08-14-2021, 08:33 AM
KISWAHILI NI BAHARI.
**************************
N'shatamburikiwa kuwa, ni bahari Kiswahili,
Lahaja ze maridhawa, pia chaenea mbali.
Kila leo kinakuwa, kipo fasi mbalimbali,
kina dhima duniani, ni moja ya lugha kuu.
Kiswahili ni bahari, mawimbi ye yenda kasi,
kwa mwenendo wa ushwari, kimefika nyingi fasi.
Ulimi huu fahari, ya kasikazi na kusi,
magharibi mashariki, kote kimeshakuwanda.
Kwendelea sintoweza, miye nali mwanagenzi,
bado wa kubangaiza, dogo kati ya watunzi.
Nikichuchuka n'taweza, tengeneza nyingi tenzi,
usin'one leo kinda, kesho nitapaa mbali.
Insha'Allah.
__________
Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda.

Mwl Maeda