08-01-2021, 06:01 PM
Sitiari
Joka la mdimu hulinda watundao
Mandhari/mazingira k.m. kilimo.
Inarejelea vitu gani? K.m. Hindi ndiko kwenye nguo na waendao uchi wapo.
- Mgeni ni kuku mweupe.
- Ahadi ni deni.
- Upweke ni uvundo.
- Mgeni ni kuku mweupe.
- Ujana ni moshi.
- Mapenzi ni kikohozi.
- Kukopa arusi kulipa matanga.
- Kawaida ni kama
- Riziki kama ajali ijapo huitambui.
- Usilolijua ni kama usiku wa giza.
- Ufalme kama mvua hupiga na kupita.
- Siri ya mtungi muulize kata.
- Paka akiondoka panya hutawala.
- Jembe halimtupi mkulima.
- Ukupigao ndio ukufunzao.
- Adhabu ya kaburi aijuaye maiti.
- Haba na haba hujaza kibaba.
- Chovya chovya humaliza buyu la asali.
- Hauchi hauchi unakucha.
- Hayawi hayawi huwa.
- Mtoto wa nyoka ni nyoka.
- Bandu bandu huisha gogo.
- Pilipili usiyoila yakuwashiani?
- Angurumapo samba mcheza ni nani?
- Wameshindwa wenye pembe seuze wewe kipara?
- Simba mla watu akiliwa huwani?
- Mzigo uko kichwani, kwapa lakutokeani jasho?
- Mavi usiyoyala wayawingiani kuku?
- Mla ni mla leo mla jana kalani?
- Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
- Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
- Mtupa jongoo hutupa na ung`ong`o wake.
- Angeenda juu kipungu hafikii mbingu.
- Mzigo wa mwenzio ni kanda la sufi.
- Maji ya kifuu bahari ya chungu.
- Usipoziba ufa utajenga ukuta.
- Chururu si ndondondo!
- Ndo! Ndo! Hujaza ndoo.
- Kiliacho pa kijutie.
- Bara Hindi ndiko kwenye nguo na waendao uchi wapo.
- Kwenye miti hakuna wajenzi.
- Asante ya punda ni mateke.
- Kigumba kwa nguruwe kwa binadamu ki uchungu.
- Kikiharibika cha fundi kikiongoka cha bwana Sudi.
- Umekuwa mung`unye waharibikia ukubwani.
- Hawi Musa kwa kubeba fimbo.
- Ucha Mungu si kilemba cheupe.
- Kichwa cha kuku hakistahili kilemba.
- Kichwa cha nyoka hakibandikwi mtungi.
Joka la mdimu hulinda watundao
- Mtu mwovu huwanyima wengine vitu asivyovihitaji.
- Kupanda mchongoma kushuka ndio ngoma
- Ni rahisi kujitia katika matata kuliko kujitoa.
- Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
- Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
- Wagombanao ndio wapatanao.
- Ukupigao ndio ukufunzao.
- Kuinamako ndiko kuinukako.
- Mwenye kelele hana neno.
- Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
- Tamaa mbele mauti nyuma.
- Mpanda ngazi hushuka.
- Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi.
- Kuainisha methali kutokana na matumizi ya lugha ni kusema mbinu ambazo imetumia.
Mandhari/mazingira k.m. kilimo.
- Ukipanda pantosha utavuna pankwisha.
- Jembe halimtupi mkulima.
- Maudhui k.m. ulezi
- Maudhui k.m. ulezi
- Samaki mkunje angali mbichi.
- Mcha mwana kulia hulia yeye
- c) fani/tamathali k.m. takriri
- Haba na haba hujaza kibaba
- Mtoto wa nyoka ni nyoka.
- d) Jukumu k.m. kuonye
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
- Ukiambiwa jiambie usijeishia kumbe.
- Maana k.m. sawa
- Haraka haraka haina baraka.
- Polepole ndio mwendo.
- Haraka haraka haina baraka.
- Maana k.m. sawa
Inarejelea vitu gani? K.m. Hindi ndiko kwenye nguo na waendao uchi wapo.
- Nchi-Hindi
- Vitu-nguo
- Watu-waendao uchi
- Inakupa wazo gani kuhusu jamii husika?
- Utamaduni na njia za kiuchumi.
Mwl Maeda