MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

HADITHI YA SIMBA NA SUNGURA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
HADITHI YA SIMBA NA SUNGURA
#1
HADITHI YA SIMBA NA SUNGURA
Hadithi……hadithi…….
Hapo zamani za kale, palitokea Simba mwenye njaa, katika pitapita zake za kuwinda, alimkuta Sungura akiwa amelala fofofo. Alishusha pumzi, akatabasamu na kumshukuru sana Mungu kwa ukarimu wake wa kutambua taabiko lake na kumtunuku chakula pasi na haja ya kukitolea jasho. Taratibu alimsogelea Sungura ili asije akamwamsha, akalala yeye…Alipoinua miguu yake kutaka kumkamata, mara akatokea Ayala mnono ambaye alipita akikimbia karibu naye, akielekea upande wa kaskazini kwenye uwanda wa nyasi fupi. Simba alimwacha Sungura na akakurupuka kumkimbiza yule Ayala. Vishindo kelele na purukushani za Simba na Ayala vilimgutusha na kumwamsha Sungura ambaye aliamka na kutimua mbio kuelekea upande wa kusini. Baada ya kumkimbiza Ayala kwa muda mrefu Simba alishindwa na kuamua kurudi ili akamle yule Sungura. Alipogundua kuwa Sungura naye alikuwa ameamka na kukimbia, Simba alisema kwa kujilaumu, “ama kweli nimepata nilichostahili; kwa kuwa nilikiacha chakula nilichokitia mkononi tayari kwa tamaa ya kutaka kupata zaidi.”
Hadithi hii inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)