MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

HADITHI YA MBWEHA NA PAKA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
HADITHI YA MBWEHA NA PAKA
#1
HADITHI YA MBWEHA NA PAKA
Mbweha alikuwa akijigamba mbele ya Paka kuwa yeye ana mbinu nyingi sana za kuwakwepa maadui zake. “Nina fuko zima la mbinu na ujanja,” alisema, “ambalo lina mamia ya njia za kujiepusha na maadui zangu wakati wa hatari.” “Mimi ninayo mbinu moja tu,” alisema Paka; “lakini ninaiamini, na inanifaa hiyo hiyo.” Wakiongea maneno hayo, punde wakasikia sauti za Mbwa wawindaji zikielekea upande wao, na Paka alichupa akauparamia mti haraka na kujificha juu kwenye matawi. “Hii ndiyo mbinu yangu,” alisema Paka. “Je mwenzangu wafanyaje?” Mbweha akafikiri kwanza kutumia njia hii, mara njia ile, na kabla hajafanya maamuzi, Mbwa walimkaribia na kumkaribia, na mwishowe Mbweha akiwa katika mkanganyiko huo, alikamatwa na kuuawa na Wawindaji. Paka ambaye alikuwa akishuhudia kinachotokea, alisema; “Heri njia moja salama kuliko njia mia ambazo huwezi kuzitumia.”
 
Hadithi hii inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)