08-01-2021, 08:41 PM
DHANA YA NAHAU
Nahau ni msemo uliojengwa kwa kutumia maneno ya kawaida lakini ambayo huwa inasetiri maana tofauti na ile iliyobebwa na maneno hayo hayo iliyo katika matumizi ya kawaida. Nahau aghalabu hutumia lugha ya picha kutoa maana iliyokinyume.
Mifano :
Toa maana ya nahau hizi :
Nahau ni msemo uliojengwa kwa kutumia maneno ya kawaida lakini ambayo huwa inasetiri maana tofauti na ile iliyobebwa na maneno hayo hayo iliyo katika matumizi ya kawaida. Nahau aghalabu hutumia lugha ya picha kutoa maana iliyokinyume.
Mifano :
- Ana jicho la nje−asherati
- Yeye ni jamvi la wageni−mwasherati
- Yeye ni bao la mkahawani=kahaba.
- Juma ana mkono wa birika=yeye ni mcoyo/mroho/bahiri.
- Kukata mitaa=Kutembea mitaani.
- Kulala fofofo=Kulala sana na kusahau kwenda kazini.
- Kufyata mkia=Kuogopa.
- Kuaga dunia=Kufa.
- Kujifungua=Kupata mtoto, kuzaa.
- Tumbo moto=Kuwa katika hali ya wasiwasi.
- Chungu nzima=-ingi sana.
- Kuvimba=Kukasirika.
- Kujiona=Kulinga.
- Kuvaa miwani=kuwa mtungi=Kuiandika tarakimu naane=Kulewa pombe.
- Kumpaka mtu matope=Kuongea vibaya juu ya mtu.
- Kuona cha mtema kuni=Kujuta, kupata shida.
- Kutoka=Kutakata=Kuvaa vizuri.
- Kuvunja ungo=Kuwa mwanamwali, kigori.
- Kupata kitanda=kulazwa hospitalini.
- Siku nenda rudi=Siku nyingi.
- Kupata jiko=Kuoa.
- Kumtoa mtu kijasho=Kumbabaisha mtu.
- Mfuko umetoboka=Kutokuwa nafedha.
- Hiyo ni mboga=Jambo rahisi.
- Kuponda raha=Kufurahi.
- Kwenda kujisaidia=Kwenda uani=Kwenda choo.
- Kwenda haja ndogo=Kwenda kukojoa.
- Kwenda haja kubwa=Kwenda kunya.
- Kaa chonjo=Tafadhari.
- Kuwa pete na kidole=Kuwa marafiki sana.
- Mbabe=Shupavu.
- Mzito=Mtu mwenye mali au madaraka.
- Kufunga majani=Kuwa na noti nyingi.
- Lugha chafu=Lugha mbaya.
- Kuwa mja mzito=Kuwa na mimba.
- Kutia chumvi=Kuongeza maneno zaidi ya yaliyokuwepo kwa kuchonganisha.
- Avya muye=Toa hasira au ghadhabu.
- Mbuzi=mtu ovyo
- Akina yaye=Mtu duni
- Kuchungulia kabuli=Kuwa mgonjwa mahututi, karibu kufa.
- Kufa kupona=Kwa kila hali.
- Kumezea mate=Kutamani kitu sana.
- Pua na mdomo=Kuwa karibu sana.
- Kupekua=Kutembea bila kuvaa viatu.
- Kuvimba=Kukasirika.
- Kula njama=Kufanya mpango wa siri wa kumfanyia mtu mabaya.
- Kupiga ubwana=Kukaa bila kufanya kazi wakati wa kazi.
- Kumwaga unga=Kupigwa kalamu=Kufukuzwa kazini.
- Kupana mwili=Kunenepa.
- Kwenda mwayo=Kupiga mwayo.
- Kwenda kombo=Kuwa nje ya mstari, mambo kuwa katika hali isiyo nzuli.
- Kwenda chafya=Kupiga chafya.
- Kuona cha mtemakuni=Kujuta, kuwa na shida ya jambo fulani.
- Mbavu za mbwa=Nyumba lilyojengwa kwa miti bila kukandikwa sawa.
- Kigingi=Taniboi.
- Kufunga mdomo=Kunyamaza.
- Hana masikio=Hatii
- Kuchongewa na ulimi=Kuponzwa na mambo yako mwenyewe.
- Kuvunja uso=Kuaibisha.
- Kupiga moyo konde=Kujipa moyo.
- Kupiga shabaha=Kulenga.
- Kupiga umalidadi=Kuvaa vizuri sana.
- Kutega sikio=Kusikiliza kwa makini.
- Kuyatia maneno sikioni=Kuyazingatia maneno.
- Kula miaka=Kufungwa kwa miaka mingi.
- Kujaa farafara=Kujaa tele, mpaka juu.
- Kwenda kapa=Kwenda kwa mikono mitupu.
- Kichwa tupu=Kutokuwa na akili.
- Kupiga swata=kutofanikiwa
- Kupiga domo=kuzungumza bila kufanya kazi
- Kushusha moyo=kukata tama
- Kushupaza moyo=kujipa nguvu
- Kula mwata =kupata taabu
- Kushuika taliki =kushika njia na klwenda
- Kuyoyoma=kwenda bila mpango
- Kakarakakara=hali ya kuwa katika mkukuriko, mshughulikohuku na huku
- Kukurukakara=tendo au hali ya kushughulika, kuhangaika, kubumburisha.
Toa maana ya nahau hizi :
- Kuvunja ungo
- Kumezea mate
- Kufa kupona
- Kumpaka mtu matope
- Kupiga soga
- Kuwa mja mzito
- kuvaa miwani
- Kutia chumvi
- Kuona cha mtemakuni
- Kufyata mkia
Mwl Maeda