoje.
Ni kwamba ikimaanisha Saidikaitastories.com printers na wale wanajiita saidikaitastories.com television Kwahiyo Ndiyo maana SAKAS.COM zimejaa Sana.
Ni sawa nimekuelewa kwakuweza kulinunua jina Hilo Kwakweli kama ni faida kubwa Sana itakuwepo.
Ndiyo maana Yake.Kwahiyo Mimi nataka nikuweke kuwa kama Manager mkuu.
Aaaaa Kweli kabisaaaaaaa Zaidu?.
Au vibaya !?.
Aaaaa hapana. Siyo vibaya.
Kwanini unashtuka hivi.
Aaaa siamini kama kweli Unataka kunipa cheo cha juu kama hicho.
Aaaa mbona cheo cha kawaida tu hicho.
Daaa Kwakweli siamini kabisaaaaaaa.
Utaamini  pindi utakapoanza kukalia kiti cha kiheshimiwa.
Daaaa labda.
Lakini utakuwa na msaidiizi wako.Kwasababu kazi ya umeneja si ya utani utani Kabisaaaaaaa.
Sawa itakuwa vizuri.
Aaaaaa Unajua mke  Wangu Mimi nataka Kwakweli kama ni kutengeneza Hela nataka tutengeneze Hela kwelikweli.
Sawasawa.
Kwasababu najua tulipotoka huko kwakweli Maisha yetu sijui yalikuwa vipi tu Yaani.Kwahiyo nachokuomba ni kuwa makini kweli kweli kazini.
Sawasawa.
Kwasababu Unajua hawa watoto wetu nataka wasome vizuri Yaani katika shule nzuri zenye kufaulisha vzuri.
Sawasawa.
Siyo kama shule ambazo sisi tumesoma za kichangani kweli kweli. Yaani jua likiwaka tu hapafai hapo ardhini.
Sawasawa mume wangu.
Mimi Natumai watoto wanne watatutosha kabisaaaaaaa.Hawa wawili na Mimi pia nahitaji wawili. Watakuwa ni madume wote.
Itapendenza kwelikweli.
Kwa Mimi Kesho kutwa tu namaliza haya Mambo ya kusoma. Kwasababu kwa huko chuo haina shida nitajua namna ya Mimi kusoma Wakati nikiwa naendelea na harakati nyingine hapa mjini na hata nje ya nchi Kabisaaaaaaa.
Itakuwa vyema sana.
Aaaaa kuna Jambo pia nilikuwa nalifikiria kwa Wewe.
Jambo gani mume wangu?.
Aaaaa nilitaka ujifunze vitu kama viwili kwa miezi kadhaa hivi. Aaaaaaa Nataka ujifunze compyuter na lugha ya kiingereza.
Daaaa umejuaje."Zamda alifutarahi Sana. "
Aaaaa ni kutokana na hicho cheo ambacho utakuwa nacho Kwakweli vitu kama hivi haviepukiki kuvijua.Kama ni safari za nje lazima ziwe za kutosha.
Sawasawa. Hapo Sawa.
Mathalani taarifa mbalimbali unahitaji udhihifadhi kwenye compyuter.
Sawasawa.
Kwahiyo itakuwa vizuri sana kama ukijifunza hiyo issue.
Sawasawa.
Basi Natumai hayo Mambo yote yatakuwa yamekamilika Baada ya kama miezi sita hivi.
Ndiyo. Sehemu gani wanafundisha vizuri compyuter?.
Zipo nyingi tu.Tulia kesho tutaenda mjini nikupeleke Hiyo sehemu ili Jumatatu uanze mafunzo.Hiyo sehemu kuna wakufunzi wazuri Sana.
Sawasawa.
Hadi na wewe ukishakamilisha mafunzo yako Basi na mimi tayari ntakuwa hata Mambo ya kufungua hiyo sehemu yatakuwa tayari na pia hata Mimi kwa mambo ya masomo ya A-levels ntakuwa nimeshakamilisha .
Sasawa mume Wangu.
Baada ya kupita miezi miwili mbeleni Hivi Kijana Zaidu Sudaysi Zaidu aliweza kuteuliwa na waziri wa Mambo ya uchumi bwana Kaizage kabuziri kuwa kama Balozi wa vijana.Waziri Kabuziri alimchagua Zaidu Sudaysi Zaidu kuwa kama balozi wa vijana ni Kwasababu tu ya namna Zaidu Sudaysi Zaidu anavyokuwa na uchapakazi wake.
Basi siku hiyo ikiwa ni Siku ya jumamosi ambapo ndiyo Mambo ya uteuzi yalifanyika hapo. Uteuzi huo uliohudhuriwa na Viongozi wa sekta nyingine mbalimbali.Waandishi wa habari mbalimbali Kwakweli walijaa sana katika eneo hilo ili kuweza kupata vitu vya kuweza kuuza katika magazeti mbalimbali na Runinga mbalimbali.
Basi uteuzi huo ulifanywa mishale ya saa tatu asubuhi. waziri Kabuziri mda huo akiwa amekaa mda huo maiki za waandishi wa habari zikwia zimejaa Mbele yake kweli. Kwa pembeni katika mkono wake wa kulia akiwa amekaa kijana Zaidu Sudaysi Zaidu na wanaofuatia ni viongozi mbalimbali kama vile kutoka taasisi za elimu mbalimbali.
Basi mda huo waziri Kabuziri alikuwa akisema Hivi.
Ni Furaha njema kuwa hapa Jamani. Pia niwashukuru sana waandishi wa habari kwakuweza kuwa Basi katika kuweza kuweka rekodi za Mambo yanayofanywa.Aaaa ni Ghafla ndogo hivi imefanyika hapa .Ghafla hii ina madhumuni yake.Aaaaa siku zote katika hali ya kawaida katika Jamii lazima kila mtu kuwa na rolemodo wake.Yaani kwamba kila mtu Ana yule mtu wake kwamba akifanya hivi na wewe unafanya.
Kwahiyo kwa Sisi Basi kama nchi ya Kinani kupitia katika sekta ya Kiuchumi. Tumeamua kumchagua kijana ambaye ni mjasiriamali Mali akiwa bado Kweli ni mdogo Sana. Naye si mwingine Bali ni Zaidu Sudaysi Zaidu.
"Hadhira (watu walimpigia makofi Kijana Zaidu Sudaysi Zaidu pindi waziri Kabuziri aliposema vile. Kisha waziri Kabuziri akaendelea kusema hivi".
Ni Kijana ambaye bado yuko kwanza kwenye masomo miezi ikiwa imebaki kidogo tu na Yeye kuweza kumaliza kidato cha sita.Lakini tukiangalia Mambo ambayo ameyafanya kwelikweli Tangu ashinde tunzo ya uandishi wa hadithi za kufikirika na zisizo za kufikirika za dunia Kwakweli amezidi kupiga hatua Zaidi.
Kwasababu ingekuwa ni mtu mwingine hapo tayari angeanza kujibweteka tu na kusema Kwamba Yeye ni star sana Kwahiyo wala asijoongeze tena .
Zaidu hadi mda huu hajafikisha hata miaka thelathini Lakini tayari kwa miezi huwa kodi zake kwa ujumla analipa hadi asilimia sabini na Tano kabisaaa hata themanini.Kwahiyo ndiyo maana tumeamua kumchagua kama balozi wa vijana ili naye azidi kuwahamasisha vijana mbalimbai katika nao kuweza kujikomboa kimaisha na kutokubaki kusubiria ajira kwa serikali.
Zaidu kwa historia yake kama mtu atakuwa amesoma kitabu chake Ambacho amekitoa siku za Hivi Karibuni tu kiiitwacho MAISHA YANGU Kwakweli utajikuta wewe kama mtu ambaye umezaliwa mjini,ukakulia mjini,ukasomea mjini na Mambo yote mjini bado hujapiga hatua. Wakati kuna mwenzako hapa mjini Kwasasa Sijui ana mwaka wa tano tu Hivi maisha yake si  kama ya mtu aliyeishi hapa mjini miaka ishirini na kitu Lakini bado anategemea ugali wa shikamo.
Ni vyema sana mtu kuweza kutumia akili ili na wewe kuweza kupiga hatua zenye maana.Haina haja yoyote ya kupiga hatua fulani kwenda mbele alafu ukishapita tu tayari hatua zako zimefutika.
Vijana tuwe makini Sana kwa umri tulio nao kwa Sasa.Basi nisichukue mda mrefu Sana katika kuongelea jambo hili.Ni vyema Sana nikamruhusu balozi wa vijana nchini Kinani kijana wetu Zaidu Sudaysi Zaidu. Karibu.
"Nakweli mda huo akawa amesimama Zaidu na akaanza kusema hivi".Habari za asubuhi Jamani. Ni Furaha isiyokifani kwa mimi kuwepo hapa na kuweza kupewa cheo hiki na Mimi Nasema nawashukuruni sana wanauchum wakiongozwa na waziri Kabuziri kwakuweza kuona mihangaiko yangu na hatua zangu ambazo nilipita mahali huwa hazifutiki lazima ziwapate watu wa kuingia katika hatu hizo.
Jamani sina mengi sana ya kuzungumza bali tutaanza tu kuwa pamoja pindi nikishamaliza masomo yangu ya A-levels.Niseme Shukurani sana Jamani.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)