MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 29

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 29
#1
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU
SEHEMU YA 29
Mda huo Jeni akiwa anarekodi pale hakuna aliyekuwa akijua kama Jeni alikuwa anafanya jambo hilo. Kwahiyo matusi na maneno mengine chungumzima ambayo ni machafu yakawa yamezidi kwelikweli.
Lakini kweli mda huo Zamda akawa analazimisha aingie ndani hapo ndipo Tito alipozidi kupandisha hasira kwelikweli. Akawa kweli kama anamtishia kumchoma na kisu hivi kisha Jeni akasema Hivi.
Zamda toka tu nje .
Sawasawa.
" Tito akasema ".Ndiyo mwambie atoke nje sijui lugha hii ngumu Sana tunayoizungumza hapa.
Sawa natoka.
Ndiyo utoke Sasa hivi.
" Mama Tito akasema ".Ndiyo utoke na hao watoto wako kabisaaaaaaa na Mizigo yako hiyo.
Sawa natoka nao.
Haya Kwaheri kafie Mbele huko.
" Tito akawa  anasema Hivi "Mwanamke, mwanamke gani wewe.Kati ya wanawake hata wa mtaa wakiitwa unafikiri na wewe utatoka kabisaaaaaaa.
" Mda huo Jeni akiwa bado ameshikilia simu Yake .Wakawa wanamshangaa na Jeni naye anatoka nje akiwa amevaa suruali Yake hivi na Kuanza kumfuata Zamda anapoelekea.
Kwahiyo hadi mda anaondoka tayari na giza kidogo limeshaanza kuingia.
Pale nyumbani Kwakweli walibaki wakiwa wanashangaa tu Kisha mama Tito akamuuliza Tito Hivi.
Huyu Jeni naye anaenda wapi?.
Hapo Ndiyo sielewi kabisaaaaaaa.
Si Kwamba anamfuata Zamda.
Hawezi kumfuata.kwanza amfuate huyo Zamda Ana Msaada gani kwa Jeni.
Huwezijua Tito.Inawezekana kuna mchezo umechezwa hapa.
Ayaaaa, mchezo gani Sasa huo utakaochezwa utuletee madhara?.
Ohooooo. Wewe chukulia masihara tu.
Wala.Jeni mtu wangu wa karibu sana ananielewa vizuri.
Haya Ndiyo ujiulize swali huyo Jeni anaenda kufanya nini huko anakokwenda Zamda.
Kwani wewe Unajua Zamda anakoenda?.
Anaenda Kulala stendi huyo na watoto wake.Nakwambia watamuibia kila kitu.
Inawezekana Kweli.
Ila Lakini embu ingia hapo chumbani kwa Jeni uangalie pakoje.Kwasababu tusijetukawa tunajipa moyo tu kumbe tunaishi na bonge la kinyonga hapa.
Kivipi yaani?.
Siyo kivipi Yaani tena.Wewe ingia hapo ndani angalia kama kuna vitu ili tuwe na uhakika wa tunachokiongea.
Sawasawa.
Nakweli Tito akawa ameelekea mlangoni na Kisha akafungua mlango na kuingia chumbani. Alipoingia tu hakukuta kitu chochote kisha akasema Hivi.
Mamaaaaa aaaaaa.
"Mama Tito akiwa sebuleni huku anakimbilia chumbani kwa Jeni akiwa anasema Hivi".Nini huko .Tito umekuta nini huko?.
Mama uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Nini Tito.
Hamna chochote huku. Yaani pamebaki kama alivyopakuta alivyokuja kipindi ile kupangisha.
" Mama Tito tayari mda huo kaingia chumbani na kusema hivi "mbona Kweli.
Ndiyo  maana Yake. Yaani amechukua vitu vyake vyote kasepa.
Sasa huko wanaenda wapi?.
Yaani mama kwahilo swali ni jipya kabisaaaaaaa kwangu.Hapa Sasa Kweli huyu kinyonga.
La kufanya Sasa.
Hatuna la kufanya.
Kwakweli Tito mategemeo yake ya kusema Kwamba atakuwa anaburudika sana na Jeni yakawa yameishia njiani. Mda huo akiwa yuko chumbani kwake pekee yake akawa anaongea huku akisema Hivi.
Duuuuuuuuuuuu Yaani huyu demu ni kweli ndiyo nimeshamkosa kabisaaaaaaa. Haaaaaaa kweli Jeni mbona siamini. Kwani wewe siuliniambia kwamba utaishi hapahapa. Duuuuuuuuuuuu laki tano imeenda, sijui ile hela ya kodi nayo imeenda, halafu hujanionjesha hata utamu wako.duuuuuuuuuuuu Kwakweli kuna wadada hapa mjini wengine waangalie tu hivyo na kuwatema mate kabisaaaaaaa. Sasa hapa Mimi sielewi kabisaaaaaaa. Yaani sikuwahi kuhonga demu namna hii alafu nisimuonje hata kidogo. Yaani nimeishia mate tu Kwa Jeni.Sasa huyu Jeni Yaani kabisaaaaaaa simuelewi Yaani hata kidogo. Mbona alikuwa haoneshi sura yoyote ya kusema atanisaliti hivi. Amakweli nimeamini msemo usemao Kwamba Msaliti naye kusalitiwa.Daaaaaaa Amakweli Hawa wadada wa mjini ni noma kabisaaaaaaa. Duuuuuuuuuuuu nimemkosa Zamda na nimemkosa Jeni.
Ikiwa ni siku iliyofuatia asubuhi na mapema Yaani ni mishale ya saa tatu asubuhi Hivi. Wanaonekana Zamda, Jeni wakiwa wamekaa kwenye kochi ambapo hapo ni kwenye chumba ambacho Jeni amekipangisha.Kinavyoonekana ni chumba kikubwa kabisa. Ambapo alipangisha vyumba viwili hivi. Basi mda huo Zamda, Jeni Wakiwa na rafiki yake Jeni aitwaye Rumda.Rumda kwa utaalamu Yeye ni mwanasheria katika mahakama kuu ya Kimbu. Sasa mda huo kuna mpango ambao Walikuwa wakipanga kuhusiana na tukio amablo alifanyiwa Zamda siku iliyopita.Mda huo Rumda alikuwa akisema Hivi.
Jamani hapa Mimi nachotaka ili niwakamilishie Hilo jambo chamsingi ni  kuwa na hizo taarifa ambazo ni muhimu kabisaaaaaaa.
"Jeni akasema Hivi"Kama taarifa gani?.
Aaaaa chakwanza ni ushahidi ambao unaonesha kwamba kweli huyu rafiki yako alikuwa akitishiwa.
Ayaaaa sikiliza Rumda.Hapa nina tukio zima la Jana ilivyotokea.
Ulifanyaje?.
Nilirekodi.
Ahaaaaaaaa. Unayo hiyo rekodi kwenye simu hapo?.
Ndiyo Ninayo hapa.
Basi sawa ushahidi tunao wa kutosha Kabisa.Nakwambia huyu leo leo anafikishwa mahakamani.Kwahiyo Dada hata usiogope."Dada huyo anayemwambia ni Zamda. Kisha Zamda akasema Hivi".
Sawa.
" Jeni akasema Hivi ".Rumda Kweli uifanyie kazi Kweli Kweli. Kwasababu huyu jamaa nataka tumuoneshe Kweli na sisi tunaweza.
Hamna Jambo litakalokwenda mrama hapa.kila kitu kitaenda vizuri.
Sawasawa.
Kwahiyo Kweli baada ya mazungumzo Yale kumalizika tayari wakawa wametoka wote Lakini Zamda akawa amemuacha Glady ambaye ni mwanaye wa kwanza. Kwasababu huyo hata kutembea na kucheza na wenzake anaweza kabisa.Kwahiyo kuna wapangaji wengine Walikuwa na Watoto wao hapo Kwahiyo kwa wale watoto wakawa wanacheza na Glady pale.
Walienda hadi katika mahakama hiyo ambako anakofanyia kazi huyo Rumda.Kisha Rumda akawa amewaelekeza vizuri eneo dhahiri la kuweza kutoa malalamiko ya Zamda ili huyo Tito aweze kufuatiliwa.
Kwakweli yalikuwa ni kama majonzi sana kwa familia ya nyumbani kwa kina Tito ila kwa Upande mwingine Zamda ilikuwa ni Furaha kwake ndipo hata akawa amepata na hata nafasi ya kuwasiliana na Zaidu vzuri.
Basi Siku hiyo Zamda na Zaidu walikuwa na maongezi kidogo Kwenye simu.Kwasababu kwa kipindi hicho Zaidu hakuwa amerudi nyumbani kwao Bali yuko sehemu nyingine ambapo sehemu hizo Walikuwa wakienda sana na mheshimiwa waziri wa habari michezo sanaa na utamaduni ila kwa siku si chache tu ataweza kuwasili mkoani Kimbu.
Mda huo Zamda akiwa amekaa kibarazani Hivi na huko sehemu anakoonekana huyo Zaidu ni katika Jumba fulani Hivi la kifahari akiwa amepumzika vyema sana. Mda huo ilikuwa ni mishale ya saa mbili usiku. Maongezi yao yalikuwa hivi.
Mambo vipi mke Wangu?.
 Safi.
Duuuuuuuuuuuu siku mbili tatu hivi hatujawasiliana.
Ni kweli.
Nini tatizo?.
Hamna tatizo mme wangu.
Aaaaaa Mimi nahisi kuna tatizo.
Hapana huku kuna furaha sana Mbona.
Kwanini?.
Siishi tena na Tito.
Kweli Zamda unachoongea?.
Ndiyo maana Yake nakwambia mme wangu.
Ahaaaaa alafu wiki iliyopita Jeni alinieleza kuhusiana na huo mchongo wenu Lakini nikawa nimesahau.
Usisahau Jamani. Unajua kuanzia Sasa Mimi ni mke wako wa halali Kabisaaaaa.
Ni kweli. Basi Zamda siku si chache naweza kuja huko. Ila Nataka tuje tufanye hata kuhama huko Kimbu tuje kuishi huku.
Kwanini mme Wangu.
Aaaaaa Kwaujumla Mimi kwasasa ni mtu ambaye najulikana katika ofisi mbalimbali za kitaaluma.Na Mambo haya ambayo niliyashinda juzi hapa fursa zao nyingi sana ziko katika huu mkoa.
Kwahiyo Kweli Unataka tuhamie huko?.
Ndiyo maana Yake.
Vipi kuhusu Jeni?.
Hata Jeni tunamtoa huko na  kuja kumpangishia Nyumba huku na Lazimaaaaa nimfungulie biashara yoyote nzuri hivi ya kumuingizia fedha. Kwasababu Kwakweli Jeni amenisaidia katika vitu vingi sana tena sana.
Ni kweli. Kwahiyo mume wangu huku unakuja lini?.
Nitakuwa huko siku si chache sana. Kwasababu kuna mikataba tu naanza kuingia na baadhi ya watu huku Kwahiyo wala usihofu Mimi niko kwaajili yako mke wangu.
Sawasawa mme wangu.
Haya.Lakini watoto hawajambo kabisaaaaaaa?.
Ndiyo wako vizuri Kabisaaaaaaa.
Ahaaaaa basi vizuri sana.
Mimi nikawa najua ndiyo tayari umeshaanza kunisahau hivyo.
Weeeeeeeeeeeeeeeeee...... Weeeeeeeeeeeeeeeeee Yaani ntaanzaje anzaje kabisaaaaaaa.
Siwezi jua Kwasababu Yaani Sijui nisemeje.
Nikwambie Kitu Zamda.
Mimi kama tangia mwanzoni tu nilivyokueleza kwkaweli Zamda hata ingekuwa vipi wewe lazimaaaaaa tu ningekuoa.Nanilishakuahidi kabisaaaaaaa Zamda. Siwezi kukutenda,Yaani siwezi kukusaliti hata siku Moja.
Kweli kabisaaaaaaa Mme wamgi.
Ndiyo Ukweli wenyewe huo.
Haya .Nasubiri basi kwa uhakika.
Sawa.Zamda kumbuka wewe ndiyo ambaye mda wowote nilipokuwepo huko Kimbu ulikuwa ukinipatia mautamu sana.Halafu kwasasa kirahisi rahisi tu Unataka Yaani Weeeeeeeeeeeeeeeeee. Siwezi kukusaliti kirahisi Hivyo Wewe.
Haya.
Nilishakwambia tena kuhusu hao watoto wala usiumize kichwa chako Kabisaaaaaaa. Wote nitawahudumia kwa namna yoyote ile huku tukiwa tunaendelea kutafuta wengine.
Haya bana wanifurahisha wewe Jamani.
Lazima nikufurahishe mke wangu Jamani. Unafikiri nani mwingine tena ndiyo nimfurahishe?.
Mashabiki zako.
Ahaaaaa ukiachana na Hayo mambo. Mimi nazungumizia kwenye Mambo ya MAPENZI kwa Sana.
Ahaaaaa. Kwa hapo wakunifurahisha ni Mimi tu.
Basi sawa ndiyo hivyo.Sasa Kwahiyo Zamda nakuomba niamini kwamba Kabisaaaaaaa sitokusaliti.
Sawasawa.
Kwakweli kwa siku ile wapenzi wale walifurahika sana nyoyo zao baada ya kila mtu kuweza kusikia sauti ya mwenzake.
Ikiwa tayari kesi ya kutishia kuua iliyokuwa ikimkabili Tito tayari imeshafikishwa mahakamani na tayari hata huyo Tito ameshashikiliwa na polisi na hadi watu wa ustawi wa Jamii wameshalipata jambo hilo Yaani malalamiko hayo ya Zamda.
Kwahiyo baada ya kupita kama wiki hivi tayari Tito akawa amehukumiwa kifungo cha miaka Kumi kwakutishia kuua na akiwa anahitajika pia kulipa faini ya shilingi laki tano.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)