08-19-2021, 09:35 AM
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU
SEHEMU YA 09
Sasa ghafla Dada wa Tito ambaye anaitwa Bite akawa ameona mbona haya Mambo kama yamezidi ndipo akawa ameamua kutoka nje ili kuweza kufanya hata angalau utatuzi tu wa makelele yanayoendelea pale.Anafungua mlango Kweli anamkuta mama analazimisha kuwatoa Zamda na Tito, Yaani mda huo Zamda ni analia tu hata haelewi ni wapi aende kama kweli Ndiyo hali hii.
Basi baada ya Bite Kutoka akiwa amevalia nguo za kulalia nywele zake akiwa kaziachia Kweli Kweli zilizokuwa na urefu kweli kweli hadi mabegani na umbo lake alikuwa amejaaliwa Yaani Ana mofolojia ambayo Kwakweli ya kipekee kwelikweli. Si mrefu sana wala si mfupi sana rangi yake ni mweupe Mwenye unene fulani Hivi. Basi Bite akaamua kuingilia kati kwa kuanza kusema Hivi.
Mama Eee mama wasamehe,"Mda huo akiwa anamkimbilia mama amshike Mkono Kwasababu anawalazimisha kwelikweli Tito na Zamda watoke nje kwakuwasukuma kisha mama Tito akawa amesema hivi".
Na wewe usiniingilie hapa,unaona Kabisa huyu mdogo wako kafanya maujinga hapa alafu bado unamtetea tu hapa.
Mama embu kwanza waache kwanza, ni Sawa wamekosea tena aliyekosea ni huyu Tito Lakini kwa mda huu ni mbaya, Kwanza ukifikiria huyu mdada wa watu inawezekana hapajui hata huku Kimbu hata kidogo. Kwahiyo hata ukiwafukuza inawezekana Tito akamuacha huyu mwanadada hapo na huyo mdada akapotea.Sasa jiulize hapo atamlaumu Tito Au wewe uliyewafukuza?.
Bite unajua Tito amefanya makosa makubwa Sana, Yaani Kabisaaaaaaa.
Ni Sawa mama Ndiyo Hivyo Mambo ya Vijana haya embu punguza hasira Kwasababu itakuletea hasara Kweli Kweli.
Kwakweli matarajio ya mama Tito kwa mwanae kwakweli yalianza kukwea yaani bila mafanikio yoyote Kabisa. Mama Tito ni mwanamama ambaye kwa ujumla ni mwanauchumi ambapo shahada (degree) yake ya uchumi aliweza kuipata miaka ya nyuma sana katika chuo kikuu cha Kimbu.Elimu yao ya awali aliipatia kijijini kwao huko.Kwakweli mama Tito ni mwanauchumi ambaye aliweza kuonesha uanauchumi wake kazini pamoja na nyumbani. Kwasababu nyumbani hapo alikuwa na banda la kuku ambao Walikuwa ni kwaajili ya biashara, Hivyo Basi kuku wale walimsaidia katika kuweza kuinua vizuri kipato chake na kuweza kujiendeleza vizuri kimaisha badala ya kutegemea tu mshahara wa kazini.
Mama Tito alikuwa akionesha uanauchumi wake Hivyo Kwasababu pia Yeye Ndiye ambaye kama alikuwa kichwa cha nyumba.Yaani ndiyo mama na ndiyo Baba. Yote hii ni Kwasababu mme wake wake aliweza kufariki miaka kadhaa iliyopita.Ambapo mume wake mama Tito Kwakweli ni mtu ambaye alikuwa amejulikana sana katika mkoa wa Kimbu kutokana na cheo chake alichokokuwa nacho.Ambapo cheo chake alikuwa mhandishi katika mkoa wa Kimbu. Kwahiyo hakuna jengo Ambalo Kwakweli hapo mjini bila Yeye kama lingekamilika.Lakini Ndiyo Hivyo waswahili Wanasema kizuri hakidumu.
Sasa siku Hiyo ikiwa tayari imeshapita miezi kaka mitano hivi tangu Zamda kupewa mimba na Tito na akawa amekubaliwa kwamba aishi pale.Siku hiyo Mdogo wake mama Tito aitwaye Benedetta alikuja kumtembelea Dada yake Yaani mama Tito. Benedetta naye ni Mwanadada ambaye Kwakweli alijaaliwa kuipata elimu yake ya juu na pia naye alisomea Mambo ya uchumi hivyo basi hiyo ikawa ndiyo shahada yake ya Kwanza. Baada ya kumaliza tu chuo tayari akawa amefanikisha kupata nafasi ya kwenda kufanya kazi kwa mkataba huko nchini Marekani. Kweli nafasi ile hakuweza kuilalia mbali na akawa ameifanikisha nafasi hiyo.
Alienda nchini Marekani na kufanya kazi kwa mda wa miaka Saba. Kwahiyo hata pindi mme wa mama Tito alipofariki Benedetta hakuweza kuwasili katika mazishi.Basi baada kurudi kutoka huko nchini Marekani ikabidi aje hadi nyumbani kwa mama Tito huko Loronjo mkoani Kimbu.
Basi mda huo wakiwa wanaonekana wamekaa sebuleni wakiwa wanaangalia Runinga. Kwa siku hiyo ilikuwa ni siku ya Jumapili mda huo ikiwa ni mishale ya saa saba mchana.Basi Siku hiyo ndipo Sasa ikabidi mama Tito aweze kumweleza vizuri nini haswaa chanzo cha kifo cha baba Tito.
"Mda huo mama Tito akiwa amekaa kwenye kochi akiwa ameshikilia remote (kitenzambali) huku akimpa simulizi ya kuhusiana na namna kifo cha mume wake kilivyoteokea". Mdogo wangu kifo cha mme wangu Kwakweli ni kifo cha kutatanisha sana na cha kushangaza sana.Kifo cha mme wangu Kwakweli kimetikisa sana familia hadi nikaja kufikia hata kugombana na Ndugu wa mme kwamba Mimi Ndiye msababishi wa kifo cha baba Tito. Ndugu wengi kutoka kwa upande wa mme wake Kwakweli walinijia juu sana hadi kutaka kunipokonya Mali zangu zote kwamba wakidai Mimi Ndiye msababishi wa kifo. Lakini Mimi Nakumbuka kabisaaaaaaa siku Hiyo Kifo chake kinatokea.Asubuhi na mapema Baba Tito aliamka na kuchukua mswaki kisha akaenda hadi bafuni "Alihema kihemo cha kumaanisha yatakikana aende hatua kwa hatua kwa machungu aliyonayo moyoni mwake". fuuuuuuuuu,Haraka Haraka baada ya kuvaa nguo akawa ameniaga na akawa ameniambia hivi, ambapo Hayo ndiyo Kama maneno yake ya mwisho sikuwahi tena kuongea na mme wangu Ana kwa ana hadi leo hii Alisema" Mke wangu mimi naenda kazini kaa na Watoto vizuri kuna kazi kubwa Sana nimeipata hapo mkoani nikimaliza Kwakweli itakuwa ni furaha sana.ila Safari ni ndefu cha msingi wewe ishi na watoto vizuri, unaweza kushangaa nimepata hata nafasi ya kwenda kufanya kazi huko nje ya Nchi. Nachokuomba usiyumbishwe na Ndugu. Kwaheri".Hayo ndiyo maneno ambayo mme wangu aliniambia hadi leo nayakumbuka na sauti yake nikiyaongea haya maneno naisikia kabisaaaaaaa yanijia masikioni.mda huo Mimi nilikuwa bado niko kitandani.Baada ya kumaliza kuongea vile kisha akawa ameniaga na kuondoka na akawa ameenda kuwagongea Watoto na kuwaaga kisha anaondoka.
"Mda huo Benedetta akiwa amekaa Kwenye kochi naye amejaaliwa na nywele zake alivyozilaza mithili ya muamerika Kweli Kweli kumbe mazoea tu.Benedetta akasema Hivi". Kwahiyo Lakini haikuwa kawaida yake kwenda kazini kwa kuaga nyumba nzima?.
Hapana, hakuwa na tabia kama hiyo. Bali ni alikuwa ananiaga tu Mimi hapa na tayari anaondoka kurudi ni usikuuuuu.Lakini siku Hiyo ilipofika mishale ya saa saba mchana hivi alinitumia ujumbe unaosomeka hivi " Hujambo pamoja na familia hapo?."kisha Benedetta akawa ameshangaa kwelikweli na kumuuliza mama Tito hivi ".
Heeeeeeeeeeeeeeeeee kweli kabisa.
Ndiyo Hivyo Yaani.Sasa nikashangaa huyu baba Tito vipi Au kuna tatizo. Basi mimi nikaamua kumjibu tu Lakini hakuendelea tena kunitumia ujumbe. Mwisho wa siku inakuja kufika mishale ya saa nane Hivi napigiwa simu na mme wangu.Nikawa najiuliza huyu baba Tito leo Vipi?.Kwa kawaida yake simu yake alikuwa hawekagi namba za siri. Nikawa nimepokea Lakini nashangaa ni sauti nyingine kabisa. Wala si baba Tito tena.
" Benedetta akawa ameshangaa na kusema Hivi "yesu wangu Dada ikawaje kumbe ni sauti ya nani ilikuwa?.
Ilikuwa ni Sauti ya mfanyakazi mwenzake.Baba mtu huyo ananiambia kwamba fanya mpango uje Sasa hivi hapa round About ya kuelekea hospitali ya garisa mzee wako anataka aje aongee na wewe jambo Fulani Hivi la mkataba. Basi mimi nikawa najua kwamba yale maneno aliyokuwa akiniambia asubuhi basi yatakuwa ni Kweli. Kwahiyo ikanibidi nitoke Haraka Haraka pale kazini na kisha nikapanda pikipiki na kuelekea hapo round about ya kuelekea hospitali ya Garisa.
Daaaa pole Lakini Lakini wewe ulikuwa Unajua vingine kabisa.
Ndiyo Hivyo mdogo Wangu. Basi baada ya hapo nikawa nimefika pale Lakini kufika Pale nakutana na rafiki zake wa kazini wakiwa wanahudhunika Kwelikweli Lakini yule aliyenipigia sim ndiyo anakuja na kuanza kuniongelesha maneno mengine ambayo yatanifanya nisipanic.Lakini mwisho wa siku nawauliza mume Wangu yuko wapi ndipo wakaniambia panda gari twende zetu.Palikuwa na Gari tu za kazini kwao Kwahiyo tukawa tunaelekea Kweli huko hospitali ya Garisa.nashangaa geti linafunguliwa eti tunaingia hospitali.Haaaa wakawa wamepaki gari vizuri kisha tukashuka nashangaa wananipeleka mochwari.Haaa si Ndiyo ikabidi nisimame Sasa nakuanza kuwauliza vizuri Ndiyo Sasa wakaniambia kwamba mme wangu amefariki. Hapo hapo nilizimia mdogo wangu."Kwakweli mama Tito alianza tena kuyarudisha machozi ya miaka kama sita iliyopita ya kufiwa na mme wake mchana kweupe.Ndipo Sasa Benedetta akawa anambembeleza mama Tito akisema Hivi ".
Dada nyamaza tu yameshapita bana Hayo " Mama Tito akawa anaongea huku analia kwelikweli akisema Hivi ".
Ndiyo baadae wanakuja kuniambia Kwamba mume Wangu alianguka kutoka ghorofa ya kumi na Tisa hadi chini hapo hapo akawa amefariki.
Daaaa pole Sana Dada yangu "Sasa mda huo hapo ndani pakawa ni kilio tu si mama Tito wala Benedetta".
Basi ikiwa tayari ni miezi tisa kwa Zamda imeishafika basi kilichobaki tu ni mda wowote kwa Zamda kuweza kutoa nje kificha alichokuwa amekificha kwa mda wote huo.Basi mda huo ikiwa ni mishale ya saa saba usiku tayari Zamda Sasa maumivu yalikuwa yamemzidi kweli kweli. Hiyo basi inaashiria kwamba mda wowote tu anaweza kujifungua. Basi ndipo wakaamua kumpeleka katika hospitali ya karibu. Baada ya kufika hapo aliingizwa kwenye chumba hicho maalumu cha wanamama kujifungua. Kwakweli makelele aliyokuwa akiyapiga kwa uchungu aliokuwa akiuhisi si ya utani.Kama ni mwanamme Mwenye huruma atasema kwamba sitompa mke wangu mimba.
SEHEMU YA 10
Hospitali ambayo alikuwa amepelekwa Zamda ilikuwa ni hospitali inayoitwa Mazwei iliyopo mkoani Kimbu.Ni hospitali ambayo wahudumu wake Kwakweli ni wahudumu ambao wanafanya kazi kwa kujali kweli maisha ya mgonjwa kuliko kujipendelea wenyewe kwa wenyewe tu.Yaani mgonjwa akipelekwa katika hospitali ya Mazwei Kwakweli huduma atakayopatiwa hapo ni nzuri Sana.
Basi mda huo kijana Tito akiwa yuko amekaa Kwenye benchi la rangi nyeupe akiwa anawaza kwelikweli kwamba mke wake atatoka salama huko.Kwasababu si kwa makelele Hayo aliyokuwa akiyapiga.
Nakweli baada ya kupita kama saa Moja hivi Zamda akawa ameshajifungua Salama salimini. Mda huo Dada yake Tito Huyo Bite akawa anakuja Sasa kumtaarifu Tito.
"Mda huo Bite akiwa anaonekana anatoka katika mlango wa wanamama kujifungua akiwa anafurahi kwelikweli huku akiwa ameanza kuongelea mbali kabisa, akisema hivi".Titooo,hongera sana Tito, Sasa hivi na wewe unaitwa baba naniiii
" Tito akionekana ana furaha kweli kweli hadi akainuka sehemu aliyokuwa amekaa na Kuanza kusema hivi "Haaaa acha utani Bite,
Ndiyo ukweli huo,Sasa hivi wewe baba Mbona.Alaaaaa chezea nini.
Haya bana Mtoto gani.
Wa kike kitu jiko jiko chezea nini,
Alaaaaa wa kike
Ndiyo Hivyo wa kike.
Duuu haya bana.
Ikiwa ni mishale ya saa mbili asubuhi Zamda alikuwa amesharudishwa nyumbani. Wakiwa wanaonekana wako chumbani na Tito,mda huo Tito alikuwa kwelikweli akijishughulisha na vishughuli kwaajili ya kuweza kumsaidia Zamda. Kwasababu Zamda na mama mkwe wake kidogo kama vile hazipandi tangu siku ile Tito alivyomleta Zamda na kumtambulisha Zamda usiku ule.Lakini mda huo Walikuwa wana mazungumzo kidogo.
" Mda huo zamda akiwa anaonekana kavaa mavazi ya kumuonesha kwamba Yeye ni mzazi.Sehemu aliyokaa ni kitandani akiwa amemlaza mwanaye ambaye jina lake wameshampatia anaitwa Glady".ila daaa Tito kufanya mapenzi Raha sana ila njoo kwenye kujifungua, Yaani kama Jana usiku nilikuwa natamani Sijui Yaani nifanyeje tu.Kwasababu huo uchungu niliokuwa nikiuhisi laaaa si wa utani.
Aaaaaa pole sana Zamda.Me mwenyewe nimekaa pale nje Palikuwa pana baridi mda huo Ndiyo Nikawa nasikia hayo makelele huko ndani hadi nikawa Nasema daa Zamda simpi tena mimba.
Weeeeee utamu utarudi palepale tu siku si chache mbona.
Haya bana.
Tito umenileta hapa kwa madhumuni ya kuweza kukupatia mtoto. Sasa wa kwanza Ndiyo huyu hapa, wapili anafuatia baada ya huyu akishamaliza kunyonya tu.
Ahaaaaa haina shida, kwani si natoa tu Kisha nakupatia.
Haya bana.
Lakini siku hiyo Tito akiwa yuko mtaani na mchepuko wake hivi aitwaye Nunu.Walikuwa wana maongezi.
"Mda huo wakiwa wanaonekana wako chumbani kwa Huyo Nunu.Kwasababu naye Nunu amepangisha huwa anajishughulisha na shughuli ya ufundi cherehani.Hivyo Basi vimia mia anavyovipata huwa anajilipia kodi.Basi Nunu alikuwa na haya ya kuongea na Tito".sasa Tito ni mda basi na Mimi niwe nakaa nawewe Mara kwa Mara kwa mda wa usiku. Kwasababu tayari yule mke wako kwasasa Ana mtoto,hana lolote kwasasa embu njo kwangu bana.
Nunu ni Kweli yule kajifungua Lakini."Tito alivyosema Lakini tu Nunu akawa amemkatisha maneno na Kisha Nunu akawa anasema Hivi".
Lakini nini Tito huoni Mimi ndiyo mtamu kwasasa Jamani.Yaani natamani hata leo tu ungelala hata Hapa kwangu tu."Mda huo Nunu anamsogelea Tito huku akiwa anamuangalia Tito machoni ili hata Tito asiweze kujitetea kwa namna yoyote ile".
Kweli Nunu sikatai ila daaa inahitaji mda kwelikweli.
Yaani mda wa kufanya nini?.
Mda wa Mimi kuanza kutoka pale nyumbani na kumuacha mke wangu na kuja Kulala huku.
Kwahiyo Tito hivyo Unamaanisha dhahiri hunipendi.
Siyo kwamba sikupendi Nunu.
Bali ninini tatizo?.
Usiharakishe bana mbona mambo kawaida tu.
Lazima niharakishe na Mimi kwasasa nikufaidi Jamani Tito.
Haya Basi haina shida ntapanga ratiba Basi ili nisije nikajikoroga au nikagonganisha watu.
Hayo ndiyo Majibu sahihi bana.kwasasa inabidi nikupe na Mimi utamu wangu kwelikweli.
Amakweli vitabia tabia siku zote vinaweza kumuangusha mtu hata kazini.Tito Kwakweli alizidi kuwa na tabia ya kila msichana atakayemuona Mbele ya macho yake ni mzuri lazima amtongoze.Lakini mwisho wa siku akawa amefikia kutoka Kimapenzi na Mtoto wa Meneja mkuu.mwanadada huyo alikuwa ni mrembo kwelikweli ambaye aliweza kupata elimu yake ya kompyuta na hadi kuipatia shahada ya Kwanza ndipo baba yake kama Meneja akawa amempatia kazi Kwenye kampuni hiyo ya kichina inayojihusisha na Mambo ya ujenzi wa miundombinu.
Basi mwisho wa siku ikiwa tayari Tito amekaa kwenye mapenzi na huyo mtoto wa Meneja kwa jina alikuwa akiitwa Sophie. Kwahiyo walikaa kwenye mapenzi na Sophie kwa mda wa miezi sita hivi ndipo siri inakuja kufichuliwa hadharani kwamba Tito anatoka Kimapenzi na Sophie ambaye ni mwana wa Meneja mkuu.
Basi baada ya Meneja mkuu kusikia jambo Hilo akawa ameona kwamba huyu Tito ni kumfanyia jambo moja tu Ambalo litamfanya awe anaheshimu ofisi za Watu. Basi siku Hiyo Tito aliitwa na meneja mkuu Kwenye kikao cha dharura.Mda huo ikiwa inaonekana ni mishale ya saa nane na robo saa ya ukutani ya katika eneo walilokuwa wamekaa Ndivyo ilikuwa ikisema mda huo.
Katika meza wanaonekana yuko Meneja mkuu,Secretary wa ofisi na wafanyakazi wengine pamoja na Sophie.Mda huo Sophie yuko anaonekana amekaa karibu na baba yake ambaye Ndiyo Meneja mkuu na wengine pia wakawa wamekaa kwa Upande wa pili katikati palikuwa na meza kubwa hivi .Lakini hadi mda wa kikao hicho unafika hakuna aliyekuwa nini dhumuni la kikao. Yaani si Tito wala nani hamna aliyekuwa analijua Hilo swala Bali Meneja mkuu tu ndiye aliyekuwa akijua kwamba mada ya kikao ni nini. Basi mda huo tayari walioalikwa katika kikao kile wakawa wameshakaa wote na kukawa na utulivu kwa sekunde. Baada sekunde chache ambapo Meneja anaonekana ananong'onezana na secretary kwa sekunde chache kisha secretary akawa amesimama na kusema Hivi.
Habarini za mchana.
"Watu walijibu kwa furaha kwa kusema ".
Swalama kabisa.
Aaaaaa tunawaomba mtunuie radhi kwakuweza za kuwasumbua kidogo kwa kuweza kuitisha kikao cha dharura.Kikao hicho hakikutarajiwa kufanyika leo bali imebidi tu kifanyike leo leo na maamzi yatolewe leo leo.Basi sitakuwa na mengi ya kuongea bali namuachia nafasi hii Meneja mkuu ambaye Ndiye aliyeiitisha Kikao hiki.karibu Meneja."Wafanyakazi waliokuwa wamekaa pale wakawa wamempigia makofi secretary baada ya kumaliza kuongea na kisha secretary akawa amekaa na ikawa ni nafasi kwa Meneja mkuu kuweza kuongea".
Aaaaa poleni na kazi Jamani.
Shukrani Sana.
" Mda huo hapo mezani kwake anaonekana anafunua makatatasi mbalimnbali yakiwa yameandikwa.Akawa anasema Hivi ".Aaaaaaaa naimani kuwa kila mtu hapa atakuwa anashangazwa na kuitishwa kwa kikao hiki mda huu.Kwasababu si kawaida yetu.Ila kuna jambo limefikia kileleni linahitajika kufanyiwa ufumbuzi na kuweza kuleta matokeo ambayo ni mazuri kabisa. Aaaaa niseme tu Jamani dunia kwasasa inabadilika na sisi wanadamu inatakikana tubadilike na si kuwa tu kama tela siku zote Wewe unasubiria uvutwe tu Wakati unaweza kujiongoza.Aaaa mabadiliko ninayoyaongelea hapa ni katika masuala ya kielemu na kazi zetu.Kwasababu kuna maendeleo ya utandawazi kwelikwel ambayo yanaenda sanjari na Maendeleo ya sayansi na teknolojia. Sasa kama na sisi wanadamu hatubadilki kutokana na Maendeleo ya sanyansi na teknolojia Kwakweli itakwa ni vigumu sana hata kwa nchi yetu ya Kinani kuweza kuendelea. Hivyo sina haja ya kuongea sana mengi Bali kwanza nitambulishe mada itayokuwa mezani ni ipi.Mada ya Kwanza ni kusimamishwa kazi,Kupunguzwa mshahara na kuingizwa kwa wafanyakazi wapya na mengineyo."Baada ya Meneja mkuu kutaja hizo mada kwakweli kuna watu wakawa Tayari kidogo wameanza kukosa Raha Kabisa katika kikao kile.Meneja mkuu anasema Hivi".Tukianza na kusimamisha kazi.Hapa kama mwanzoni nilivyoanza kusema mapema kwamba Jamani kwasasa dunia nayo inazidi kuchange Kwahiyo hatuna budi na sisi kuweza kubadilika kutokana na Maendeleo ya sayansi na teknolojia. Hapa katika kusimamishwa kazi si kwa kosa lingine Bali ni kutokana na Kwamba kuna baadhi ya watu tuko hapa tunafanya kazi kutokana na udhoefu Bali ksa karne hii hamna Jambo kama Hilo.Dunia inavyobadilika na sisi tubadilike.Hivyo basi sitakuwa napoteza mda Sana katika kipengee kidogo sana Bali kwa hapa nitataja jina la mfanyakazi ambaye atasimamishwa kazi na kuanzia mda huo hatojulikana kama mfanyakazi wa Kwenye kampuni letu la ujenzi.Jina la Kwanza Kabisa ni "Mda huo kila mfanyakazi ambaye anajijua kwamba elimu yake ni hafifu Kwakweli wakaanza kukosa Raha na kujikuta vichwa chini tu wakiwa wanasubiria Majina yatajwe tu.".Tito Mwijange kabuti,"Tito alishtuka Kwelikweli kwa jina lake kutajwa Lakini Meneja akawa anaendelea kuongea tu".Huyu ni kijana ambaye kwa elimu yake ni ya kidato cha pili Wakati kuna watu wana Elimu za vyuo vikuu hapa wanahitaji Kazi. Kwahiyo kijana Tito baada ya kumalizika kwa kikao Hiki utaende Kwenye ofisi ya secretary akupatie barua za uthibitisho.Yote hii pia ni kutokana na cheo ambacho ulikuwa nacho hapa ni cheo ambacho hata hakifananii na maendeleo ya sasa.Utatunuia radhi sana kwa maamuzi yaliyofikiwa kwa ofisi.
Kwakweli jambo hilo likawa ni shitukizo sana kwa Tito.Ambapo kwa Mambo yalivyokuwa yanambana hali ndipo ilizidi kuwa Hatari kabisa.
Basi mwaka ukawa tayari umepita tangu Zamda kujifungua mwanaye wa kike huyo Glady.Maisha ya Kimbu tayari Zamda akawa ameshayazoea tu.Lakini kwa ujumla Zamda Yeye alikuwa ni mtu wa ndani tu mda wowote. Yaani ndani na yeyey na Yeye na ndani. Kwasababu nama Tito hakuwa anamruhusu Zamda Kutoka nje.Kwahiyo Zamda akabaki ndani tu akawa ni mtu wa kusema akiamka afue nguo za Tito, nguo za mwanaye,nguo za mama mkwe ,nguo za wadogo zake Tito ambao ni Soni na Shezi baada ya kumaliza kufua ndipo Sasa anaingia kudeki Nyumba nzima na ndipo kama ni uji au Chai ndipo atapika.Kwahiyo Yeye akishamaliza Mambo yote Hayo ndipo anaendelea tu kuangalia Runinga.
Lakini kipindi hicho Kwakweli huyo Tito majukumu yamemjaa kwelikweli hadi saa nyingine hakuwa anamletea chochote Zamda.Yote hiyo ni kutokana na Kwamba tangu Tito afukuzwe kazini kwakweli akawa Hana kazi maalumu ya kuweza kumuingizia kipato chochote.
Siku hiyo ikiwa ni mishale ya saa mbili usiku Tito na Zamda wanaonekana kama vile wakiwa katika mgogoro hivi.Ilikuwa Hivi.
"Mda huo Zamda akiwa amekaa kitandani na Mtoto wake akiwa anamnyonyesha huku anasema Hivi ".Hivi Tito mbona sikuelewi kwasasa nakuona unazidi kubadilika.kwanza unajua......Unajua wewe ni muongo Sana Tena sana.
Kwanini Zamda uongo gani huo.
Wewe Kipindi kile unasema ulifukuzwa kazi Kwasababu ya elimu tu Lakini kuna maneno nilikuja kuyasikia naninajua ni Kweli Kabisaaaaaaa.
Maneno gani uliyasikia Hayo na ni kwa nani?.
Wewe jua tu Hivyo wewe.Unasema ulifukuzwa kazi Kwasababu ya elimu yako ni ndogo kumbe kulikuwa na tatizo lingine nyuma yake.Yaani unafikia kunisaliti na hadi unatoka na mtoto wa Meneja Jamani.
Wewe nani kakuambia Hayo maneno ya mimi kutoka na meneja?.Wewe Kwani barua yangu siinaonesha hapa Kabisa au. Kwanza mbona Hayo mambo ni ya mda mrefu Hivyo. Yaani hadi leo bado unayaongelea tu.
Haaaaaaa Yaani nakwambia hilo gazeti lako lilikuwa linasomwa Pole pole huku linachambuliwa na likiwa linachambuliwa linaanza kutafutiwa Majibu na wenyewe waliopo Jikoni. Poa tu Kwa kunisaliti Hivyo.
Hivi wewe Zamda Yaani Mimi nataka Kwanza nijue tu nani aliyekuambia Mambo Hayo.Kwanza wewe Kwanini unapenda kusikiliza maneno ya watu Hivyo Zamda.
Ndiyo Hivyo wewe jua hamna siri katika chini ya jua.
Kwakweli ni mgogoro mkubwa sana ambao ulikuwa hapo.Kwasababu taarifa hizo kwa mara ya kwanza zilikuwa zimemfikia mama Tito.Ambapo mama Tito anarafiki yake ambaye naye wana undugu na Meneja mkuu Kwahiyo Ndiye ambaye amemwambia mama Tito siri yote na siku hiyo Zamda alikuwepo ndani anasikiliza tu mama Tito akijua Zamda amelala.
Mwl Maeda