MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 22

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 22
#1
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU  
         
SEHEMU YA 22
  Yaani Tito unanijibu kiurahisi rahisi tu ?."Mda huo Zamda  amechafukwa na sura Kweli Kweli Yaani hasira zimempanda kweli kweli ".
"Mda huo Tito kainuka kutoka kitandani na akawa amekaa  akiwa anaongea huku anamuangalia Zamda. Ilikuwa hivi"
Kwani wewe ulitaka nikujibu kigumu gumu au vipi wewe Zamda.Yaani nakushangaa sana kinachokuleta  juu ni kipi Sasa.
Kipi sasa. Hivi wewe Tito mbona huna moyo wa ubinadamu Kabisa.
Yaani tuseme Mimi nina moyo wa wanyama kama simba sio?.Embu fikiria na unachokiongea.kwani umemuona huyo msichana Hapa?.
Hapana.
Sasa nini makelele?.
Nimesikia sauti ya kike. Alafu kabisa mnawekeana ahadi.
Kwani ahadi ni kwa wanawake tu.Wewe vipi aise.embu usinichanganye akili yangu.
Hivi Tito tulia nikuulize swali Yaani rahisi sana.Kwasababu nahisi kama tunataka kufanyana watumwa Hapa.
Sawa.
Hivi wewe ndiye uliyenitongoza kabisa kwa mara ya kwanza Kabisaaaaa au Mimi ndiye niliyekulazimisha tuwe kwenye mapenzi Mimi na Wewe.Tito ulinipamba sana wakati ulipokuwa ukinitaka.
Swali Hilo Kwakweli Zamda ni Sawa Sawa na mwanafunzi wa chuo kikuu umuulize swali la kujumlisha na kutoa.Nahisi Majibu yatakuwa marahisi tu kama ilivyo kwako.
Sijaona kama umenijibu swali Langu.
Hapana, nilikuwa nakupatia ufafanuzi Zaidi.
Ufafanuzi wa nini wewe. Mimi nimetaka ufafanuzi Au Majibu.
Yote kwa pamoja.
Hapana. Mimi Nataka Majibu tu.
Unajua Zamda kichwa chako na akili yako iko kama ya panzi Mwenye usahaulifu sijui kama nini vile.
"Hapo ndipo tena Hasira zilimzidi na kujikuta hadi analia tu.Akasema Hivi"Mimi kabisaaaaaaa wanifananisha na panzi kabisaaaaaaa.
Kwasababu panzi ndiyo mwenye kichwa cha kusahau kama wewe .
Nini nimesahau.
Nilishawahi kukuambia  kwamba hapa nyumbani nini kabisa unachokosa ?.
Nakosa mapenzi ya dhati.
Kutuoka kwa nani?.
Kwako wewe....Au mwingine nani... Weee si Ndiye uliyenipa hizi mimba zote Au wewe siyo Tito.
Labda,yawezaikawa Hivyo.Nilishakwambia kwamba hapa nyumbani unakula bureeeee, unalala bureeeee, unakunywa Bureee, unaagalia bureee kila kitu Bureee tu hapa. Sasa nini tena wataka ?.
Tito asante sana kwakunifanya Mimi kama mtumwa wa mapenzi. Ila iko siku Chozi langu moja hili unaloliona linatoka Jichoni mwangu basi najua iko siku Chozi hili halitakuwa kama Chozi la hasara kama la mda huu. Lahashaa.
Bali litakuwa Chozi gani.
CHOZI LA DHAHABU.
Yaani wewe ndiyo unachekesha umati kabisaaaaaaa.
Haina shida. Yaani Tito unaongea na mchepuko wako huko na Mimi nikiwepo kabisaaaaaaa Hapa. Sawasawa. Malipo ni Hapa Hapa Duniani akhera mahesabu.
Kwakweli Zamda na Tito walirushiana maneno hadi wakapitiliza na hadi mtoto ambaye Zamda alimlaza pale kitandani akawa ameinuka.
Basi ni baada ya kupita kama mwezi mmoja hivi ambapo Kipindi hicho naye Mtoto wa mama Tito aitwaye Bite alikuwa ameshajifungua.Kwahiyo Bite akawa halali huko maeneo ya chuo bali akaamua  kurudi nyumbani na kwenda chuo kila siku.
Pia naye Mwanadada Bite jamaa ambaye alimpatia mimba alikuwa ni muislam akiitwa Mpundu.Sasa siku Hiyo wakawa wameitishwa tena kikao kwa mara nyingine wakiwemo Mpundu,Tito, Zamda na Bite.Aliyewaitisha kikao ni Mama Tito ambaye ndiye Kama kichwa cha familia ile.Yaani Yeye Ndiyo Baba na Yeye ndiyo Mama.
Wanaonekana sehemu waliyokuwa wamekaa ni sebuleni huku Runinga ikiwa imepunguzwa Sauti. Muongezi mkuu alikuwa ni Mama Tito. Ambapo mda huo ni mishale ya saa saba mchana ni baada tu ya wao kumaliza kupata chakula cha mchana ambacho Walikula kwa pamoja.
Basi muongeaji wa kwanza katika kufungua kikao kile alikuwa ni Mama Tito. Ilikuwa hivi.
Aaaaaaah niwashukruni kwakutii taarifa yangu ambayo niliwatolea kuhusiana na kikao cha leo.Aaaaaaàaaa Mpundu karibu Sana.
Asante Mama.
Aaaaa lengo kubwa la Mimi kuwaiteni hapa na ndiyo Kama lengo kuu ni kuhusiana na uchumba wenu mlio nao kwa mda huu.Natumai hiki ni kama kikao cha Mara ya pili nimekiitisha na mada ikawa inazungumziwa hii hii.Au sivyo Jamani.
"wote walijibu"Ni kweli
Basi kama ndiyo Hivyo kwamba ni Kweli nitafurahishwa na namna Kweli kikao kitakavyokwenda.Kwahiyo swali ambalo nilishawahi kuliuliza Basi leo pia itanipasa niulize.
" Wote walijibu"Sawa
Aaaa....swali langu kubwa ambalo ndilo kama litafungua na kufunga kikao kwa siku ya Leo ni kwamba vipi kuhusiana na suala la utofauti wa kidini mlio nao?."Kwa mda huo kidogo palinyamaza kimya  walipokuwa wamekaa mathalani ya shetani kapita sehemu hiyo Kwa ukimya uliokuwa umetawala.Lakini baada ya kimya cha mda kidogo ndipo huyo Mpundu akaamua kuongea jambo Fulani."
Aaaaa....mama Hilo ni swali zuri sana na pia natumai hata Majibu yake yatakuwa hivyo Hivyo kutoka kwangu.Aaaaaaàaaa ni kwamba Hilo suala nalo kwa Mimi limeniumiza sana kichwa na wazazi wangu nimewauliza swali hili.Lakini Majibu wanayonipatia ni Majibu ambayo yanahitajika kuwa katika ukweli Wangu.
"mama Tito akasema Hivi"Ukweli gani huo Mpundu?.
Aaaaa Kwaujumla niseme tu dini ni kama utamaduni hivyo Basi kama ni utamaduni Kwahiyo unaweza kubadilika. Lakini kwangu kwakweli naona utamaduni wangu bado umetuwama katika kuamini kwa utamaduni niliozaliwa nao au dini niliyozaliwa nayo.
Kwahiyo ukimaanisha Kwamba.
Nikimaanisha kwamba ni vigumu kwa Mimi kuweza kuingia katika utamaduni ambao sikuzaliwa nao.Japokuwa Kweli nampenda sana Bite kama mchumba wangu na mke wangu mtarajiwa.
Aaaaa Kwahiyo Mpundu kwamba unaamua kusimamia katika imani yako?.
Ndiyo maana yake mama.Nitaomba uninuie radhi sana Kwasababu hata wazee huko Kwakweli hawajaafiki kabisaaaaaaa Kwa Mimi eti kuweza kubadili dini kwaajili ya Suala hili Lahasha.
Basi Sawa.
Kwakweli kwa mada ile waliyokuwa wakijadili kwa siku ile kila mtu alitetea upande wake hadi maamzi yanakuja kufikia  kutolewa kwamba ni vyema tu kila mtu akafuata imani Yake.
Kwasababu ni vigumu sana mtu kumuingilia imani ya mwenzake.Ulikuwa muislam Kwasababu ya umezaliwa katika familia ya kiislamu na umekuwa mkiristo Kwasababu umezaliwa na ukawakuta wazazi wako ni wakristo Au ni kwa Upande mwingine ni Mchanganyiko kabisa. Basi ni vyema sana kwa kila mtu kuwa na maamzi ya kuweza kufanya jambo jema linalomtuma kichwani mwake.Si kwamba watu wake wa Karibu kumlazimisha .
Basi siku Hiyo ikiwa ni siku nyingine kabisa. Wakiwa wanaonekana Zamda na Jeni wanamaongezi kidogo. Mda huo Jeni akiwa amejifunga kanga tu hadi Kwenye kifua.Jeni naye kama kawaida yake kajifunga naye kanga tu.Basi maongezi yao yalikuwa hivi.
Hivi Jeni mbona Mimi naona Ndiyo mateso yanazidi sana kwangu?.
Unajua shoga yangu Zamda siku zote mvumilivu hula mbivu.
Sasa Mimi hiyo mbivu ntaila lini.Kwasababu ni kila siku nala mbichi tu.
Sasa Ndiyo unisikilize vizuri Zamda.
Sawa.
Zamda naposema mvumilivu hula mbivu nina maana kubwa Sana.
Ipi Hiyo?.
Unajua Zamda Kwasababu ni mda Natumai tu tayari umeshawadia.waache wakutese tu na mwisho wa siku wataamua hata kukufukuza.
Ntaenda wapi Sasa?.
Sasa wewe tulia tu utajua ni wapi mahali pakwenda.Zamda Mimi namuamini kabisaaaaaaa Zaidu kama hata ni asilimia elfu moja lazima atakuoa tu.Yule akirudi siyo mtu wa utani utani tena.Wewe kwasasa vumilia tu yataisha siku si chache. Zaidu kile ni kipaji chake kabisaaaaaaa amejaaliwa na ataweza kushinda kabisa kwa ninavyoamini na ninavyomuombea ashinde.
Kwa Zaidu Kwakweli Hilo halipingiki kwangu kabisaaaaaaa. Yaani Jeni kwa hapo sipaachii.
Ndiyo hivyo Kwasababu Wewe  jifanye kama mjinga tu.wewe siku hiyo wakileta tu ng'eweeeeee na wewe unafanya tu kweeee.Zamda kila kitu kina Wakati wake Kwahiyo wala hata usihofu haya majanga iko siku yataisha tu .
Lakini Jeni kwa yanayoendelea hapa Ndani. Yaani Tito kuna mda usiku hivi tuko nae kitandani anaanza kuchati na michepuko yake huko.
Sasa Ni Sawa anavyokufanyia Kweli si vyema bali wewe jifanye wewe ni mjinga tu.Kwasababu haelewi hapa mjini akili tu na ujanja wako.wewe subiria kwanza Zaidu arudi ndipo Sasa timbwili timbwili tuliamshe kwa mda huo.
Nakutegemea wewe Unajua Jeni.
Najua kabisa.
Kwahiyo nakuomba uijseniangusha shogaaa.
Yaani nakwambia Zaidu akirudi hapa mbona matajiri.Zaidu Nakumbuka siku moja aliwahi kuniambia Kwamba alishawahi kushiriki kwenye haya mashindano kwa Mkoa tu akawa amezawadiwa laptop tano na Ndiyo moja wapo ile ambayo ulikuwa ukimuona akija nayo Mara nyingi hapa kipindi akiwa huku Kimbu. Kwahiyo kwa yule ni asilimia mia moja kabisaaaaaaa.
Yaani kwa Zaidu Natumai hata nitakuwa naishi kama mwanadamu.
Haina shida yatakwisha tu iko Siku. kwanza mbona zimebaki siku chache tu.
Ili arudi siyo
Ndiyo maana Yake.Yaani lazima atangazwe kwenye TV.
Yaani mbona watabaki macho kodo tu.
Ikiwa ni siku nyingine kabisa Mishale ya saa Kumi jioni.wanaonekana Zamda na Tito wakiwa sebuleni. Inaonesha kabisa siku Hiyo watu kwa hapo nyumbani wengi walitoka sana kwa Siku hiyo Yaani kwenda matembezini.Pia hata Jeni hakuwepo.Ilikuwa ni Siku ya jumapili. Zamda alikuwa akisema Hivi.
Tito nakuomba nikuulize swali au hata kama maswali kama inafaa.
Uliza.
Hivi Tito nini hatima ya penzi Letu?.
Hatima?.
Ndiyo Hatima.
Nini maana ya hatima?.
Unajua ila Unataka tu kurefusha mada Hapa.
Sawa.Aaaaa.hatima ya penzi hili sijui Kwasababu bado naona lipo gizani.
Hivyo Unamaanisha uchumba wetu hautofika mahali?.
Inawezekana Hivyo.Kwasababu Watu wanaweza kuishi kwenye uchumba ni kama hata miaka kadhaa hivi na wakaja kuachana kiurahisi tu.
Ndiyo lengo lako kwangu au siyo?.
Yawezekana.
Haaaaa eeeee mungu weeeeeee nisaidie miye muja wako.
Dua yako itakubaliwa lini?.
Najua itakubaliwa tu
Pole sana kwakusubiri maembe kwenye mti wa mbuyu.
Sawa haina shida. Ila  kumbuka tu Tito nzi anasema Hivi kama  Wewe Unajua kwa Mbele Basi na Mimi najua kwa nyuma.
Kitaelewela mbeleni bana. Acha Mimi kwanza niende kijiweni
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)