MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
FANI NA MAUDHUI YA HADITHI FUPI ZA KISWAHILI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
FANI NA MAUDHUI YA HADITHI FUPI ZA KISWAHILI
#1
Sura ya Tatu
KANUNI kubwa ya kuipima kazi ya sanaa na fasihi kwa ujumla ni kuangalia uwiano uliopo kati ya fani na maudhui katika kazi inayohusika. Kanuni hii ndiyo uti wa mgongo na roho ya kazi ya sanaa, hususan hadithi fupi ya Kiswahili.
Suala la fani na maudhui katika fasihi ni pana na limeleta utata mwingi miongoni mwa wanataaluma mbalimbali. Kwa sababu hii, ni muhinu kupambanua vipengele hivyo vya kisanaa. Katika sura hii tutajaribu kueleza maana ya fani na maudhui katika ngazi tatu. Kwanza tutajadili maana ya fani kama inavyoelezwa na wanataaluma ama wanafasihi mbalimbali. Pili tutaangalia maana ya maudhui kama inavyoelezwa pia na wanataaluma hao. Tatu, tutaona uhusiano na uwiano ulioko kati ya fani na maudhui katika kazi ya sanaa. Mwisho tutaangalia kwa kifupi wapi waandishi wa hadithi hizo wanaweza kuchota dhamira na aina za dhamira hizo.
Maana ya Fani
Cleanth Brooks na Robert Penn Warren wanaelezea maana ya fani kuwa ni “vipengele mbalimbali katika kazi ya fasihi. Ni jinsi kazi hiyo inavyojengwa ili kuipata maana yake.”1 Halafu wanaendelea kusisitiza kuwa “vitu hivyo ni lazima vihusiane vyenyewe, na pia vihusiane na kile kinachosemwa ili kujenga kazi bora na yenye kuleta maana ya kifasihi.”2 Babette Deutsch naye anaelekea kukubaliana na wazo hilo anaposema, fani ya ushairi ni “mpangilio wa mizani, beti…”3 n.k.
Akijadili maana hiyohiyo ya fani, Walter Blair na wenzake anasema kuwa, “katika fasihi, fani ina maana ya tawi ama aina ya kazi ya sanaa inayohusika.”4 Halafu anaendelea kutoa mifano ya matawi au aina yake kama vile hadithi, ushairi, na tamthiliya. Hii ni maana ya kwanza anayoitoa mwanafasihi huyo. Maana yake ya pili anayoitoa ni ile inayohusu mpangilio au umbo la kazi ya sanaa. “Ni jinsi kazi ya fasihi ilivyojengwa, bila ya kujali maudhui yake.”5
Dhana hii ya pili anayoitoa Blair na wenzake inatenganisha fani na maudhui ya kazi ya sanaa. Jambo hili lina dosari kwa sababu sivyo ilivyo katika kazi za sanaa za kifasihi. Kimsingi, fani na maudhui ni vitu ambavyo vinatazamwa katika umoja na wala haviwezi kutenganishwa. Swala hili tutalijadili baadaye.
Kwa upande mwmgine, maelezo yaliyotolewa hapa juu yanatupa dhana mbili. Kwanza, kuna wazo linaloieleza maana ya fani kwa dhana ya tawi na pili, kwa dhana ya umbo.
Dhana ya umbo inahusu uwezo wa msanii wa kusanifu kazi yake, yaani kuunganisha vipengele mbalimbali vinavyoijenga kazi ya kisanaa anayoishughu-likia.
Katika ushairi kwa mfano, fani ya ushairi huo itakuwa imepimwa kwa kuangaliwa vipengele vyake kama vile miundo, mtindo, lugha, wahusika n.k.
Katika tamthiliya, licha ya kuangalia vipengele vilivyotajwa hapojuu, vitu kama mandhari, wahusika, vifaa, lugha n.k. vitaangaliwa kama vipengele muhimu vya fani ambavyo katika ujumla wake, vitatoa maana ya kazi nzima.
Kwa upande wa hadithi, fani yake itajumuisha mambo kama vile wahusika walivyojengwa, lugha ilivyotumika, mandhari, muundo na mtindo, n.k., na Batimaye jinsi vipengele hivyo vinavyoleta na kuathiri maana ya kazi nzima.
Dhana nymgine ya fani m ile ya tawi ama utanzu. C. Hugh Holmann6 anasema kuwa utanzu ni istilahi inayosimamia aina ya kazi ya kisanaa kufuatana na umbo ama fani yake, yaani kufuatana na mbinu za uumbi ama ujenzi wake. Ziko namna mbalimbali za kugawanya tanzu hizo. Kwa mfano, katika fasihi simulizi na fasihi andishi tuna tanzu kama vile ushairi, hadithi na tamthiliya. Lakini pia katika tanzu hizo tunaweza kupata matawi mengine yanayogawanywa kwa kutumia misingi maalumu na ambayo bado yataitwa tanzu. Matawi hayo, kwa mfano, katika hadithi tuna riwaya (hadithi ndefu) na hadithi fupi. Katika ushairi tuna tanzu ama matawi mengineyo kama tarbia, tathlitha n.k. Na katika sanaa za maonyesho tuna tamthiliya, vichekesho, n.k. Pengine tanzu hizo zinaweza kugawanywa kidhamira.
Mgawanyo wa kitanzu una maana kuwa kuna makundi ya kazi za sanaa zenye sifa maalumu katika aina moja ya utanzu, k.v. ushairi, au aina mbalimbali ya kazi za sanaa k.v. ushairi na tamthiliya, na mbinu za ujenzi wake bila kujali wakati na mahali pa uandishi wake, dhamira n.k. na kwamba vipengele hivyo vya kifani ni vya msingi katika kuainisha kazi ya sanaa inayohusika. Tanzu za kifasihi, kwa mujibu wa Rene Wellek na Austin Warren zinabadilika kufuatana na kazi mbalimbali za kifasihi zinazoandikwa.
Tukizingatia maelezo ya fani ya awali na fani ya pili tunaona kuna haja ya kuzipambanua vyema istilahi hizo ili kuondoa utata wa matumizi uliopo miongoni mwa wanafasihi.
Kutokana na hoja hiyo, tutatumia istilahi ya FANI kwa maana ya UMBO la kazi ya sanaa ya kifasihi. Dhana ya pili ambayo inahusu TAWI la kazi ya sanaa tutatumia istilahi ya UTANZU.
Maana ya Maudhui
Kwa upande wa maudhui imekuwepo mikinzani na mikanganyiko nuongoni mwa wanataaluma wa kazi za fasihi juu ya maana yake. Wengi wa wananadharia hao wanajadili fani na maudhui pamoja, japo pengine mitazamo yao haiwi sahihi.
Baadhi ya wanataaluma wa kazi za fasihi wanasema kwamba fani na maudhui ni vipengele ambavyo havina uhusiano wowote na kwamba vinaweza vikatenganishwa. F.V. Nkwera7 analinganisha fani na maudhui na kikombe na maji. Kikombe kinachukuliwa kama ndiyo fani, na upande mwingine maji ndiyo maudhui. Mnywaji wa maji hayo analinganishwa na msomaji wa kazi ya fasihi.
S.D.Kiango na T.S.Y.Sengo8 wanafafanua fani na maudhui kwa kulinganishwa na chungwa ambalo lina sehemu ya nje na ndani. Maudhui ya kazi ya sanaa yanalinganishwa na nyamanyama za chungwa na fani ni ile sehemu ya nje.
Mawazo mengine juu ya fani na maudhui yanatolewa na Penina Muhando na Ndyanao Balisidya ambao wanaelekea nao kuukubali mtazamo huu ulioelezwa hapo juu wakati wanapoelezea hadithi kuwa na “umbo la nje” wakati lugha inapotumiwa na kujenga hilo umbo la ndani (maudhui) ambalo huhusika na wazo kuu analolitaka fanani, (dhamira) ujumbe wake, maadili, na falsafa zake (kama zipo) za maisha.”9
Nadharia hizo zote zilizojadiliwa hapo juu kwa ujumla zinaonyesha kupwaya na zinaweza kuwakanganya wasomaji. Nadharia hizo hazionyeshi ama kuwakilisha ukweli wa mambo ulivyt) juu ya uwiano uliopo kati ya fani na maudhui katika kazi ya sanaa kwani zinaonyesha kuwa fani na maudhui ni vitu viwili vinavyoweza kutazamwa katika utengano, jambo ambalo si la kweli. Ukweli ni kwamba vitu hivi viwili vinategemeana na kukamilishana, na wala havitazamwi katika utengano.
Ufafanuzi wa kuiona fani na maudhui kama kitu kisichoweza kutenganishwa umefanywa na Henri Arvon10, Avner Zis11 na wanataaluma wengine wengi walio na mtazamo wa kisayansi ama kiyakinifu.
Kwa upande wa fasihi ya Kiswahili, M.M. Mulokozi na K.K. Kahigi wamekuwa na mtazamo wa aina hiyo pia. Wanafasihi hao wanasisitiza kuwa “fani na maudhui huathiriana na kutegemeana … Maudbui ni maana ya shairi (kazi ya sanaa), ni yale mawazo yanayozungumzwa (dhamira, falsafa, maoni), pamoja na mtazamo wa mtunzi juu ya mawazo hayo… wazo kuu (dhamira) na mtazamo wa msanii hutupa ujumbe.”12
Akiungana na mtazamo huu, Senkoro naye anasema kuwa “maudhui ni jumla ya mawazo, mafunzo yapatikanayo katika kazi ya fasihi… Maudhui huunda lengo kwa mwaudishi. Kutokana na lengo, mawazo na mafunzo ya mwandishi ndipo tunapata falsafa. Mawazo, mafunzo, lengo na falsafa au mtazamo wa mwandishi kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii huunda msimamo.”13
Mawazo hayo aghalabu yanajaribu kufafanua nini hasa ni maudhui. Lakini dhana ya kutotenganishwa kwa vitu hivi viwili haijawekwa waziwazi. Ndipo Senkoro anapotumia mfano wa “sarafu” kwa kufananisha fani na maudhui ya kazi ya sanaa na “sura mbili za sarafu moja.”14 Mfano huu unajaribu kusisitiza dhana ya kutotenganishwa kwa fani na maudhui katika kazi za sanaa za kifasihi. Mfano huu wa sarafu unajaribu kuonyesha dhana ya ukamilifu ya fani na maudhui kama kitu kimoja cha kazi ya sanaa kwa kutumia mfano wa sarafu yenye sura mbili, lakini umuhimu wake kama sarafu moja unategemea tuweko kwa sura hizo mbili. Sura moja ya sarafu ikikosekana, basi, sarafu hiyo haiwezi kuwa na hadhi yake ya kisarafu. Jambo la muhimu ni kuona jinsi kitu kimoja (fani) kinavyoweza kukikamilisha kingine (maudhui).
Kwa kuzingatia nadharia hizo, tunakubaliana na Senkoro15 au Mulokozi na Kahigi16 wanaosema kuwa “fani na maudhui huwiana, hutegemeana na hatimaye kuathiriana.” Uhusiano huu ndio unaojenga kazi bora ya fasihi. Aidha ni vizuri kutoa tahadhari hapa kuwa uwiano wa fani na maudhui wa kazi ya sanaa huwa ni lengo la msanii. Maudhui iliyotawala kuumbwa kwa kazi ya sanaa inatakiwa kujitokeza katika fani inayohusu. Ili maudhui yatawale fani, sharti yajitokeze kama kazi ya sanaa na si kama hotuba ya mwanasiasa. Ni wajibu wa msanii kuchagua fani inayomruhusu kutumia maudhui anayotaka kuyafikisha kwa hadhira yake.
Uhusiano wa Fani na Maudhui
Mwandishi wa hadithi fupi anatakiwa autazame uhusiano huu muhimu uliojadiliwa hapa kwa makini sana. Kama hatakuwa mwangalifu anaweza kujikuta katika hali ya utata wakati wa uandishi wake.
Tatizo kubwa linalowakabili waandishi wengi wa hadithi fupi na fasihi kwa ujumla ni lile la kipi kipewe uzito wa kwanza katika uandishi. Wasanii wenyewe wanagawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna ambao wanaian-galiajanui kama kitu kinachobadilika kulingana na mfumo wa kihistoria kwa wakati na mahali maalumu na kuna wale wanaoona kuwa kila jambo linalotendeka katikajamii ni kudra ya Mwenyezi Mungu. Yawezekana kuna wasanii wenye mtazamo ulio nje na hii tuliyoitaja. Kisanaa, wako wale wanaoona kazi ya sanaa kama chombo maalumu kinachobeba maudhui muhimu kwa ajili ya jamii na kuna wate wanaoiona kazi ya jamii ya sanaa ikiwa na kazi ya kufurahisha ambayo haipaswi kuambatana na itikadi ama mfumo wowote ule wa maisha ya jamii. Sanaa, walidai wataalamu hao isihusighwe na maisha bali itazamwe kama sanaa tu.
Tukianza na mtazamo tulioutaja kwanza tutaona msisitizo huwekwa kwenye maudhui (maana) ya kazi ya sanaa. Lakini fani pia hawajaiacha katika mtazamo huo. Wanataaluma hao huiona fani kuwa inategemeana na maudhui katika sanaa nzima. A. Lunarchasky, mwanafasihi mwenye mtazamo wa kiyakinifu anasema:
Quote:Mhakiki (msanii) wa Ki-Marx atachukua kwanza maudhui (maana) kama ndilo lengo la uhakiki (usanii) wake. Atatafuta uhusiano wake na jamii, pia atazingatia matokeo ya kazi yake katika jamii hiyo. Baada ya hapo atarudi kwenye fani na kuona imetosheleza vipi lengo lake la kuieleza kazi hiyo na kuvutia wasomaji17
Tunaweza kuifikiria kauli hii kwa kuihusisha na hadithi fupi ya Kiswahili. Mwandishi wa hadithi fupi akitaka kazi yake iwe na manufaa kwa jamii anayoiandikia lazima awe mwangalifu Katika kuchagua dhamira zile ambazo zinafundisha na kujenga msimamo wa kimaendeleo katika kuikwamua jamii kutoka katika minyororo ya utumwa na ukandamizwaji. Itabidi msanii huyo afanye utafiti juu ya matakwa na mategemeo ya jamii yake. Dhamira hizo lazima zielezwe kifundi ili kufanya watu wapende kusoma kazi za sanaa hizo. Kama kazi ya sanaa itakuwa na fani duni lakini maudhui yake ni mazuri, basi, hata maudhui yaliyokusudiwa hayatatoa ujumbe unaokusudiwa inavyopasa. Au ikitokea maudhui ni duni na fani ni bora, pia jamii itapata hasara ya kufikiwa na maudhui yasiyo na maana katika jamii hiyo kwa kupitia fani iliyo bora. Wana-Marx walilazimika kurekebisha mtazamo wao wa kutoa uzito kwa maudhui peke yake kwa sababu iligundulika kuwa maudhui hayawafikii wasomaji bila kutumia kiungo cha fani.
Mtazamo mwingine tulioutaja hapa juu ni ule unaoiona sanaa kama kitu cha kufurahisha tu. Mtazamo huu kimsingi hujali sana fani zaidi kuliko maudhui. Maudhui kwao sio kitu cha muhimu sana, kwa hiyo wasanii wa aina hii hujali na kuchunguza maneno, jinsi yanavyofanya kazi yakiwa katika msisitizo, urefu wa msitari (kama ni ushairi) na kadhalika. T.S.Eliot na Allan Poe ni kati ya wanataaluma waliosisitiza mtazamo huu. Jambo la muhimu kutamka hapa ni kuwa mazingira ni muhimu katika kufanya uamuzi huu. Katika itikadi nyingine mtazamo kama wa Eliot na Poe ni sahihi lakini kwa itikadi ya kimaendeleo ionayo fasihi kama chombo muhimu kinachohitajika katika kusaidia jamii katika mapambano yake, mtazamo huu si sahihi. Lile linalosemwa haliko katika fani, bali fani ni njia ya kusemea. Kwa hali hii, suala la wasanii pia kuwa na msimamo fulani linafuata udhamini na itikadi inayotawala na kutetea maslahi maalumu. Kwa vyovyote, msanii hawezi kusaliti tabaka linalomlea na kumtunza. Ni wasanii wachache wanaweza kukemea utawala wao kama unawasaliti umma wa wakulima na wafanyakazi. Nao wakifanya hivyo, wana- jikuta katika matatizo makubwa kama tulivyokwisha ona hapo mapema katika sura iliyotangulia.
Ikiwa mwandishi wa hadithi fupi atajali “maneno” tu kama mtazamo huu unavyodai, itakuwa ameshindwa kabisa kuijengajamii yake. Atakuwa ameian-gusha fasihi na kufanya ishindwe kufanya kazi yake. Kwa kuzingatia hali halisi, mtazamo sahihi utakuwa ule unaoihusisha kazi ya sanaa ya fasihi na maisha ya jamii ambayo imeandikiwa kazi ya fasihi inayohusika. Maisha ya jamii yana matatizo na furaha. Mtazamo sahihi utakuwa unawahudumia watu kwa kadiri inavyowezekana. Mwandishi wa hadithi fupi anategemewa awe na mtazamo wa kisayansi wa aina hii kwa janui yake. Ni juu ya mwandishi wa hadithi fupi kuwa mwangalifu wakati wa usanii wake kama atataka kazi. yake iwafae kwa kiwango cha kuridhisha umma wa wakulima na wafanyakazi. Uhusiano muhimu juu ya vipengele vinavyoijenga hadithi fupi umeonyeshwa katika Kielelezo Na. 2.
[Image: p036.gif]
Kielelezo 2: Vipengele vya Fani na Maudhui ya Kazi ya Fasihi (Hadithi Fupi)
Kielelezo hiki kimezingatia ukweli na msimamo kuwa maudhui kama kile kinachosemwa ndicho kitu muhimu katika kazi ya sanaa ya kifasihi. Kitu hiki muhimu kinasaidiwa na fani kuwafikia wanaohusika inavyopasa. Aidha, msi- mamo huu kimsingi unatofautiana, na ule unaothamini fani tu katika kazi ya sanaa ya kifasihi. Suala la kuzingatia ni mazingira ya uandishi na mtazamo wa jamii inayoandikiwa. Mwandishi anaandika nim na wapi? Anamwandikia nani na kwa lengo gani? Hali hii itamsaidia kuamua jinsi au njia ya kuwasilisha alilonalo kwa hadhira aliyoikusudia.
Chimbuko la Dhamira
Baada ya kuangalia maana ya fani na maudhui, na kuona uhusiano na uwiano kati ya fani na maudhui, tuangalie sasa wapi waandishi wa kazi za hadithi za kifasihi, hususan hadithi fupi, hupata dhamira zao. Katika mjadala wetu, tutajaribu kuangalia pia jinsi dhamira inavyoweza kuunganika na fani katika kutoa maudhui kwa hadhira iliyokusudiwa.
Dhamira m mawazo yanayoelezwa katika kazi ya sanaa Ziko dhamira za aina nyingi ambazo mwandishi anaweza kuchagua.
Wakati mwingine, waandishi wanaweza kuwa katika mazingira yaleyale, na wakaandikajuu yajambo moja, labda la mapenzi. Kwa vile watu hawa wanayatazama mambo tofauti, maelezo yao yanaweza. kutofautiana. Tunaweza kujadili hoja hiyo’kwa kutoa mifano tuliyo nayo katika kitabu hiki.
Katika sehemu ya pili ya kitabu hiki, kuna hadithi kadhaa ambazo zinajadili dhamira mbalimbali. Miongoni mwa dhamira zinazojadiliwa sana ni siasa, mapenzi na utamaduni kwa ujumla.
Tunaweza kuanza na dhamira ya siasa katika kujadili suala hili. Tunapenda kujadili suala hili kwa kutumia hadithi mbili: Siri ya Bwanyenye (M.M.Mulokozi) * na Cha Mnyonge Utakitapika Hadharani (E. Kezilahabi).
Quote:* Hadithi zote zinazojadiliwa kama mifano ziko katika sehemu ya pili ya kitabu hiki.
Hadithi ya Siri ya Bwanyenye kimsingi inajadili masuala mengi yanayoihusu jaimii ya Tanzania ya wakati. wa TANU na nchi zinazoweza kuwa na mazingira ya aina hii. Mwandishi ametumia mazingira aliyomo, na wakati uliopo katika kuandika badithi yake. Kuna masuala ya watu kushangilia “Azimio la Arusha” kwa unafiki – kwamba watu wengine wamekuwa wakiimba uzuri wa “Azimio la Arusha,” wakati huo huo wanalisaliti. Kwa hiyo mambo kama uongozi bora, haki, uhuru wa kweli na kadhalika, yanajadiliwa kwa mapana.
Suala la kisiasa linavyojitokeza katika Cha Mnyonge Utakitapike Hadharani linatofautiana na Siri ya Bwanyenye. Wakati Siri ya Bwanyenye hazungumzii matatizo ya utabaka moja kwa moja, Cha Mnyonye Utakitapika Hadharani analiweka suala hili wazi zaidi anapotenga watu katika “bwana,” “ukubwa” ama “uwezo” na “unyonge”, “umaskini” na kadhalika. Si hilo tu, mwandishi wa hadithi ya Cha Mnyonge Utakitapika Hadharani ametu-mia mapenzi kama kitu cha kubebea dhamira kuu ya utabaka. Hayo ni baadhi tu ya maoni yanayojitokeza kwa upande wa siasa katika hadithi hizo mbili. Japokuwa hadithi hizo ni za kisiasa, na ingawa wote wameandikia katika mazingira wanamoishi, kuna utofauti uliojionyesha tayari.
Kwa upande wa dhamira ya mapenzi, tutazigusia hadithi za Kiumbe Mzito (M.Msokile), Kijana Yule (M.Mohamed) na Ndumila Kuwili (J. Rutayisingwa).
Ukiangalia kijuujuu, hadithi ya Kiumbe Mzito ni ya mapenzi. Lakini ikichunguzwa kwa undani sana, hadithi hii imetumia dhamira ya mapenzi katika kuelezea mambo mengine zaidi ya kijamii. Suala linalojadiiwa sana linahusu elimu ya malezi kwa vijana hasa wasichana – na matatizo yanayowapata wasichana wanaosoma shule za mijini, hususan Dar es Salaam.
Kwa upande mwingine, haditbi ya Kijana Yule nayo inahusu mapenzi pia. Lakini mwandishi alivyoyajenga mapenzi katika hadithi hiyo, ni tofauti na ilivyo katika Kiumhe Mzito Mapenzi ya Kijana Yule ni mazito, yanawahusu wanawake wasio na matarajio ya Kusoma shule kama katika Kiumbe Mzito. Tamaa ya wanawake wa Kijana Yvle ni kukidhi matakwa ya mapenzi yao, lakini katika Kiumbe Mzito, mwandishi anawasawiri wasichana wenye pupa ya kukidhi kiu yao ya pesa kwa kutumia mapenzi. Ni vipofu wanaotazama!
Ndumila Kuwili inatuonyeeha upande wa pili wa mapenzi. Hadithi hii inaelezea maisha ya ndoa yaliyokosa uaminifu na hasara ya kukosa jambo hilo. Si hilo tu, hadithi inaonyesha pia nafasi ya uaminifu katika kulinda unyumba na hata marafiki na ujirani mwema. Pamoja na mapenzi, masuala ya chuki, haki na uonezi yanajitokeza pia.
Dhamira zote hizi zimetokana na mzingira wanayoyaishi waandishi hao kila siku. Lakini je, kwa nini dhamira hizo zimeelezwa kwa viini vinavyoto-fautiana kati ya mwandishi na mwandishi? Kwa nini mapenzi yameelezwa tofauti miongoni mwao? Kwa nini suaia la siasa nalo limepewa uzito tofauti kati ya waandishi wanaohusika?
Maswali haya yanajibika kwa kuzingatia msimamo wa mwandishi, mtazamo, falsafa na uwezo wa jumla wa kisaaaa alionao msanii anayehusika.
Falsafa, Mtasamo, na Msimamo waa Mwandishi
Katika kazi yoyote ya kifasihi mambo hayo lazima yawepo. Aidha, kila msanii ana nafasi na uwezo wake katilca kuyakabili na kuyawasiIisha katika mazingira yanayohusika. Tutavijadili vipengele hivyo kimoja kimoja hapa chini.
Pengine tuanze na dhana ya mtazamo kwa msanii m nini? Kimsingi, tunasema kuwa mtazamo m jinsi ya kuona mambo katika maisha. Tunaweza pia kusema kuwa kila mtu ana namna najinsi ya kuyatazama mambo yanay-omzunguka katika maisha yake.
Wasanii wana mitazamo au maono ya aina mbili. Kwanza, huutazama ulimwengu au mazingira yanayomzunguka binadamu kiyakinifu – kisayansi. Msanii wa aina h» huuona ulimwengu kuwa ni kitu kinachobadilika kufu-atana na mfumo wa kihistoria. Mtazamo huu humfanya msanii kuutazama ulimwengu kama kitu dhahiri – kitu katika uhalisia wake.
Kinyume cha mtazamo huu, kuna mtazamo wa kidhanifu. Mtazamo huu huuchukulia ulimwengu kama kitu kinachobadilika kulingana na matakwa ya Mungu. Msanii mwenye mtazamo huu, atauwasilisha hivyo katika kazi yake ya sanaa.
Vilevile falsafa inahusiana sana na mtazamo. Kwa mujibu wa kamusi ya Kiingereza ya Concise Gxford Dictionary, falsafa imeelezwa kuwa “ni busara au elimu inayoshughulikia ukweli – chanzo cha jumla cha mambo na mawazo, welewa wa binadamu na maisha. (Falsafa) m msingi muhimu wa maisha.”18
Kwa kuzingatia kauli hii, falsafa ya kazi ya kifasihi inatakiwa ichambuliwe kwa kuzingatia jinsi kazi hiyo ilivyoutazama ulimwengu unayoihusu. na kuueleza ukweli juu ya mambo mbalimbali. Ukweli huo lazima uhusishwe na binadamu. Kwa hiyo falsafa ya kazi ya kifasihi inahusiana na mtazamo, na uyakinifu au udhanifu huunda falsafa.
Mtazamo na falsafa ni vitu vya msingi katika kujenga msimamo wa msanii. Msimamo wa msanii ndio unaosababisha kazi ya sanaa iwe na mwelekeo maalumu na hata kutofautiana na kazi za wasanii wengine.
Katika fasihi ya Kiswahili kwa mfano, kuwa baadhi ya wasanii wanaosema kuwa ushairi lazima uwe na kanuni ya vina, mizani, mistari, na kadhalika. Huu ni msimamo wao, na wako katika kutokubaliana na wale wanaosema vitu hivi si vya lazima kama yalivyo maudhui.
Katika kusoma kazi hizo, mtu anaweza kupata ujumbe, maadili, mafunzo na kadhalika, kwa kuzingatia mtazamo, msimamo na falsafa.
Aidha, msanii huwajenga wahusika kwa kuwapa lugha na tabia zinazolingana na dhamira zinazoelozwa. Lugha mara zote ni kiungo muhimu katika kutoa maudhui yanayostahili kwai hadhira iliyokusudiwa.
Tunahitimisha hapa kwa kusema kuwa maudhui ya kazi ya sanaa ya kifasihi, lazima yajumuishe dhamira zinazoelezwa, msimamo, matazamo falsafa, ujumbe, maadili na kadhalika.
Maelezo
1. C- Brooks na R.P. Warren, Understanding Fiction, F.S. Crofts & Co., Inc. 1943.
2. Kama Na. 1.
3. B. Deutsch, Poetry Handbook, Jonathan Cape, Thirty Bedford Square, 1965.
4. W. Blair (na wenzake), Literature, Scott, Foresman and Company, New York: 1966.
5. C.H. Holman, A Handbook to Literature, The Odysey Press, New York, 1936.
6. R. Wellek na A. Warren, Theory of Literature, A Harvest/HBJ Book London 1975.
7. F-V. Nkwera, Sarufi na Fasihi: Vyuo na Sekondari, TPH, 1978
8. S.D- Kiango na T.S.Y. Sengo, Hisi Zetu – I . TUKI, 1973.
9. P. Muhando na N. Balisidya, Fasihi na Sanaa za Maonyesho, TPH, 1976
10. H. Arvon, Marxist Aesthetics Cornell University Pres, 1973.
11. A. Zis, Foundations of Marxist Aesthetics, Progress Publishers, Moscow, 1977.
12. M.Mulokozi, na K-K- Kahigi, Kunya. za Ushairi na Diwani Yetu”, TPH, Dar es Salaam: 1979.
13. F.E.M.K Senkoro, Fasihi, Press and Publicity Centre, Dares Salaam: 1979.
14 Kama Na. 18.
15. Kama Na. 13.
16. Kama Na. 12.
17. A. Lunacharsky, On Literature and Art, Progress Publishers, Moscow, 1973.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)